Friday, June 28, 2013

WAWILI WALA SHAVU WACHAGULIWA KITUO CHA VIPAJI ASPIRE

Wachezaji wawili kutoka Tanzania wamechaguliwa miongoni mwa 50 waliofanyiwa majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) kilichoko Doha nchini Qatar kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream.
Abdulrasul Tahir Bitebo (15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa Karume, na Martin Omela Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka Tanzania kuingia katika kituo ambapo watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini mkataba rasmi wa kuendelezwa.

Wachezaji wengine walikuwa wakitoka katika nchi za Uganda na Kenya. Mchezaji mwingine aliyefuzu katika nafasi tatu zilizokuwepo ni kutoka nchini Kenya.

Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani, na kwa hapa nchini uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

TFF ina jumla ya vituo 14 vya kuendeleza vipaji kupitia mpango huo wa Aspire Football Dream. Vituo hivyo ni Karume, Kigamboni, Tandika, Kawe, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Makongo, na Tabata vilivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Vingine ni Bagamoyo kilichopo mkoani Pwani, Morogoro, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kituo kingine cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) cha Aspire kipo Dakar nchini Senegal.

TFF KUENDESHA KOZI SITA KATI YA JULAI- SEPTEMBA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha kozi sita tofauti za mpira wa miguu kati ya Julai na Septemba mwaka huu.

Kozi hizo ni FIFA 11 For Health itakayofanyika Hombolo mkoani Dodoma kuanzia Julai 8 hadi 19 mwaka huu. Julai 6 hadi 15 mwaka huu kutakuwa na kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer) itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Waamuzi wa FIFA nao watakuwa na kozi itakayofanyika kati ya Agosti 22 hadi 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati kozi ya ukocha kwa ajili ya Copa Coca-Cola itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Agosti 12 na 17 mwaka huu.

Vilevile kutakuwa na kozi ya mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 itafanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati tamasha (festival) la grassroots litafanyika Uwanja wa Karume, Septemba 14 mwaka huu.

RCL KUKAMILISHA HATUA YA NNE JUMAPILI
Mechi za marudiano za hatua ya nne ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zitachezwa Jumapili (Juni 30 mwaka huu) kwenye viwanja vya Sokoine jijini Mbeya, na Kambarage mjini Shinyanga.

Friends Rangers ya Dar es Salaam ambayo katika mechi ya kwanza ilifungwa nyumbani mabao 3-0 itakuwa mgeni wa Stand United FC mjini Shinyanga wakati Kimondo SC itaikaribisha Polisi Jamii ya Mara jijini Mbeya. Katika mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

Hatua ya mwisho ya RCL itachezwa Julai 3 mwaka huu kwa mechi za kwanza wakati zile za marudiano zitafanyika Julai 7 mwaka huu. Timu tatu za kwanza zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MAN UNITED USO KWA USO NDANI YA EVERTON WATAKA KUIBOMOA

Mabingwa wa BPL msimu uliopita Club ya soka ya Manchester United imeamua kumtengea kitita cha paundi milioni 15 kwa ajili ya kumnasa beki wa Everton, Leighton Baines. Baada ya kukataa ofa ya awali ya United ya Pauni Milioni 12, Everton imesisitiza kuwa beki huyo wa kushoto wa kimataifa wa England hauzwi. Lakini United imepania kupanda dau hadi paundi milioni 20 katika kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. Mrithi wa Moyes, Everton, Roberto Martinez anataka kumbakzia beki huyo na klabu hiyo inataka kumpa mkataba mpya ikimuongezea mshahara hadi paundi 70,000 kwa wiki. Mpango huu unamuweka shakani beki Mfaransa, Patrice Evra juu ya mustakabali wake Old Trafford na wazi sasa anaweza kuhamia Monaco au Paris Saint-Germain.

WAMSHANGAA MESSI BAADA YA KUTUA NCHIN SENEGAL-WAKANYAGANA

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi ametua nchini Senegal jana kwa ndege binafsi na kulakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Dakar na mashabiki wa soka na vijana wadogo waliotoka pembe mbalimbali za nchi hiyo. Nyota huyo anayecheza katika klabu ya Barcelona alialikwa na shule ya soka ya Qatar Aspire ambao wana tawi lao nchini humo kwa ajili ya kwenda kwenye kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria. Kwa mujibu wa waratibu ya ziara hiyo maelfu ya neti ambazo zitakuwa na picha ya Messi zitasambazwa kwa watoto na familia katika vijiji mbalimbali nchini humo. Messi atasafiri kwa helikopta kwenda Saly eneo la karibu na mji wa Dakar ambapo atatembelea nyumba za yatima na kuongea na wenyeji wa hapo jinsi watakavyoweza kujikinga na malaria.

HISPAIN YATINGA FAINALI SASA KUUMANA NA WENYEJI BRAZIL

Close shave: Spain moved through to the Confederations Cup final after beating Italy on penalties in FortalezaTimu ya taifa ya hispain imefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuitooa Italia katika Kombe la Mabara kwa ushindi wa matuta wa 7-6 mjini Fortaleza, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 katika mchezo wa Nusu Fainali usiku huu.
Wataliano walifungwa na Waspanyola katika Fainali ya Euro mwaka jana wameshindwa kulipa kisasi na sasa Fainali ya michuano hiyo mwaka huu Jumapili Uwanja wa Maracana, itawakutanisha wenyeji La Roja na Brazil wenyeji.
Leonardo Bonucci wa Italia alikosa moja ya penalti 14 na Jesus Navas akaweka nyavuni mkwaju wa mwisho na kuipeleka Hispania Fainali.
 TUTAFAKARI KUELEKEA FAINALI JE NANI KUIBUKA NA UBINGWA"
USO KWA USO
JUMLA: Mechi 8
USHINDI: Brazil 4 Spain 2
SARE: 2
MAGOLI JUMLA: Brazil 11 Spain 8
Mechi zenyewe:
FIFA KOMBE LA DUNIA:
Jumla: Mechi 5
USHINDI: Brazil 3 Spain 1
SARE: 1
MAGOLI JUMLA: Brazil 10 Spain 5
1986  Spain 0 Brazil 1 {Guadalajara, Mexico}
1978  Brazil 0 Spain 0 {Mar Del Plata, Argentina}
1962  Brazil 2 Spain 1 {Vina Del Mar, Chile}
1950  Brazil 6 Spain 1 {Rio De Janeiro, Brazil}
1934  Spain 3 Brazil 1 {Genoa, Italy}
KIRAFIKI:
Jumla: Mechi 3
USHINDI: Brazil 1 Spain 1
SARE: 1
MAGOLI: Spain 3 Brazil 1
1999  Spain 0 Brazil 0 {Vigo, Spain}
1990  Spain 3 Brazil 0 {Gijon, Spain}
1981  Brazil 1 Spain 0 {Salvador, Brazil}

WAWILI WACHAGULIWA KITUO CHA VIPAJI ASPIRE

Wachezaji wawili kutoka Tanzania wamechaguliwa miongoni mwa 50 waliofanyiwa majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) kilichoko Doha nchini Qatar kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream.
Abdulrasul Tahir Bitebo (15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa Karume, na Martin Omela Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka Tanzania kuingia katika kituo ambapo watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini mkataba rasmi wa kuendelezwa.

Wachezaji wengine walikuwa wakitoka katika nchi za Uganda na Kenya. Mchezaji mwingine aliyefuzu katika nafasi tatu zilizokuwepo ni kutoka nchini Kenya.

Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani, na kwa hapa nchini uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

TFF ina jumla ya vituo 14 vya kuendeleza vipaji kupitia mpango huo wa Aspire Football Dream. Vituo hivyo ni Karume, Kigamboni, Tandika, Kawe, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Makongo, na Tabata vilivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Vingine ni Bagamoyo kilichopo mkoani Pwani, Morogoro, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kituo kingine cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) cha Aspire kipo Dakar nchini Senegal.

TFF KUENDESHA KOZI SITA KATI YA JULAI- SEPTEMBA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha kozi sita tofauti za mpira wa miguu kati ya Julai na Septemba mwaka huu.

Kozi hizo ni FIFA 11 For Health itakayofanyika Hombolo mkoani Dodoma kuanzia Julai 8 hadi 19 mwaka huu. Julai 6 hadi 15 mwaka huu kutakuwa na kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer) itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Waamuzi wa FIFA nao watakuwa na kozi itakayofanyika kati ya Agosti 22 hadi 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati kozi ya ukocha kwa ajili ya Copa Coca-Cola itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Agosti 12 na 17 mwaka huu.

Vilevile kutakuwa na kozi ya mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 itafanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati tamasha (festival) la grassroots litafanyika Uwanja wa Karume, Septemba 14 mwaka huu.

RCL KUKAMILISHA HATUA YA NNE JUMAPILI
Mechi za marudiano za hatua ya nne ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zitachezwa Jumapili (Juni 30 mwaka huu) kwenye viwanja vya Sokoine jijini Mbeya, na Kambarage mjini Shinyanga.

Friends Rangers ya Dar es Salaam ambayo katika mechi ya kwanza ilifungwa nyumbani mabao 3-0 itakuwa mgeni wa Stand United FC mjini Shinyanga wakati Kimondo SC itaikaribisha Polisi Jamii ya Mara jijini Mbeya. Katika mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

Hatua ya mwisho ya RCL itachezwa Julai 3 mwaka huu kwa mechi za kwanza wakati zile za marudiano zitafanyika Julai 7 mwaka huu. Timu tatu za kwanza zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

TENGA ASEMA MKUTANO UPO PALEPALE"-MKUU WA TFF

TFF_LOGO12SHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF, limethibitisha kuwa Mkutano Mkuu wao uliopangwa kufanyika Julai 13 utaendelea licha ya kuwa Siku hiyo hiyo Tanzania inacheza Mechi ya kwanza ya Mchujo ya CHAN dhidi ya Uganda Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Wadau wengi wamekuwa wakihoji kufanyika kwa Mkutano huo wakati Nchi inakabiliwa na Mechi muhimu Siku hiyo hiyo huku wengine wakidiriki kudai kuna walakini ndani yake.
Lakini Rais wa TFF, Leodegar Tenga, amefafanua kuwa vitu hivyo viwili haviwezi kuleta mgongano kwani Mechi itachezwa kwa Dakika 90 na Mkutano Mkuu umepangwa kuwa wa Siku mbili.
Tenga alisema: “Hamna njama zozote. Vitu hivyo viwili vitaendelea kama ilivyopangwa.”
Akifafanua, Tenga alisema Wajumbe wa Mkutano Mkuu wamezoea kujadili Ajenda hadi 12 katika Siku moja lakini safari hii Ajenda ni moja tu na imepangiwa Siku mbili.
Ajenda ya Mkutano Mkuu huo ni kujadili na kupitisha Mabadiliko ya Katiba ili kuruhusu Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo ufanyike kama ilivyoagizwa na FIFA.
Awali Uchaguzi ulikuwa ufanyike hapo Februari 24 lakini ukatokea mgongano mkubwa baada ya baadhi ya Wagombea kufutwa na pia madai kuwa Katiba ilibadilishwa bila kufuata taratibu.
Akifafanua zaidi, Tenga alisema upo uwezekano mkubwa kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu kumaliza Kikao chao kabla hata Mechi kuchezwa.
Katika Uchaguzi wa awali Tenga hakuwa Mgombea wa nafasi yake.

Thursday, June 27, 2013

FEDERER ASEMA BADO ATAENDELEA KUCHEZA MCHEZO HUO".

Mchezaji tenesi mahiri wa Switzerland, Roger Federer amesisitiza kuwa bado ataendelea kucheza mchezo huo kwa miaka mingi ijayo pamoja na kutolewa mapema katika michuano ya Wimbledon jana. Nyota huyo ambaye anashika namba tatu katika orodha za ubora duniani amesema hana hofu yoyote pamoja na kutolewa na Sergiy Stakhovisky wa Ukraine katika mzunguko wa pili wa michuano hiyo. Katika mchezo huo Federer aliburuzwa kwa kufungwa 6-7 7-6 7-5 7-6 na Stakhovsky anayeshika namba 116 katika orodha za ubora duniani. Baadhi ya wadau wa mchezo huo wamekuwa wakihoji kiwango cha Federer mwenye umri wa miaka 31 na kudai kuwa amekwisha lakini mwenye amesisitiza kuwa bado yuko fiti na ataendelea kucheza kwa miaka kadhaa ijayo. Kwa upande wa wanawake mwanadada nyota anayeshika namba mbili kwa ubora kwa upande wanawake Maria Sharapova wa Urusi naye aliyaaga mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha 6-3 6-4 kutoka kwa Michelle Larcher de Brito wa Ureno anayeshika namba 131 katika orodha hizo.