Sunday, February 23, 2014

UEFA EURO 2016: DROO KUPANGA MAKUNDI YAWEKWA HADHARANI.

DROO ya kupanga Makundi kwa ajili ya Mechi za Mchujo za kufuzu kucheza Fainali za UEFA EURO 2016, ambayo ndio Mashindano ya Mataifa ya Ulaya ,imefanyika Leo huko Palais des Congrès Acropolis Mjini Nice, France..
MAKUNDI: 
KUNDI A: Netherlands, Czech Republic, Turkey, Latvia, Iceland, Kazakhstan.
KUNDI B: Bosnia-Hercegovina, Belgium, Israel, Wales, Cyprus, Andorra.
KUNDI C: Spain, Ukraine, Slovakia, Belarus, FYR Macedonia, Luxembourg.
KUNDI D: Germany, Republic of Ireland, Poland, Scotland, Georgia, Gibraltar.
KUNDI E: England, Switzerland, Slovenia, Estonia, Lithuania, San Marino.
KUNDI F: Greece, Hungary, Romania, Finland, Northern Ireland, Faroe Islands.
KUNDI G: Russia, Sweden, Austria, Montenegro, Moldova, Liechtenstein.
KUNDI H: Italy, Croatia, Norway, Bulgaria, Azerbaijan, Malta.
KUNDI I: Portugal, Denmark, Serbia, Armenia, Albania.
EURO2016-FRANCE_LOGOMechi za Makundi zitaanza kati ya Septemba 7 na 9 Mwaka huu.
Timu mbili za juu toka kila Kundi pamoja na Timu moja Bora iliyoshika Nafasi ya 3 kwenye Makundi zitatinga Fainali na Timu 8 zilizobaki ambazo zitamaliza Nafasi ya Tatu zitapangiwa Mechi maalum za Mchujo ili kupata Timu 4 za mwisho kuingia Fainali.
Mechi za Makundi zitaanza Septemba 2014 hadi Oktoba 2015 na Ratiba kamili itatolewa na UEFA baada ya Droo.
Fainali za UEFA EURO 2016 zitachezwa Nchini Ufaransa kuanzia Juni 10, 2016 hadi Julai 10, 2016 na kwa mara ya kwanza Fainali hizo zitakuwa na Nchi 24 badala ya zile 16 za kawaida.
Kwa mara ya kwanza, UEFA imebuni Mtindo wanaouita ‘Wiki ya Soka’ ambao utafanya Gemu zichezwe kuanzia Alhamisi hadi Jumanne.
Saa za Mechi kuanza ni 18.00CET na 20.45CET kwa Jumamosi na Jumapili na 20.45CET kwa Alhamisi, Ijumaa, Jumatatu na Jumanne.
CET ni Saa za Ulaya ya Kati ambazo ni Masaa mawili nyuma ya Saa za Bongo kwa Majira ya Sasa.
Pia, Mtindo huo wa ‘Wiki ya Soka’ utakuwa na Wiki maalum ambapo Mechi mbili zitachezwa mfululizo, yaani Alhamisi/Jumapili, Ijumaa/Jumatatu au Jumamosi/Jumanne.
Droo kwa ajili ya Mechi za Fainali itafanyika Mjini Paris hapo Desemba 12, 2015.

YANGA RAHA TFF YAONDOA GEMU YA J5 DHIDI YA PRISONS

MECHI namba 118 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Tanzania Prisons iliyokuwa ichezTFF_LOGO12we Februari 26 mwaka huu itapangiwa tarehe nyingine.
Uamuzi wa kuiondoa mechi hiyo iliyokuwa ichezwe Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umefanywa ili kuipa fursa zaidi Yanga kujiandaa kwa mechi yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Ahly ya Misri itakayofanyika Jumamosi (Machi 1 mwaka huu).

Al Ahly na Yanga zitarudiana wiki moja baadaye kati ya Machi 7, 8 au 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.

RATIBA HII HAPA UBORESHAJI TAIFA STAR KATI YA MIKOA VS MIKOA

Mechi za mpango wa kuboresha Taifa Stars kati ya mikoa na mikoa wiki hii itakuwa kama ifuatavyo;
Februari 25 Njombe vs Ruvuma (Uwanja wa Njombe)
Kinondoni vs Ilala (Uwanja wa Karume)
Februari 26 Morogoro vs Pwani (Uwanja wa Jamhuri)
Geita vs Kagera (Uwanja wa Geita)
Kilimanjaro vs Tanga (Uwanja wa Ushirika)
Iringa vs Mbeya (Uwanja wa Samora)
Shinyanga vs Simiyu (Uwanja wa Kambarage)
Lindi vs Mtwara (Uwanja wa Ilulu)
Februari 27 Temeke vs Kinondoni (Uwanja wa Karume)

Mashidano haya ni moja ya mikakati ya Rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kukuza soka ya Tanzania.

TWIGA STAR YAJIFUA KUIKABILI ZAMBIA FEB 28

Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inaendelea kujinoa kwa ajili ya mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa Wana

Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage na Msaidizi wake Nasra Juma inaendelea vizuri, na kwa mujibu wa programu ya benchi lao la ufundi kesho (Jumatatu), Jumanne na Jumatano itafanya mazoezi saa 10 jioni.
TFF_LOGO12Mazoezi hayo yatafanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Uwanja huo ndiyo utakaotumika kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.
Shepolopolo ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 2-1 wiki iliyopita inatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet, na siku hiyo hiyo itafanya mazoezi Azam Complex.
Waamuzi wa mechi hiyo Ines Niyonsaba, Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis Iratunga, wote kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili nchini Jumatano

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207WATOTO WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA ANOLD ZAKAYO (06) MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA SHULE YA MSINGI MWANYANJE NA SELINA EMMANUEL (06) MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI MWANYANJE WALIFARIKI DUNIA WAKIWA WANAOGELEA KWENYE MADIMBWI YA MAJI KATIKA MTAA WA NSALAGA. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 22.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI HUKO UYOLE KATA YA NSALAGA TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA VIFO HIVYO NI BAADA YA MAREHEMU HAO KUZIDIWA NA MAJI AMBAYO YAMETOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA PINDI WANAOGELEA NA WATOTO WENZAO. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA/KUFUKIA/KUZIBA MITARO/VISIMA/MASHIMO YALIYO WAZI KWANI NI HATARI KWA WATOTO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA JITOKEZA.
MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG  SONGWE MKOA WA MBEYA AKUTWA AMEFARIKI DUNIA SHAMBANI KWAKE.
MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG SONGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MARIA LEONARD (38) MKAZI WA IGIDA AKUTWA AMEFARIKI DUNIA KWENYE SHAMBA LAKE LA MAHINDI. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 22.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:30HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA IGIDA, KATA YA UTENGULE USONGWE, TARAFA YA SONGWE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. AWALI MNAMO TAREHE 15.02.2014 MAREHEMU ALIWAAGA WAUMINI NA MAJIRANI KUWA ANAKWENDA KUHUDHURIA MAZISHI KATIKA KIJIJI CHA ISUNGO WILAYA YA MBOZI NA TOKEA HAPO MAREHEMU HAKUONEKANA NYUMBANI MPAKA MAITI YAKE ILIPOONEKANA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UMESHAHARIBIKA HUKU PEMBENI KUKIWA NA JEMBE LAKE. TAARIFA ZA AWALI ZINASEMA HUENDA MAREHEMU ALIPIGWA NA RADI WAKATI AKIWA SHAMBANI KWAKE. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA KUKAA/KUJIFICHA KARIBU NA MITI MIKUBWA WAKATI MVUA INANYESHA KWANI NI HATARI.
WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].

BPL:MAN UNITED YAMKA USINGIZINI YAILAZA PALACE 2-0

Wakiwa Ugenini katika dimba la Selhurst Park kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na vijana wagumu wa Crystal Palace, Mabingwa Watetezi wa England, Manchester United, walishinda Bao 2-0 na kujongea jongea Nafasi moja juu hadi Nafasi ya 6.
Mabao ya Kipindi cha Pili Dakika ya 62, Robin van Persie pamoja na Dakika ya 68  na Wayne Rooney wameiwezesha Man united kuizamisha Crystal palace katika mtanange huo.
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Chelsea 27 28 60
2 Arsenal 27 25 59
3 Man City 26 42 57
4 Liverpool 26 34 53
5 Tottenham 26 4 50
6 Man Utd 27 12 45
7 Everton 26 10 45
8 Southampton 27 6 39
9 Newcastle 26 -6 37
10 West Ham 27 -3 31
11 Hull 27 -2 30
12 Swansea 26 -3 28
13 Aston Villa 26 -9 28
14 Stoke 27 -15 27
15 Crystal Palace 26 -18 26
16 West Brom 27 -8 25
17 Norwich 26 -20 25
18 Sunderland 26 -16 24
19 Cardiff 27 -29 22
20 Fulham 27 -32 21

KILI MARATHON DK. MUKANGARA MGENI RASMI

KATIKA mbio za 12 za Kilimanjaro Marathon ambazo zinazotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo tarehe 2 Machi, 2014 mjini Moshi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dk. Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Aggrey Marealle, Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, Waratibu wa mbio hizo alisema jana kuwa Dr. Mukangara amekubali kuwa mgeni rasmi na atahuduria sherehe ya utoaji zawadi ambapo atatoa zawadi kwa washindi kumi wa mbio defu za kilomita 42 maarufu kama Full Marathon kwa wanaume na wanawake.
Dk. Mukangara ameeleza mara kadhaa kwamba serikali inaunga mkono Kilimanjaro Marathon kwa kutambua mchango wake michezo, utalii na uchumi,” alisema Marealle.
Marealle ameongeza baada ya sherehe ya utoaji zawadi Waziri ataungana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na mpenda michezo Mhe. Leonidas Gama, wawakilishi wa wadhamini na watu wengine mashuhuri kwenye mlo maalum  wa mchana uliodhaminiwa na Kibo Palace Hotel. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro binafsi na kupitia ofisi yake amekuwa muungaji mkono wa Kilimanjaro Marathon na amekuwa akifurahia kukaribisha maelfu ya watu wanaokuja Moshi kutoka mataifa mbalimbali.
John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema “mbio za mwaka huu zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza idadi ya washiriki. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za kilomita 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 4 kila mmoja, shilingi milioni mbili kwa washindi wa pili na shilingi milioni 1 kwa washindi wa tatu. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za  nusu marathon (km 21) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 2 kila mmoja, shilingi milioni 1 kwa washindi wa pili na shilingi 500,000 kwa washindi wa tatu.
Addison aliongeza kuwa medali na t-shirt zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42, wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu marathon na wanariadha 80 wa kwanza kumaliza mbio za walemavu.  Washiriki 3,000 wa kwanza kumaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watapewa t-shirts baada ya kumaliza mbio na watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali za kuvutia kupitia droo.
Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water,Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne,