SHIRIKISHO la Soka la
Ethiopia-EFF limemtimua kibarua katibu mkuu wake baada ya kukiri
kumtumia mchezaji kimakosa katika mechi za kufuzu michuano ya Kombe la
Dunia 2014 hatua ambayo inaweza kuigharimu timu nchi hiyo kukatwa alama
tatu. Kamati ya
Utendaji ya EFF ilipiga kura za kumtimua katibu huyo aitwaye Ashenafi
Ejigu lakini walipinga barua ya kujiuzulu kwa makamu wa rais wa
shirikisho hilo Berhanu Kebede ambaye ndiye alikuwa akilaumiwa kutokana
na mkanganyiko huo. Baadhi
ya wajumbe na waandishi wa habari za michezo waliokuwepo katika mkutano
huo walikuwa wakitaka uongozi mzima wa shirikisho hilo ujiuzulu kwa
kile walichokiita uzembe. Rais
wa EFF, Sahilu Gebremariam alikiri kuwa suala hilo ni la kizembe na
wanapaswa wote kujiuzulu na kudai kuwa atafanya hivyo katika mkutano
mkuu utakaofanyika Septemba mwaka huu. Akihojiwa
kuhusiana na suala la kumchezasha mchezaji aliyepewa kadi mbili za
njano kocha wa Ethiopia Sewnet Bishaw alijitetea kuwa anapokuwa uwanjani
huwa hatumii karatasi na kalamu anachofanya yeye ni kuhakikisha timu
inapata matokeo mazuri.
Tuesday, June 25, 2013
YANGA WAJIPNGA NA MECHI ZA KIRAFIKI
Mabingwa wa soka Tanzania Bara , Afrika Mashariki
na Kati, Klabu ya Dar Young Africans watacheza mechi za kirafiki dhidi
ya Rayon Sport ya Rwanda Julai 6 na 7, mwaka huu katika sehemu ya ziara
yake ya kulitembeza Kombe lake la ubingwa wa Ligi Kuu mikoa ya kanda ya
Ziwa inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake,
Kilimanjaro Premeum Lager.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa kaimu katibu mkuu wa Yanga Lawrence
Mwalusako , Yanga maarufu kama Kwalalumpa Malysia itaondoka Dar es
Salaam Julai 5, siku mbili tu baada ya kuanza mazoezi Uwanja wa
sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam kuelekea Mwanza tayari kwa
mchezo wa kwanza dhidi ya mabingwa hao wa zamani wa Afrika Mashariki na
Kati, Uwanja wa CCM Kirumba, Julai 6.
Baada
ya kipute hicho, Julai 7, timu hizo ambazo zimewahi kufundishwa na
kocha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Raoul Jean Pierre
Shungu kwa wakati tofauti na kwa mafanikio, zitarudiana kwenye Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga.
“Yanga
tuna mipango mingi sana, bahati mbaya tumeshindwa kwenda Sudan kutetea
ubingwa wetu wa Kagame, lakini bado tuna michuano mikubwa barani Afrika,
ikiwa ni heshima kwa mashabiki wetu na wanachama wanaotuunga mkono, ni
nafasi yao kuliona taji letu la ligi msimu uliopita, tutapita mikoani na
kushangilia pamoja”. Alisema Mwalusako.
Baada ya hapo , Yanga SC
wataelekea mjini Tabora, kucheza mechi nyingine na wenyeji, Rhino FC
waliopanda Ligi Kuu msimu huu Julai 11, mwaka huu Uwanja wa Ally Hassan
Mwinyi.
Katika
ziara hizo, Yanga watatembeza Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu,
walilolitwaa kwa mara ya 24 msimu huu kwenye mitaa mbalimbali
kushangilia na mashabiki wao.
Yanga
SC, imekuwa na mafanikio makubwa tangu ianze kudhaminiwa na TBL mnamo
2008, ikitwaa jumla ya mataji sita katika kipindi hicho, yakiwemo mawili
ya Kagame, 2011 na 2012 na manne ya Ligi Kuu Bara, 2008, 2009, 2011 na
2013.
Agosti 2, mwaka 2011, TBL ilisaini Mkataba wa udhamini na Yanga wa miaka minne sawa na kwa watani wao pia, Simba SC.
Katika
mkataba huo mpya, uliotiwa saini kwenye hoteli ya Double Tree, Masaki,
Dar es Salaam, TBL iliongeza dau la fedha za mishahara kwa wachezaji
kutoka Sh. Milioni 16 hadi Milioni 25 kwa mwezi, ikaongeza basi moja
kubwa, Yutong lenye uwezo wa kubeba abiria 54 na fedha kwa ajili ya
kugharamia mikutano ya wanachama ya kila mwaka Sh. Milioni 20 kugharamia
tamasha la mwaka la klabu na vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh.
Milioni 35 kila msimu.
Yanga pia inapewa bonasi ya Sh. Milioni 25 ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu
Bara au Milioni 15, ikishika nafasi ya pili katika Mkataba huo wenye
thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 5 tangu Agosti 8, mwaka huu hadi Julai
31, mwaka 2016.
TETESI ZA MASTAA NA KITUO CHA REDIO CHA NAPOLI MARTE-CAVANI
KITUO
cha Redio cha Napoli, Marte kimetangaza kuwa dau la Pauni Milioni
49.3 limetolewa na Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji Edinson Cavani
ambaye muda wote anampasua kichwa mmiliki wa klabu ya Chelsea Bilionea
Roman Abramovich mwenye lengo la kuimarisha kikosi chake chini ya kocha
Jose Mourinho.
Katika
taarifa ya jana usiku, Radio Marte ilitangaza: “Tumepokea taarifa
kutoka ofisini kwa vyanzo vya kuaminika kwamba, Napoli imekubaliana dili
la kuiuzia Chelsea Cavani.
Kitu moto: Chelsea sasa ipo katika nafasi ya kumnasa Edinson Cavani
“Rafa
Benitez pia amebariki, lakini kabla ya kutangaza rasmi, Napoli inataka
kupata mshambuliaji atakayeziba pengo la Il Matador.
“Aurelio De Laurentiis”, klabu itasomba kiasi cha Euro Milioni 58, sawa na dili la Ezequiel Lavezzi kwenda PSG mwaka jana.
“Mchezaji huyo atajiingizia mshahara wa Euro Milioni 8.5 kwa msimu pamoja na haki za picha,”. Habari zimevuja kama kwamba Cavani
ametangaza anataka kukutana uso kwa uso na Rais, Aurelio de Laurentiis
na kuna taarifa kwamba Manchester United nayo imo kwenye mbio hizo.
Mshambuliaji
huyo wa Uruguayna baba yake awali walionyesha nia ya kutaka kwenda Real
Madrid. Klabu hiyo ya Hispani iliwasiliana na Napoli, lakini sasa
itabidi waipiku ofa iliyotolewa na Chelsea.
Monday, June 24, 2013
RAMBIRAMBI MSIBA WA MATHIAS KISSA

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani enzi zake, Kissa akiwa na timu ya Tabora alitamba katika michuano ya Kombe la Taifa wakati huo ikiitwa Sunlight Cup. Alikuwa akicheza katika nafasi ya ulinzi.
Baadaye alijiunga na Cosmoplitan ya Dar es Salaam, na pia kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ambapo enzi zake akiwa na wachezaji kama Yunge Mwanansali wakiiwakilisha Tanganyika na baadaye Tanzania Bara walitamba katika michuano ya Kombe la Chalenji wakati huo ikiitwa Gossage, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
Kissa ambaye alipata tuzo ya mchezaji bora wa karne kwa upande wa Tanzania, tuzo inayotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) alikuwa ndiye mchezaji msomi kupita wote wakati akichezea timu ya Taifa akiwa amehitimu elimu ya Darasa la Kumi.
Kwa mujibu wa binti yake, Erica, marehemu ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alioupata miaka mitano iliyopita, na kisukari. Baadaye alipata kidonda ambacho ndicho kilichosababisha kifo chake.
Msiba uko nyumbani kwa marahemu, Masaki, Mtaa wa Ruvu karibu na Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST). Maziko yatafanyika keshokutwa, Jumatano (Juni 26 mwaka huu) kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kisa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Cosmopolitan na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Kisa mahali pema peponi. Amina
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
TYSON AFUZU MBIO ZA DUNIA BAADA YA KUTUMIA SEKUNDE 19.74
Mwanariadha nyota wa Marekani, Tyson Gay amefanikiwa kufuzu kushiriki mbio za mita 200 za duniani zitakazofanyika jijini Moscow kwa kutumia muda wa sekunde 19.74 ambao ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Gay ambaye ni bingwa wa dunia wa mwaka 2007, sasa atachuana na mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani kutoka Jamaica, Usain Bolt katika mbio za mita 100 na 200 kwenye mashindano ya dunia yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi Agosti mwaka huu. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka aliwashinda Isiah Young aliyeshika nafasi ya pili na Curtis Mitchell alishika nafasi ya tatu. Kwa upnde wa wanawake mwanadada nyota katika mbio fupi kutoka Marekani Allyson Felix alishindwa kutamba kwenye mbio za mita 200 baada kushindwa na Kimberlyn Duncan.
ARSHAVIN SASA AFIKIRIA KURUDI ALIPOTOKA KISOKA CLUB YA "ZSP"
SUAREZ AWEKA REKODI YA KUWA MCHEZAJI ALITUPIA MABAO MENGI NA TIMU YA TAIFA.
MSHAMBULIAJI Mahiri wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao waliibigiza Tahiti kwa mabao 8-1. Nyota anayekipiga katika klabu ya Liverpool ya Uingereza alifunga bao lake la 35 na 36 na kumpita mchezaji mwenzake wa nchi hiyo Diego Forlan wakati timu hiyo ilipokata tiketi ya kucheza nusu fainali dhidi ya wenyeji Brazil Jumatano huko Belo Horizonte. Mabao mengine ya Uruguay katika mchezo huo yalifungwa na Abel Hernandez aliyefunga manne huku Diego Perez na Nicolas Lodeiro wakifunga bao moja kila mmoja na kupelekea Tahiti chovu kuaga mashindano hayo na mzigo wa magoli 24 ya kufungwa. Uruguay ilitinga uwanjani bila kuwaanzisha nyota wake kama Forlan, Edinson Cavani na Suarez ambaye aliingia kipindi cha pili kwa ajili ya kuwapumzisha kwa ajili ya mchezo wa Jumatano.
Subscribe to:
Posts (Atom)