Sunday, May 4, 2014

STARS YATOA SARE NA MALAWI MECHI YA KIRAFIKI-SOKOINE

Kikosi cha Taifa Stars, chini ya Kocha mpya wa Mart Nooij leo amekiongoza kikosi chake kutoka sare ya bao 0-0 dhidi ya Malawi katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, leo.


Nooij raia wa Uholanzi alikipanga kikosi chake leo kikiongozwa na wachezaji wengi wazoefu kilishambulia zaidi lakini hakikuweza kupata bao kutoka na kukosa mawasiliano mazuri katika safu ya ushambuliaji.
Hata hivyo Malawi nao walijibu mashambulizi katika kipindi cha pili  lakini hawakuweza kupata bao ambapo katika mtanange huo mashabiki wengi mashabiki mbalimbali mkoani mbeya wamejitokeza kuiunga mkono stars ya Mart Nooij.

TIMU 16 LIGI KUU MSIMU WA 2015/2016

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuanzia msimu wa 2015/2016 itakuwa na timu 16 badala ya 14 za sasa.
Mabadiliko hayo yamepitishwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Mei 3 mwaka huu) jijini Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo ya kuongeza idadi ya timu kutoka kwenye Kamati ya Mashindano.
DSC_0172Uamuzi huo umefanywa kwa lengo la kuongeza ushindani katika ligi hiyo, na kuwezesha wachezaji kupata mechi nyingi zaidi za mashindano. Kwa mabadiliko hayo maana yake ni kuwa Ligi ya msimu wa 2015/2016 itakuwa na mechi 240 wakati kwa sasa ina mechi 182.
Kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye VPL, Kamati ya Utendaji itafanyia uamuzi mapendekezo katika eneo hilo baada ya kwanza kupata maoni ya klabu za VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambazo Mei 11 mwaka huu zitakutana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ni kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni iendelee kuwa watano kama ilivyo katika kanuni za sasa za VPL.

MTAALAMU WA NYASI BANDIA AWASILI
Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClemen amewasili nchini leo alfajiri (Mei 4 mwaka huu) ambapo atakuwepo kwa siku tatu.
nyasiMcClemen ameondoka leo (Mei 4 mwak huu) kwenda Bukoba ambapo atakagua Uwanja wa Kaitaba, na kesho (Mei 5 mwaka huu) atakwenda jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Viwanja hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es

Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Thursday, May 1, 2014

YANGA YAWATAKA MASHABIKI WAKE KUONDOA HOFU.

Uongozi wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba ramba.
Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na kama kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu zitatumika wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa TFF juu ya taratibu zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya kuwasainisha Kavumbagu na Twite. 
Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa muda wa mikataba yao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga kwa ajili msimu mpya ujao 2014/2015.
Didier Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao ilikuwa mwishoni waliongea na uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi wa Septemba juu ya kuweka sahihi zao na kuendelea kuitumikia Yanga na  kukubaliana mambo yote ya msingi kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya usajili wa wachezaji wa kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la Bagamoyo linapaswa kuanza kutekelezwa msimu huu.
Uongozi wa Yanga uliandikia TFF  barua mapema kuomba kupewa mwongozo wa kanuni zitakazotumika kwenye usajli kwa wachezaji wa kimataifa kwa msimu mpya kufuatia Azimio la Bagamoyo kuelekeza msimu huu kila timu inapasa kuwa na wachezaji watatu wa kigeni, mpaka sasa uongozi wa Yanga haujapata majibu juu ya utaratibu utakaotumika kwenye msimu wa Ligi Kuu ijayo.
Hivyo makubaliano ya wachezaji Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na uongozi wa Yanga SC yalikua yakisubira majibu ya TFF juu ya kanuni zipi zitakazotumika kwenye usajili msimu wa 2014/2015 kwa wachezaji wa kigeni na katika hali ya kushangaza Kavumbagu akaonekana tayari ameshasaini kuichezea timu ya Azam FC.
Kuhusu Frank Domayo aliyeripotiwa jana kujiunga na Azam FC pia alikuwa katika makubalianoya kuongeza mkataa tangu mwezi Julai 2013, alikubaliana na uongozi juu ya mambo yote ya msingi na kilichobakia ilikuwa ni kuweka sahihi kwenye mkataba mpya, lakini Domayo alisema hawezi kusaini mpaka siku atakapokuja mjomba wake ambaye ndie wakala wake na ahadi hiyo iliendelea kwa muda wa mwaka mzima kabla ya jana kusikia ameshasaini timu nyngine.
Habari hizi zimewashitua wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans lakini ukweli ni kuwa wachezaji wenyewe walisindwa kuwa wakweli kwa viongozi na mwisho wa siku walikua na mipango yao ya kuondoka, hivyo uongozi ulijtahid kadri ya uwezo wake lakini wachezaji wanaonekana hawakua tayari kuendelea kuichezea Yanga SC.
Taarifa kamili kuhusu mipango ya timu kwa msimu ujao pamoja na ripoti ya kocha mkuu Hans pamoja na benchi lake la Ufundi zitatolewa hivi karibuni baada ya benchi la ufundi na uongozi kukaa kwa pamoja na kuafikiana mipango ya msimu ujao.
Aidha uongozi wa Yanga SC unawaomba wanachama wake, wapenzi na washabiki wasiwe na wasi wasi juu ya kuondoka kwa wachezaji hao kwani Yanga bado ina nafasi wachezaji wengi wenye vipaji na itaendelea kuboresha kikosi chake kwa kuzingatia maelekezo ya kocha mkuu Hans katika usajli wa msimu ujao.

TFF WASHAURI KUTOKATA TAMAA NA STARS YA MABORESHO.

SHIRIKISHO la soka Tanzania limeshauriwa kutokata tamaa na mpango wake wa maboresho ya Taifa Stars kupitia mkakati wake wa kusaka vipaji mikoani ulioanzishwa hivi karibuni.

Taifa stars ya maboresho iliweka kambi mjini Tukuyu mkoani Mbeya na kwa mara ya kwanza ilionekana aprili 26 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mechi hii iliyowavutia wadau wengi wa soka kwa lengo la kuona vipaji vipya kutoka mikoani, Stars ilifungwa bao(3-0).

Taifa Stars ilikuwa imesheheni vipaji vipya vilivyopatikana katika mkakati wa maboresho ya Taifa stars ambapo jopo la makocha waliteuliwa na TFF na kuzunguka nchi nzima kusaka vijana wa kuingizwa katika timu.

Wakati mkakati huu ukitangazwa, wadau waliuchukuliwa kwa mitazamo miwili tofauti ambapo na kundi moja liliunga mkono na lingine likapinga kwa madai kuwa hautakuwa na tija kwa wakati huu ambao timu inajiandaa kufuza AFCON mwakani nchini Morocco.

TFF YATEUA WAKILI KUCHUNGUZA USAJILI WA DOMAYO AZAM FC .

KatiKa harakati za usajili wa mwanzo tukio lililotokea jana (Aprili 30 mwaka huu) kwenye kambi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya likihusisha usajili wa baadhi ya timu, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo mzima wa tukio hilo.

Taarifa ya TFF ya leo asubuhi imesema kwamba, baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua.
TFF imesema katika taarifa yake inatoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao.

Viongozi wa Azam FC jana walikwenda kwenye kambi ya Taifa Stars kukamilisha taratibu za usajili na kiungo Frank Domayo, aliyemaliza Mkataba wake Yanga SC.

Baada ya kufanikiwa kumsainisha Mkataba wa miaka miwili, wasimamizi wa kambi waliwaitia Polisi viongozi wa Azam FC ambao hata hivyo baadaye waliachiwa. Lakini inadaiwa fomu za usajili zilichanwa.
Azam si klabu ya kwanza kusajili mchezaji katika kambi ya timu ya taifa, kwani vigogo wa s
oka nchini, Simba na Yanga ndiyo waasisi wa mchezo huo.

Mwaka jana Simba SC walisaini Mkataba mpya na kiungo wao, Amri Kiemba akiwa katika kambi ya Taifa Stars, hoteli ya Tansoma mjini Dar es Salaam.
Yanga SC iliwasajili Domayo kutoka JKT Ruvu, Kevin Yondan kutoka Simba SC wote wakiwa katika kambi ya Taifa Stars Dar es Salaam miaka miwili iliyopita.

Wednesday, April 30, 2014

MALAWI KUTUA NCHINI KESHO MEI 1 MWAKA HUU.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Mrisho Ngassa (kushoto) akiangalia namna ya kumtoka mlinzi wa timu ya Taifa ya Mawali, Wisdom Ndhlovu wakati timu hizo zilipochuana katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa katika uwanja mpya wa taifa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Henry Joseph wa Taifa Stars. (Picha na Mroki Mroki).TIMU ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kuwasili nchini kesho Mei 1 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Mei 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Flames yenye msafara wa 31 utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu cha Malawi (FAM) utaingia Mbeya kwa usafiri wa barabara. Wachezaji katika msafara huo ni 20.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha mpya, Mart Nooij tayari ipo jijini Mbeya kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.

KATIBU MKUU WA FIFA AWASILI KESHO DAR

Valcke ambaye atafuatana na maofisa wengine saba wa FIFA baadaye kesho hiyo hiyo (Mei 1 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi kwenye hoteli ya Double Tree by Hilton iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam.