
Makabidhiano hayo ya Uwanja huo
uliochukua Miaka 7 kujengwa yalifanyika Jana kwa kutia saini na
kubadilishana Vyeti kati ya Balozi wa China Nchini Tanzania, Li Youqing,
na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Sihaba Mkinga.
Akizungumza, Waziri wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella Mukangara, aliishukuru China
kwa msaada wao mkubwa wa Fedha na Ujenzi.
Pia, Waziri Mukangara, alisifu Usimamizi
wa China wa Uwanja huo tangu ujenzi ulipokamilika na tangu Uwanja huo
ulipofunguliwa rasmi hapo Tarehe 25 Februari 2009 na Rais wa zamani wa
China, Hu Jintao, na Rais Jakaya Kikwete.
Uwanja wa Taifa, unaochukua Washabiki
60,000 wote wakiwa Vitini, umegharimu Shilingi Bilioni 56 na kati ya
hizo China ilitoa Bilioni 33.4 na Tanzania ilitoa Fedha zilizobaki.
Uwanja huu ni wa kisasa na upo katika Viwango vinavyokubalika na FIFA na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki.
Serikali imedokeza kuwa hivi sasa wapo
kwenye mazungumzo ya kutafuta Fedha ili kugharamia Ujenzi wa Awamu ya
Pili na inatarajiwa Serikali ya China itahusishwa na pia Mkandarasi
aliejenga Awamu ya Kwanaza, Beijing Construction Engineering Company
Limited, ndio watashughulikia Awamu hii.
Baada ya kukamilika kwa Ujenzi wa Awamu
ya Pili, Tanzania itakuwa iko tayari kuwa Mwenyeji wa Mashindano makubwa
ya Michezo ya kila aina.