SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) hapa nchini limeendeleza kutunisha msuli baada ya jana kusaini
mkataba na kampuni ya proin Promotions kwa ajili ya kudhamini mashindano ya
Kombe la Taifa kwa wanawake yatakayofanyika kati ya mwezi Septemba na Oktoba
mwaka huu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti
wa Kampuni hiyo, Johnson Rukaza, alisema kuwa makubaliano hayo waliyoingia na
TFF yatakuwa ni ya miaka miwili na yatawagharimu zaidi ya Sh.
milioni 150 ili kufanikisha michuano hiyoRukaza
alisema kuwa kupitia mashindano hayo ya Kombe la Taifa wanaamini vipaji vya
wachezaji wanawake vitaonekana na baadaye kuisaidia timu ya Taifa ya jinsia
hiyo (Twiga Stars) kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ambayo
inashiriki.
Amesema kwamba wao wamefungua njia
kudhamini mashindano hayo na wanawaomba makampuni na taasisi nyingine
kujitokeza kudhamini mashindano hayo ikiwamo na vituo vya televisheni lengo
likiwa ni kutangaza soka la wanawake.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi, alisema kuwa
uongozi wake unawashukuru wadhamini hao wapya na inaahidi uongozi wake
utahakikisha soka la wanawake linasonga mbele.
Malinzi amesema kwamba wanawaomba wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wa kike kushiriki mchezo huo kwa sababu utawasaidia kiafya, kupata burudani na kuinua hali zao za kichumi pale watakapofanikiwa kupata klabu za kucheza.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Lina Kessy, alisema kwamba wanaamini sasa mpira wa wanawake utacheza na jana ilikuwa ni siku ya kihistoria kwenye medani ya mchezo huo kwa upande wa wanawake.

Kessy amesema kwamba TFF na TWFA
itahakikisha jitihada za kusaka wadau wengine zinaendelea ili mchezo huo
uchezwe sehemu zote hapa nchini.
Amesema kwamba zaidi ya mikoa 17
inatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambayo mara ya mwisho yalifanyika mwaka
2008.