Sunday, July 7, 2013

MARION AFANIKIWA KUTWAA TAJI LA KWANZA LA MICHUANO YA GRAND SLAM.

Marion Bartoli mwanadada nyota katika tenisi,  amefanikiwa kushinda taji lake la kwanza la michuano ya Grand Slam baada ya kumchalaza Sabine Lisicki wa Ujerumani kwa seti 6-1 6-4 kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Wimbledon. Bartoli ambaye anashika namba 15 katika orodha za ubora kwa upande wanawake alitumia dakika 30 pekee kushinda seti ya kwanza wakati mpinzani wake Lisicki akionekana kushindwa kumudu vishindo katika fainali yake ya kwanza ya Grand Slam. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Bartoli amesema haamini kama amenyakuwa taji hilo na alikuwa akijisikia kucheza kwa kiwango chake cha juu huku kila kitu alichofanya kikimuendea sawa. Michuano hiyo inaendelea tena baadae kwa mchezo wa fainali kwa upande wa wanaume ambapo Andy Murray wa Uingereza anayeshika namba mbili katika orodha za ubora atachuana na Novak Djokovic wa Serbia anayeshika namba moja katika orodha za ubora.

HISPAIN YATOLEWA NJE MASHINDANO YA VIJANA FIFA U-20" LEO GHANA VS CHILE

FIFA_WORLD_CUP_U-20_TURKEY_LOGOKatika  mechi ya jana iliyokuwa na upinzani wa hali ya juu kati ya Hispain vs Uruguay "dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa sare ya 0-0 "Ndipo Refa wa mtanange huo akamuru kuongeza dakika  30 za Nyongeza.
Thiago_AlcantaraHivyo katika dakika hizo 30 za nyongeza kunako dakika 103 ya mchezo Felipe Avenatti aliipatia Uruguay bao muhimu la kuongoza kwa njia ya Kichwa"ambapo bao hilo 1-0 limeiwezesha Uruguay kuibwaga Hispain na kufanikiwa kutinga hatua Nusu Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Vijana chini ya Miaka 20, U-20, yanayochezwa huko Nchini Turkey.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
MATOKEO MENGINE"
ROBO FAINALI
France 4 Uzbekistan 0
Magoli:
*Yaya Sanogo (dk31')
*Paul PogbaP (dk35' Penati)
*Florian Thauvin (dk43' Penati)
*Kurt Zouma (dk64')
Uruguay 1 Spain 0
Goli:
*Felipe Avenatti (dk103’)
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Hivyo sasa kwa ushindi huo Uruguay katika hatua ya Nusu Fainali watashuka dimbani kupepetana na Mshindi wa Mechi ya Iraq vs South Korea.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
RATIBA ROBO FAINALI  LE; JULAI 7
[Saa 12 Jioni]
Kayseri
Iraq v South Korea
[Saa 3 Usiku]
Istanbul
Ghana v Chile
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Katika Robo Fainali nyingine iliyochezwa jana Timu ya Taifa ya France ilifanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kuilaza Uzbekistan kwa Bao 4-0 hivyo sasa kwa matokeo hayo France itacheza na Mshindi kati ya Ghana vs Chile.
Bao za France zilifungwa na Yaya Sanogo, Paul Pogba, Florian Thauvin naKurt Zouma.
RATIBA/MATOKEO:
ROBO FAINALI
06/07 France 4 Uzbekistan 0
06/07 Uruguay 1 Spain 0
07/07 muda 18:00 Iraq v South Korea
07/07 muda 21:00 Ghana v Chile
NUSU FAINALI
10/07 18:00 Bursa France vs Ghana or Chile
10/07 21:00 Trabzon Uruguay vs Iraq or South Korea
MSHINDI WA TATU
Tarehe 3/07 18:00  Uwanja Istanbul  Kulingana na matokea
FAINALI
Tarehe 13/07 21:00  Uwanja Istanbul
World Youth Championship{Bingwaaaaaa}
TUKUMBUKE WASHINDI WALIOPITA:
2011  Brazil
2009  Ghana
2007  Argentina
2005  Argentina
2003  Brazil
2001  Argentina
1999  Spain
1997  Argentina
1995  Argentina
1993  Brazil
1991  Portugal
1989  Portugal
1987  Yugoslavia
1985  Brazil
1983  Brazil
1981  Germany
1979  Argentina
1977  U.S.S.R.

BOLT ATUMA SALAMU KWA WAPINZANI WAKE BAADA YA KUIBUKA NA USHINDI.

Usain Bolt Mwanariadha nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica,ametuma salamu kwa wapinzani wake baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi katika mbio za mita 200 za Diamond League zilizofanyika jijini Paris kwa kutumia muda wa sekunde 19.73 ukiwa ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Bolt ambaye anashikilia rekodi ya dunia katika mbio hizo alifabnikiwa mbio kirahisi na kuuzidi muda wa haraka zaidi uliowekwa kwa mwaka huu na Tyson Gay wa Marekani mwezi mmoja kabla ya mashindano ya riadha ya dunia yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi. Akihojiwa mara baada yam bio hizo Bolt amesema anajisikia vyema kwa kushinda mbio hizo lakini bado bado ana kazi ya kufanya kuhakikisha anakuwa katika kiwango chake ifikapo michuano ya dunia. Nafasi ya pili katika mbio hizo ilikwenda kwa Warren Weir wa Jamaica aliyetumia muda wa sekunde 19.92 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Christophe Lemaitre wa Ufaransa aliyetumia muda wa sekunde 20.07.

Thursday, July 4, 2013

ROONEY ATAKIWA KUWA SILISHA BARUA KWA MAN U

MSHAMBULIAJI Wayne Rooney atatakiwa kuwasilisha barua ya maandishi ya kuomba kuondoka ikiwa anataka kuachana na  Manchester United.
Mpachika mabao huyo wa Old Trafford, alirejea mazoezini jana huku mustakabali wake ukiwa bado haueleweki. Imefahamika hakuwa na Mkutano mahsusi na kocha mpya David Moyes juu ya suala lake. 
Hilo linaweza kutokea katika kituo cha mazoezi cha klabu, Carrington leo. Wawili hao walizungumza jana, lakini si kwa muda mrefu na msimamo wa United kwake bado haujabadilika.

Hajielewi: Mustakabali wa Wayne Rooney bao haueleweki licha ya jana kurejea mazoezini
Wamesema mshambuliaji huyo wa England hauzwi. Kuhusu tetesi za wapinzani wao katika Ligi Kuu, Arsenal kutaka rasmi kumsajili tangu wiki iliyopita, United bado haijawasiliana na yoyote anayemtaka Rooney.
Sakata hili linaweza kugeuka tu iwapo mshambuliaji mwenyewe ataamua kulazimisha kuondoka. BIN ZUBEIRY iliandika mwishoni mwa msimu uliopita kwamba, Rooney aliomba kuondoka kwa kocha aliyestaafu, Sir Alex Ferguson.
Ombi la kuondoka litamaanisha Rooney hatadai chochote katika Mkataba wake wa miaka miwili uliobakia ambao alikuwa analipwa Pauni 250,000 kwa wiki.

Moyes, bado anataka kumuongeza katika benchi lake la ufundi, beki wa zamani wa United, Phil Neville na ni matumaini Rooney atakubali kubaki msimu ujao kufanya na kazi na kocha wa zamani wa Everton, aliyeinua kipaji chake Goodison Park.
Huku Moyes akitarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari kwa mara ya kwanza kesho, ufafanuzi utakuja muda si mrefu.

Harudi: Angalau bado, kwa Cristiano Ronaldo
Wakati huo huo, mchezaji mwenzake wa zamani Rooney, Mreno Cristiano Ronaldo ameendelea kuweka wazi juu mapenzi yake na United. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid  amesema jana kwamba anataka kurudi Ligi Kuu, lakini hakusema lini.
"Nalikosa kweli soka la England. Kwangu ilikuwa moja ya miaka bora katika maisha yangu ya soka wakati nipo huko Manchester United. Ni klabu ambayo bado ipo moyoni mwangu. naikosa kweli kweli. Lakini kwa sasa maisha yangu yapo Hispania. Nafurahia kucheza huko pia. Mustakabali hatuwezi kuujua,"alisema Ronaldo.

ISCO ASEMA LENGO KUU NI KUISAIDIA MADRID KUTWAA UEFA

Baada ya kusajiliwa katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi na club ya Real Madrid Isco ametanabaisha na kusama kuwa lengo lake kubwa ni kukisaidia kikosi cha timu hiyo kinachonolewa na kocha Carlo Ancelotti kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Kocha aliyeoondoka Jose Mourinho ameinoa klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu na kuisadia klabu hiyo kufika nusu fainali ya ligi hiyo mara tatu lakini bado wamekuwa na kiu ya muda mrefu ya kulisubiria taji lao 10 katika michuano hiyo. Akijiunga na Madrid kwa mkataba wa miaka mitano kutokea Malaga, Isco sasa ana malengo ya kuiwezesha klabu hiyo kuendeleza historia yake kwa kunyakuwa taji hilo mapema iwezekanavyo. Akihojiwa katika utambulisho rasmi, Isco amesema watu wote wanahusiana na klabu hiyo wamekuwa na kiu ya taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na ni mategemeo yake kwamba msimu unaokuja taji hilo litatua Santiago Bernabeu.

GIGGS NAYE AWA KOCHA MCHEZAJI SAFU YA BENCH LA UFUNDI.

KLABU ya Manchester United imemtangaza kiungo wake mkongwe Ryan Giggs kuwa kocha mchezaji wa klabu hiyo. Giggs mwenye umri wa miaka 39, aliongeza mkataba wa mwaka mmoja Machi mwaka huu na sasa ataunganisha na majukumu yake mapya yA Kocha mchezaji wa kikosi cha kwanza cha United. Katika taarifa yake Moyes amesema amefurahishwa na Giggs kuikubali nafasi hiyo ya kuwa mchezaji na pia kocha na uzoefu wake wakipindi kirefu utasaidia kuifanya United kuendeleza ubora wake. Giggs ambaye ni raia wa Wales alianza kuchomoza katika timu ya wakubwa ya United mwaka 1991 na kufanikiwa kushinda mataji 13 ya Ligi Kuu nchini Uingereza, manne ya Kombe la FA na medali mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
RYAN GIGGS NA MAN U
-UMRI: 39
-MECHI: 941
-MAGOLI: 168
-MATAJI YA LIGI: 13
-FA CUP: 4
-LIGI CUP: 4
-UEFA CHAMPIONZ LIGI: 2

HISPAIN BADO NAMBARI MOJA DUNIANI VIWANGO VYA FIFA

LICHA wa kutandikwa na Brazil katika  Michuano ya Kombe la Mabara hatua ya fainali Mabingwa wa Dunia Spain bado wameendelea kukamata Nambari moja katika Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotoka leo huku Brazil wakipanda Nafasi 13 na kushika Nafasi ya 9 lakini England  imeporomoka Nafasi 6 hadi kufikia Namba 15 na Tanzania imeshuka Nafasi 12 na sasa ipo ya 121.
Ivory Coast ndiyo Nchi ambayo iko juu kupita zote Afrika na inakamata Nafasi ya 13.
Brazil, ambao Jumapili iliyopita walitwaa Kombe la Mabara, wamerudi 10 Bora na sasa wapo Nafasi ya 9.
Listi nyingine itatolewa Agosti 8.
20 BORA:
Spain
Germany
Colombia (Imepanda Nafasi 4)
Argentina (Imeshuka 1)
5 Holland
Italy (Imepanda 2)
Portugal (Imeshuka 1)
Croatia (Imeshuka 4)
9 Brazil (Imepanda 13)
10 Belgium (Imepanda 2)
11 Greece (Imepanda 5)
12 Uruguay (Imepanda 7)
13 Ivory Coast
14Bosnia-Herzegovina (Imepanda 1)
15 England (Imeshuka 6)
16Switzerland (Imeshuka 2)
17 Russia (Imeshuka 6)
18 Ecuador(Imeshuka 8)
19 Peru (Imepanda 11)
20 Mexico (Imeshuka 3).