Monday, June 24, 2013

RAMBIRAMBI MSIBA WA MATHIAS KISSA

Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Cosmopolitan na Taifa Stars, Mathias Kissa (84) kilichotokea leo alfajiri (Juni 24 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani enzi zake, Kissa akiwa na timu ya Tabora alitamba katika michuano ya Kombe la Taifa wakati huo ikiitwa Sunlight Cup. Alikuwa akicheza katika nafasi ya ulinzi.

Baadaye alijiunga na Cosmoplitan ya Dar es Salaam, na pia kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ambapo enzi zake akiwa na wachezaji kama Yunge Mwanansali wakiiwakilisha Tanganyika na baadaye Tanzania Bara walitamba katika michuano ya Kombe la Chalenji wakati huo ikiitwa Gossage, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

Kissa ambaye alipata tuzo ya mchezaji bora wa karne kwa upande wa Tanzania, tuzo inayotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) alikuwa ndiye mchezaji msomi kupita wote wakati akichezea timu ya Taifa akiwa amehitimu elimu ya Darasa la Kumi.

Kwa mujibu wa binti yake, Erica, marehemu ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alioupata miaka mitano iliyopita, na kisukari. Baadaye alipata kidonda ambacho ndicho kilichosababisha kifo chake.

Msiba uko nyumbani kwa marahemu, Masaki, Mtaa wa Ruvu karibu na Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST). Maziko yatafanyika keshokutwa, Jumatano (Juni 26 mwaka huu) kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kisa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Cosmopolitan na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Kisa mahali pema peponi. Amina

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

TYSON AFUZU MBIO ZA DUNIA BAADA YA KUTUMIA SEKUNDE 19.74

Mwanariadha nyota wa Marekani, Tyson Gay amefanikiwa kufuzu kushiriki mbio za mita 200 za duniani zitakazofanyika jijini Moscow kwa kutumia muda wa sekunde 19.74 ambao ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Gay ambaye ni bingwa wa dunia wa mwaka 2007, sasa atachuana na mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani kutoka Jamaica, Usain Bolt katika mbio za mita 100 na 200 kwenye mashindano ya dunia yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi Agosti mwaka huu. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka aliwashinda Isiah Young aliyeshika nafasi ya pili na Curtis Mitchell alishika nafasi ya tatu. Kwa upnde wa wanawake mwanadada nyota katika mbio fupi kutoka Marekani Allyson Felix alishindwa kutamba kwenye mbio za mita 200 baada kushindwa na Kimberlyn Duncan.

ARSHAVIN SASA AFIKIRIA KURUDI ALIPOTOKA KISOKA CLUB YA "ZSP"

Baada ya kuitumikia Arsenal kwa muda wa miaka mitano nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Urussi, Andrei Arshavin anategemewa kukamilisha taratibu za kurejea klabu yake ya zamani ya Zenit Saint PetersburgKlabu hiyo ndio ilimuwezesha arshavin mwenye miaka 32 akiwa kinda kabla ya Arsenal kumuona na kumyakuwa. aidha Arshavin ambaye alikaa Zenit kwa mkopo kwa muda wakati wa msimu wa pili wa 2011-2012 kwa sasa yuko huru baada kuachwa na Arsenal mwishoni mwa msimu huu. hata hivyo nyotahuyo ni moja kati ya wachezaji waliokuwemo katika kikosi cha Zenit kilichonyakuwa taji la Europa League mwaka 2008 na pia katika kikosi cha Urusi kkilichoshiriki michuano ya Ulaya 2008 kabla ya kwenda Arsenal.

SUAREZ AWEKA REKODI YA KUWA MCHEZAJI ALITUPIA MABAO MENGI NA TIMU YA TAIFA.

MSHAMBULIAJI Mahiri wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao waliibigiza Tahiti kwa mabao 8-1. Nyota anayekipiga katika klabu ya Liverpool ya Uingereza alifunga bao lake la 35 na 36 na kumpita mchezaji mwenzake wa nchi hiyo Diego Forlan wakati timu hiyo ilipokata tiketi ya kucheza nusu fainali dhidi ya wenyeji Brazil Jumatano huko Belo Horizonte. Mabao mengine ya Uruguay katika mchezo huo yalifungwa na Abel Hernandez aliyefunga manne huku Diego Perez na Nicolas Lodeiro wakifunga bao moja kila mmoja na kupelekea Tahiti chovu kuaga mashindano hayo na mzigo wa magoli 24 ya kufungwa. Uruguay ilitinga uwanjani bila kuwaanzisha nyota wake kama Forlan, Edinson Cavani na Suarez ambaye aliingia kipindi cha pili kwa ajili ya kuwapumzisha kwa ajili ya mchezo wa Jumatano.

FIFA YASEMA RAVSHAN AKIRI KUWAPA ITALY BAO LA PILI-KOMBE LA MABARA

SHIRIKISHO la Soka Dunia-FIFA limedai kuwa mwamuzi Ravshan Irmatov amekiri kuwapa Italia bao la pili kwa makosa wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya timu hiyo na Brazil ambao ndio wenyeji hao walitoa dozi ya mabao 4-2. Mabao hayo yalitiwa kimianina Giorgio Chiellini.
aidha bao hilo lilikubaliwa ingawa mwamuzi alishapuliza filimbi kuashiria penati kwenda kwa Italia kitendo ambacho kiliwaudhi wachezaji wa Brazil na kuzonga mwamuzi juu ya uwamuzi wake huo. FIFA imesema kuwa mwamuzi huyo wa Uzbekstan baadae alikiri kufanya kosa hilo na kukiri kupuliza filimbi kuashiria penati. Lakini pamoja na kukiri kutenda kosa kwa mwamuzi huyo FIFA hawajathibitisha kama watamrudisha nyumbani au ataendelea kuchezesha mechi za nusu fainali ya michuano hiyo.

JE?UNAMFAHAMU KWA UZURI DAVID SILVA KATIKA ULIMWENGU WA SOKA TAFAKARI ZAIDI".

             DAVID SILVA
David Silva Euro 2012 vs France 01.jpg
Taarifa kuhusu yeye
Full nameDavid Josué Jiménez Silva
Date of birth8 January 1986 (age 27)
Place of birthArguineguín, Spain
Height1.70 m (5 ft 7 in)
Playing positionAttacking midfielder / Winger
Taarifa kuhusu club
Current clubManchester City
Number21
Timu za Ujana
1995–2000UD San Fernando
2000–2003Valencia
Timu za Ukubwa
Mwaka   TimuMechiGoli
2003–2004Valencia B14(1)
2004–2010Valencia119(21)
2004–2005 Eibar (mkopo)35(4)
2005–2006Celta Vigo (mkopo)34(4)
2010–Manchester City103(14)
Timu ya Taifa
2001–2002Spain U166(2)
2002–2003Spain U1720(5)
2004–2005Spain U1914(5)
2005Spain U205(4)
2004–2006Spain U219(7)
2006–Spain74(20)
David Josué Jiménez Silva alizaliwa 8 Januari 1986 Arguineguín huko Las Palmas Hispain ni mchezaji mpira mhispania ambaye kwa sasa anachezea timu ya Man city na timu ya taifa ya Uhispania.Silva ana uwezo wa kucheza upande wowote au kama namba 10  na wakati mwingine kama mshambulizi msaidizi.Ni mchezaji mwenye mwili mdogo, na mara nyingi hulinganishwa na Aimar Pablo, alipochukua nafasi yake huko Valencia, akivalia nambari iliyohusishwa sana na Aimar; namba 21.
WASIFU WA KLABU
Silva alianza kucheza mpira wa kulipwa msimu wa 2004-05 katika Ngazi ya pili katika timu ya SD Eibar, akiwa amekopwa kutoka Valencia CF na alicheza mechi 35 katika daraja hilimna kufunga mabao matano.Msimu uliofuatia, alikopwa tena, lakini wakati huu alikopwa na timu ya Celta de Vigo, ambapo alicheza mechi 34, na kufunga mabao manne. 
Baada ya kucheza mechi mbili ambazo aliingia uwanjani katika dakika za mwisho za mechi hizo, ambapo mechi ya kwanza iliisha kwa Celta de Vigo kushinda 2-0 nyumbani dhidi ya Malaga CF tarehe 28 Agosti 2005.
Silva akamaalizia msimu huo kama mshambulizi bora huku timu hii ya Kigalisia ikifuzu katika kombe la UEFA moja kwa moja kutoka daraja la pili.Katika misimu miwili, alikosa kucheza mechi sita tu ilhali alifunga mabao 14 (bao la kwanza alilifunga tarehe 5 Novemba 2006 katika tasa ya 1-1 ugenini RCD Espanyol). Baada ya kutocheza kwa muda wa miezi mitatu kutokana na jeraha la kisigino ambapo alifanyiwa upasuaji,
Silva alirejea kikosini katikati mwa Desemba.Silva aliwakilishwa Uhispania akiwa na Cesc Fabregas mara ya kwanza mwaka wa 2003 katika michezo ya ubingwa duniani ya FIFA ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 huko Finland, ambapo alifunga mabao matatu.
Mwaka wa 2006, alijiunga na timu ya Uhispania ya wachezaji wasiozidi umri wa 21 na alifunga mabao manne katika kombe la vijana duniani la FIFA mwaka 2005; hii ilimwezesha kunyakua nafasi ya 4 katika orodha ya wafungaji bora, pamoja na mshambulizi mwitaliano Graziano Pellè.
WASIFU WA TIMU YA TAIFA
Silva alichezea mara ya kwanza timu kuu ya Uhispania tarehe 15 Novemba 2006 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Romania ambapo timu yake ilishindwa 1-0 nyumbani. Aliendelea kutajwa katika orodha ya timu ya Uhispania baada ya kuchangia vizuri katika mechi zake za kwanza.
Tarehe 22 Agosti 2007, Silva aliifungia Uhispania mabao yake ya kwanza kikosini mwa Uhispania, na alifunga mara mbili katika mechi hiyo ambapo waliishinda Ugiriki 3-2 katika mechi ya kirafiki.
Baadaye aliitwa ajiunge na kikosi cha wachezaji 23 ambao wangeiwakilisha nchi yao katika dimba la Euro 2008.
Katika nusu fainali Silva alifunga bao la tatu la Uhispania dhidi ya Urusi baada ya ushambulizi wa haraka ambayo Cesc Fabregas alimpigia krosi Silva, ambaye alitia mpira ndani ya lango la Igor Akinfeev kwa kutumia mguu wake wa kushoto.
Katika fainali, Silva alihusika katika tukio fulani na mjerumani Lukas Podolski. Baada ya kumvuta Podolski chini, Podolski alimwenedea Silva na kuzua ubishi mkali ambao haukuadhibiwa na mwamuzi.
Muda mfupi baadaye, kocha wa timu ya Uhispania, Luis Aragonés, alimwondoa Silva na kuleta Santi Cazorla ili kuzuia wezekano la vita.

NIGERIA YATUPWA NJE KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA MABARA 3-0

Timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles ambao ni mabingwawa Afrika katika michuano ya CHAN  imeondolewa kwenye michuano ya kombe la mabara baada ya kutandikwa mabao 3-0 na mabingwa wa dunia Hispania. Mabao mawili ya beki wa klabu ya Barcelona, Jordi Alba na moja la mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres yalitosha kuisambaratisha Nigeria ambao wameshinda mechi moja pekee dhidi ya Tahiti wikiendi iliyopita. Nigeria wameyaaga mashindano hayo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi B wakiwa na pointi tatu nyuma ya Uruguay walioko kwenye nafasi ya pili wakiwa na point sita. Hispania ni vinara wa kundi B wakiwa wamemaliza hatua ya makundi na ushindi wa asilimia mia moja wakiwa na pointi tisa ambapo sasa watakwenda kuwavaa Italia katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo hapo siku ya siku ya alhamisi mjini Fortaleza. Uruguay wao wametoa kipigo cha magoli 8-0 kwa timu chovu kwenye michuano hiyo Tahiti ambao wameondoka na jumla ya magoli 24 ya kufungwa na kupata bao moja pekee walipocheza na Nigeria. Kwa matokeo hayo, Uruguay watacheza nusu fainali dhidi ya wenyeji Brazil, hapo siku ya jumatano.
MATOKEO
Uruguay 8
*Abel Mathias Hernandez Dakika ya 2, 24, 45 & 67 [Penati]
*Diego Perez 27
*Nicolas Rodiero 62
*Luis Suarez 82 & 88
     vs 
Tahiti 0
>>>>>
Spain 3
    vs
Nigeria
>>>>>
Nusu fainali
Jumanne Juni 26
Brazil v Uruguay
Muda saa 4 usiku
uwanja:Belo Horizonte
Jumatano Juni 27
Spain v Italy
uwanja Fortaleza
Muda saa 4 usiku
Mshindi wa tatu
Jumapili Juni 30
uwanja Salvador
Saa 1 usiku
Fainali
Jumapili Juni 30
Rio De Janeiro