YANGA,
RHINO KUCHEZA TABORA VPL
Yanga
inaumana na Rhino Rangers katika moja kati ya mechi mbili za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) zitakazochezwa wikiendi hii katika miji miwili tofauti.
Mechi
hiyo itafanyika kesho (Machi 22 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,
mjini Tabora ambapo kiingilio kitakuwa sh. 5,000 kwa jukwaa kuu na sh. 3,000
mzunguko.
Nayo
JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbeya City katika mechi itakayochezwa kesho Uwanja
wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Ligi
hiyo itaendelea keshokutwa (Jumapili) kwa mechi nne ambapo Simba itacheza na
Coastal Union katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Azam itaoneshana kazi na
Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex. Mechi hizo mbili zitakuwa ‘live’
kupitia Azam Tv.
Mechi
nyingine za Jumapili ni Mgambo Shooting dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga, wakati Ruvu Shooting na Ashanti United zitapimana ubavu
kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
MSIMAMO:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GD
|
PTS
|
1
|
Azam
FC
|
20
|
12
|
8
|
0
|
27
|
44
|
2
|
Yanga
SC
|
19
|
11
|
7
|
1
|
29
|
40
|
3
|
Mbeya
City
|
21
|
10
|
9
|
2
|
10
|
39
|
4
|
Simba
SC
|
21
|
9
|
9
|
3
|
17
|
36
|
5
|
Kagera
Sugar
|
21
|
8
|
8
|
5
|
3
|
32
|
6
|
Ruvu
Shooting
|
20
|
7
|
7
|
6
|
-4
|
28
|
7
|
Coastal
Union
|
21
|
5
|
11
|
5
|
1
|
26
|
8
|
Mtibwa
Sugar
|
21
|
6
|
8
|
7
|
-1
|
26
|
9
|
JKT
Ruvu
|
21
|
8
|
1
|
12
|
-13
|
25
|
10
|
Prisons
FC
|
20
|
3
|
10
|
7
|
-4
|
19
|
11
|
Mgambo
JKT
|
20
|
4
|
6
|
10
|
-17
|
18
|
12
|
Ashanti
United
|
21
|
4
|
6
|
11
|
-18
|
18
|
13
|
JKT
Oljoro
|
21
|
2
|
9
|
10
|
-16
|
15
|
14
|
Rhino
Rangers
|
21
|
2
|
7
|
12
|
-14
|
13
|
RATIBA
MECHI ZIJAZO:
Jumatano
Machi 26
Mgambo
JKT v Azam FC
Yanga
v Tanzania Prisons
Jumamosi
Machi 29
Ashanti
United v JKT Oljoro
Jumapili
Machi 30
Mbeya
City v Tanzania Prisons
Kagera
Sugar v Ruvu Shooting
Mtibwa
Sugar v Coastal Union
JKT
Ruvu v Rhino Rangers
Azam
FC v Simba
Mgambo
JKT v Yanga
KIKOSI
KAZI KUSHUGHULIKIA TIKETI ZA ELEKTRONIKI

TFF
na CRDB zimefanya kikao cha pamoja jana (Machi 20 mwaka huu) kuhusu masuala ya
tiketi za elektroniki na kukubaliana kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya
uboreshaji matumizi ya mfumo huo.
Kikosi
kazi hicho kitakuwa na wajumbe kutoka TFF na CRDB. Kwa upande wa TFF wajumbe
wake ni Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama, Evodius Mtawala, Ofisa Habari na
Mawasiliano, Boniface Wambura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga.
Rais
wa TFF, Jamal Malinzi ametoa shukrani za kipekee kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei ambaye alihudhuria binafsi kwenye kikao
akiongoza timu yake.
Malinzi
amesema ni imani ya TFF kuwa mfumo wa tiketi za elektroniki ndiyo mkombozi wa
ulinzi wa mapato milangoni, na anaamini kwa pamoja TFF na CRDB zitafanikisha
matumizi hayo ya tiketi za elektroniki.