Monday, February 17, 2014

WENGER AMJIBU MBWATUKAJI MOURINHO

Kocha wa Klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amefafanua kauli ya Jose Mourinho kumuita mtaalamu wa kushindwa kuwa ni kauli ya kijinga na iliyokosa heshima. Kauli ya hiyo ya Mourinho aliitoa kujibu kauli iliyotolewa na Wenger kuwa baadhi ya mameneja wa timu za Ligi Kuu nchini Uingereza wanadai kuwa hawana mpango na taji hilo msimu huu kutokana na uoga wao. Akihojiwa Wenger amesema hataki kuingia katika vita ya maneno na Mourinho lakini anadhani kauli yake ni aibu kwa timu yake ya Chelsea kuliko ilivyo kwake. Wenger amesema asingependa kuzungumzia kauli za kijinga na zilizokosa heshima kwasababu huwa hapendi kumzungumzia Mourinho katika mikutano yake na waandishi wa habari na hatakuja kufanya hivyo. Kocha huyo alikipongeza kikosi chake kwa kucheza vizuri katika mchezo dhidi ya Liverpool ambao uliwawezesha kukata tiketi ya robo fainali ya Kombe la FA kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

KAKA ASEMA NI MCHEZA NA MCHEZAJI BORA CRISTIANO RONALDO

KIUNGO Mahiri wa klabu ya AC Milan ya Italia, Kaka amebainisha kuwa Lionel Messi na Zinedine Zidane ni wachezaji bora aliokutana nao na kudai kuwa Cristiano Ronaldo ndio mchezaji bora kabisa kuwahi kucheza naye. Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil, amewahi kukutana na Messi mara kadhaa wakati akicheza Real Madrid ambako alikuwa akicheza sambamba na Ronaldo. Kaka aliandika katika ukurasa rasmi wa twitter wa Milan wakati akijibu maswali ya mashabiki ambapo amesema wachezaji bora aliowahi kucheza dhidi yao ni Zidane na Messi huku akimtaja Ronaldo kama mchezaji bora aliyewahi kucheza naye. Kaka pia alimtaja Paulo Maldini kama beki bora kabisa duniani kuwahi kucheza naye kabla hajaondoka Milan kwenda Madrid.

TPS KUWAWEZESHA WASICHANA WALIOKOSA FURSA

Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), imeahidi kuchangia Sh. milioni 1.7 kwa ajili ya kitengo cha wasichana waliokosa fursa.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa TPSF, Godfrey Simbeye, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitengo hicho kilichopo chini ya usimamizi wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara, kazi za mikono na nguo. (Tahowete).

Simbeye alisema atakwenda kuwaombea fedha hizo TPSF ili kuwasaidia wasichana hao watano katika shule ya ushonaji na kuongeza kuwa wajasiriamali wangewezeshwa kwa kuwa wakifanya biashara wanaweza na bila kuwezeshwa hawawezi kufanya jambo lolote.

Aidha alisema serikali ina mpango wa kuanzisha miradi ambayo wanataka iwawezeshe wanawake,.

Mwenyekiti wa Tawohate, Anna Matinde, alisema chama hicho kinasaidia jamii hasa wasichana wanaomaliza masomo na kukosa ajira, pamoja na wale wanaonyanyasika kijamii kwa kuanzisha miradi ambayo wasichana hao waliokatiza masomo waweze kuendelea na masomo.
Chanzo: Nipashe

Sunday, February 16, 2014

JUVE WAJIHAKIKISHIA UBINGWA WAKO JUU POINTI 12 MBELE YA AS ROMA

JUVENTUS Mabingwa wa Italy wakiwa katika dimba la Nyumbani wamefanikiwa kuichapa Timu ya Chievo Verona  Bao 3-1 Mabao ya Kwadwo Asamoah, Mchezaji kutoka Ghana, na Claudio Marchisio pamoja na Fernando Llorente huku Chievo Verona ikijipatia Bao moja baada ya Juve kujifunga wenyewe wakati Stefan Lichtsteiner akiwa katika harakati za kuokoa na Mpira kumgonga Martin Caceres na kutinga wavuni
Jumamosi Februari 15
ACF Fiorentina 1 Inter Milan 2
[Saa za Bongo]
Jumapili Februari 16
Calcio Catania 3 SS Lazio 1
Atalanta BC 0 Parma FC 4
Juventus FC 3 AC Chievo Verona 1
Cagliari Calcio 1 AS Livorno Calcio 2
Genoa CFC 3 Udinese Calcio 3
US Sassuolo Calcio 0 SSC Napoli 2
2245 AS Roma v UC Sampdoria
Jumatatu Februari 17
2245 Hellas Verona FC v Torino FC

MSIMAMO-Timu za Juu:
NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Juventus FC 24 20 3 1 59 19 40 63
2 AS Roma 22 15 6 1 45 11 34 51
3 SSC Napoli 24 15 5 4 49 27 22 50
4 ACF Fiorentina 24 13 5 6 43 26 17 44
5 Inter Milan 24 10 9 5 42 28 14 39
6 Parma FC 23 9 9 5 36 27 9 36
7 Hellas Verona 23 11 3 9 39 37 2 36
8 Torino FC 23 8 9 6 36 30 6 33
9 AC Milan 24 8 8 8 37 35 2 32

LA LIGA-REAL MADRID YAINYUKA GETAFE CF NYUMBANI 3-0

Real Madrid, ambao hawajapoteza Mechi tangu wafungwe na Barca 2-1 katika uwanja wa Nou Camp Mwezi Oktoba, Leo wakicheza dhidi ya Getafe bila ya Mshambuliaji wao Mahiri Cristiano Ronaldo, ambae yuko Kifungoni Mechi 3, walianza kufunga kwa Bao la Jese katika Dakika ya 6, kisha Dakika ya 27 Benzema akapiga Bao la Pili na Modric kupiga Bao la Tatu Dakika ya 66.
Ambapo hapo Jana, fc Barcelona waliifumua Rayo Vallecano Bao 6-0 na Atletico Madrid waliichapa Real Valladolid Bao 3-0.
RATIBA
Jumamosi Februari 15
Atletico de Madrid 3 Real Valladolid 0
Levante 1 UD Almeria 0
FC Barcelona 6 Rayo Vallecano 0
Villarreal CF 0 Celta de Vigo 2
Jumapili Februari 16
Granada CF 1 Real Betis 0
Getafe CF 0 Real Madrid 3
2100 Athletic de Bilbao v RCD Espanyol
2300 Sevilla FC v Valencia
Jumatatu Februari 17
2400 Malaga CF v Real Sociedad
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
FC Barcelona
24
19
3
2
69
17
52
60
2
Real Madrid CF
24
19
3
2
68
24
44
60
3
Atletico Madrid
24
19
3
2
59
16
43
60
4
Athletic Bilbao
23
13
5
5
42
28
14
44
5
Villarreal CF
24
12
4
8
44
29
15
40
6
Real Sociedad
23
10
7
6
42
34
8
37
7
Sevilla FC
23
8
7
8
42
41
1
31
8
Valencia
23
9
4
10
36
35
1
31

TAMBWE JEZI NAMBA 17 NA MABAO 17 MSIMBAZI SIMBA SC


Amisi Tambwe, raia wa Burundi ni moja kati ya washambiliaji mahiri mwenye kujitambua akiwa uwanjani ambapo amedhihirisha kuwa yeye ni mkali wa mabao
kutokana katika mechi 23 alizoichezea Simba SC hadi sasa za mashindano yote na kirafiki, amefunga mabao 17.
Kwa sasa, Tambwe ndiye mchezaji anayeongoza kwa mabao katika Ligi Kuu, akiwa amefunga mabao 15 na anafuatiwa kwa mbali na mshambuliaji wa AzamFC, Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast, mwenye mabao 10.
Tambwe amekuwa kipenzi cha wana Msimbazi kutokana na kuweza pia kutikisa nyavu za mahasimu, Yanga SC katika mechi mbili mfululizo baina ya timu hizo.
Tambwe alikuja Simba SC kwa pamoja na Mrundi mwenzake, beki Gilbert Kazewakitokea wote Vital’O msimu huu, baada ya kung’ara katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame nchini Sudan wakiiwezesha klabu yao kutwaa taji la michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Hata hivyo, Kaze amepoteza namba katika kikosi cha kwanza tangu ujio wa kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic, ambaye amekuwa akimpanga beki Mkenya, Donald Mosoti aliyetokea naye Gor Mahia ya Kenya.  

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207MTOTO AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI MKOANI MBEYA.
MTOTO ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FRED ROBERT (08) MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI KATIKA SHULE YA MSINGI MBALIZI NA MKAZI WA MBALIZI ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA DEREVA WAKE. 
TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 15.02.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA HUKO MBALIZI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. 
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA PIKIPIKI HIYO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. 
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA SILAHA [PISTOL] BILA KIBALI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. JACKSON MWAKALUNGWA (24) NA 2. SAIKO WAILODI (35) DEREVA WOTE WAKAZI WA MLOWO WAKIWA NA SILAHA AINA YA PISTOL ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI NA INAYOTUMIA RISASI ZA SHOTGUN.
 WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.02.2014 MAJIRA YA SAA 14:25HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHENGE WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA.
 MTUHUMIWA JACKSON MWAKALUNGWA ALIKAMATWA AKIWA NDANI YA GARI AINA YA TOYOTA HIACE AKIELEKEA WILAYA YA MBARALI KUFANYA UHALIFU NA ALIKIRI KUAZIMISHWA SILAHA HIYO NA MTUHUMIWA ALIYEMTAJA KWA JINA LA SAIKO WAILODI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI. 
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIMILIKISHA SILAHA BILA KIBALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. 
AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA AU PINDI WAONAPO VIASHIRIA VYA WATU KAMA HAO KATIKA MAENEO YAO ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.