Thursday, June 5, 2014

CECAFA NILE BASIN CUP: VICTORIA UNIVERSITY BINGWA, WAULA DOLA 30,000!!


UNI2
UNI1VICTORIA UNIVERSITY wamefanikiwa kuwa Mabingwa wa Mashindano mapya ya CECAFA NILE BASIN CUP baada kuichapa AFC Leopards ya Kenya Bao 2-1 katika Fainali iliyochezwa huko Khartoum International Stadium Jijini Khartoum Nchini Sudan hapo Jana.
Haya ni Mashindano ya kwanza kabisa ya Kombe hilo yaliyoshindaniwa na Klabu kadhaa toka Nchi za Afrika Mashariki na ya Kati ambao ni Wanachama wa CECAFA.
Kwa ushindi huo, Victoria University pia wamejinyakulia Donge nono la Dola 30,000 na ni baraka kwa Klabu changa iliyoshiriki michuano ya CECAFA kwa mara ya kwanza kabisa.
Victoria University ndio waliowatoa Wawakilishi wa Tanzania Bara, Mbeya City, kwenye Robo Fainali baada ya kuwafunga Bao 1-0 kwa Bao la Penati.
UNI3Kwa kuwa Washindi wa Pili, AFC Leopards walipewa Dola 20,000.
MAGOLI:
Victoria University 2
-Odongo Mathew Dakika ya 29
-Mutyaba Muzamir 90+2
AFC Leopards 1
-Ikene Austin Dakika ya 45

Nao, Timu ya Sudan, Al Shandy, ilinyakua Dola 10,000 kwa kumaliza Washindi wa Tatu baada ya kuifunga Academie Tchite ya Burundi Bao 4-1.
Klabu zilizoshiriki muchuano hii ni:
KUNDI A
-Polisi [Zanzibar]
-Victoria University Uganda]
-Malakia [South Sudan]
Al Merreikh [Sdan]
KUNDI B
-Mbeya City [Tanzania Bara]
-AFC Leopards [Kenya]
-Academie Tchite [Burundi]
-Enticelles [Rwanda]
KUNDI C
-Defence [Ethiopia]
-Dkhill FC [Djibouti]
-Al Shandy [Sudan]

TAIFA STARS: 28 WAITWA KUPIGA KAMBI YA SIKU 3 KUANZIA JUNI 11

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea taarifa za kutolewa wito bungeni wa kulitaka litumie tiketi za elektroniki katika kukusanya mapato.
Tunataka ieleweke wazi kwa umma wa Watanzania kuwa si nia yetu kuchelewesha matumizi ya uingiaji mpirani kwa tiketi za elektroniki. Ieleweke kuwa mfumo wa kuingia kwenye mbuga, KCMC, mipakani ni tofauti na uingiaji mpirani.
Katika mpira wa miguu wanaingia maelfu ya watu katika kipindi kifupi. Kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda usalama wa watazamaji na miundombinu ya viwanja ndio maana tulisitisha matumizi ya tiketi za elektroniki hadi tujihakikishie usalama wa matumizi yake.
Tunafanya jitihada kwa karibu na mzabuni benki ya CRDB ili kuhakikisha mfumo huu unaanza kutumika mara moja.
Kwa niaba ya sekta ya michezo tunatoa wito kwa Serikali kushusha au kuondoa kodi kubwa zinazotozwa kwenye vifaa vya michezo, hasa vinavyotumiwa na watoto kuanzia umri wa miaka 6-12, ili watoto wetu waweze kuvipata kirahisi toka kwa wazazi wao ili waweze kujifunza kucheza michezo kisasa tangu wakiwa wadogo.
TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI JUNI 11
Kikosi cha Taifa Stars kinaingia tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku tatu jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.
Wachezaji wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Wednesday, June 4, 2014

WAMBURA AKABIDHIWA KWA WAKILI LUGAZIYA

KAMATI ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inakaa Jumatatu (Juni 9 mwaka huu) kusikiliza rufani moja inayopinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi
ya Simba.

Michael Wambura amewasilisha rufani yake TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba iliyomwengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Kamati hiyo inayoongozwa na Wakili Julius Lugaziya itakutana saa 5 asubuhi kwenye hoteli ya Courtyard iliyopo Upanga, jijini Dar es Salaam.

NYOTA WAWILI COPA WAENDA BRAZI

WACHEZAJI wawili waliochaguliwa kwenda kwenye kambi ya Copa Coca-Cola ya Dunia nchini Brazil wamekabidhiwa bendera tayari kwa safari hiyo inayofanyika leo (Juni 4 mwaka huu).
Hafla ya kukabidhi bendera hiyo kwa Ali Shabani Mabuyu na Juma Yusuf imefanyika leo katika hoteli ya
Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda ndiye alikabidhi bendera.
Wakati Mabuyu kutoka Ilala alikuwa mchezaji bora wa michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 kwa mwaka 2013/2014, Yusuf kutoka Zanzibar ndiye aliyeibuka mfungaji bora katika michuano hiyo.

Wachezaji hao watakuwa katika kambi hiyo itakayokuwa katika Jiji la Sao Paulo kwa siku kumi ambapo watafundishwa masuala mbalimbali ya mpira wa miguu. Pia watashuhudia mechi ya ufunguzi ya Fainali za Kombe la Dunia katika ya wenyeji Brazil na Croatia itakayochezwa Juni 12 mwaka huu.

Monday, June 2, 2014

STARS KUWASILI LEO, PONGEZI ZAMIMINIKA BAADA YA JANA KUINYAMAZISHA ZIMBABWE.



Kikosi cha Taifa Stars ambacho jana (Juni 1 mwaka huu) kiliitupa Zimbabwe (Mighty Warriors) nje ya michuano ya Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kinarejea nchini leo (Juni 2 mwaka huu) kutoka Harare.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Harare kupitia Nairobi.
Stars imefuzu kucheza raundi inayofuata kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2, kwani awali (Mei 18 mwaka huu) iliifunga Zimbabwe bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika raundi ya pili, Taifa Stars itacheza na Msumbiji ambapo itaanzia nyumbani kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.
Wakati huo huo, Taifa Stars imeendelea kupokea salamu za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali baada ya kufanikiwa kuvuka kikwazo hicho cha kwanza katika harakati zake za kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Salamu hizo zimetoka kwa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Manyara (MARFA), mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA), John Kadutu, na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Idd Mgoyi.
U15 TANZANIA YATUA MEDALI VIFUANI
Timu ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 15 iliyoshika nafasi ya pili katika Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) iliyofanyika Gaborone, Botswana inawasili leo (Juni 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
U15 ambayo imeshinda mechi tatu, sare moja na kufungwa moja inawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Gaborone kupitia Nairobi.
Tanzania ambayo imepata medali za fedha kwa kushika nafasi hiyo ikiwa chini yaKocha Abel Mtweve ilizifunga Afrika Kusini 2-0, Botswana 2-0, Swaziland 3-0 na ikatoka sare ya bao 1-1 na Mali. Ilifungwa mabao 2-0 na Nigeria ambao ndiyo walioibuka mabingwa.
Wachezaji 16 waliounda kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.

Sunday, June 1, 2014

MKUTANO MKUU WA YANGA SC SAFIIII WAFANYIKA BILA BUDHABU YOYOTE

Mkutano Mkuu wa marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika salama na furaha kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay huku wanachama wakipitisha kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC Yusuf Manji amewaongoza wanachama hai wapatao 1,560 kupitisha kipengele hicho kipya kwa ajili ya maslahi na faida ya Wana Yanga kwani bila kufanya hivyo timu isingeweza kuruhusiwa kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Aidha katika mkutano huo Manji amewatoa hofu wanachama kwa kuwaambia kuwa usajili unaendelea kufanyika na nafasi zilizobakia ni nne tu hivyo pindi utakapokamilika basi wataweka wazi kila kitu.
Kuhusu nafasi ya Kocha Mkuu Manji amesema Kamati ya Mashindano imemkabidhi mapendekezo yao na kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na Marcio Maximo aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania kuja kukinoa kikosi cha Jangwani.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mama Fatma Karume aliongoza kikao cha waachama kilichomuomba Bw Manji kuendelea na uongozi ambapo mwenyeikti alitoka nje na kamati yake ya utendaji na pindi waliporejea walikubali ombi hilo na kusema watafuata taratibu za kikatiba.
Mwisho kupitia mkutano mkuu wa leo wa wanachama umeazimia kuwaongezea muda wa mwaka mmoja Mwenyekiti Yusuf Manji pamoja na Makamu wake Clement Sanga ili waweze kukamilisha masuala ya katiba na kuweza kuandaa mkutano wa uchaguzi baada ya katiba kupitishwa na TFF.

STARS MAMBO SAFI JIJINI HARARE, WAINYAMAZIMA ZIMBABWE KWAO NA KUSONGA MBELE AFCON

Taifa stars ya Mart Nooij itakabiliana na Msumbiji katika mchezo wa mwisho wa mtoano kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morroco.
Hii imetoAFCON_2015_LOGO-MOROCCOkana na sare ya 2-2 waliyopata jioni hii dhidi ya wenyeji wao, timu ya taifa ya Zimbabwe.
Zimbabwe walioripotiwa kuwafanyia hujuma vijana wa Tanzania wameambulia patupu leo hii baada ya kuoneshwa soka safi na vijana wa Tanzania.
Haikutegemewa kuwa mechi ya mabao mengi kiasi hiki, lakini Zimbabwe ndio walianza kuamsha `mizimu` ya vijana wa Taifa stars waliokuwa wanamtazama kiongozi wao wa msafara, Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwa jukwaani.
Bao la dakika ya 10 walilopata Zimbabwe kupitia kwa Phiri Danisa  liliwashitua mashabiki wa Tanzania, lakini nahodha wa Taifa Stars, Nadir Haroub Canavaro katika dakika ya 21 aliwazisha bao hilo na kuufanyaubao wa matangazo kusomeka 1-1 mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Wakati Zimbabwe wakiwa katika presha ya kusaka bao la pili, dakika ya 46 kipindi cha pili walifanya makosa na Thomas Emmanuel Ulimwengu hakufanya makosa na kuwaadhibu goli la pili.
Dakika ya 55 kipindi hicho cha pili, Katsande Willard  aliifungia Zimbabwe bao la pili la kusawazisha.
Baada ya hapo mpira ulianza kuchezwa kwa timu zote kutafuta mabao zaidi, lakini wenyeji ndio walikuwa kwenye presha kubwa zaidi kwasababu tayari Stars walikuwa na mtaji wa mabao zaidi.
Taifa stars ya Mart Nooij ilionesha kiwango safi na upinzani mkubwa ugenini na kuwafurahisha watanzania wachache waliokuwa uwanjani na waliokuwa wanaangalia kupitia televisheni.
Haikuwa kazi nyepesi kwa vijana wa Tanzania kuwafunga Zimbabwe, lakini jitihada kubwa walizofanya na kutambua kuwa mamilioni ya watanzania wapo nyuma yao, ilitosha kuwapa morali kubwa.
http://dailynews.co.tz/images/STARSULIMWENGUU.jpgMechi ya kwanza ambayo Stars ilishindi bao 1-0 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, tatizo kubwa lilionekana katika safu ya kiungo, lakini leo vijana walijidhatiti na kuonesha kandanda zuri.
Canavaro amekuwa kiongozi wa kuigwa kwani alionesha ushupavu wa kuwaelekeza njia wenzake ikiwemo kufunga bao muhimu la kusawazisha.
Beki kazi yake ni kulinda, inapofika wakati anafunga, basi amejiongezea majukumu kwa lengo la kuisaidia timu yake ipate mafanikio.
Kuwa nahodha sio kuvaa kitambaa tu bali ni pamoja na kuisaidia timu kama wanavyofanya akina Sergio Ramos.
 Kazi nzuri Nadir Haroub `Canavaro`.
Ulimwengu ni mchezaji wa TP Mazembe. Kuna faida ya kuwa na wachezaji wa kimataifa kama yeye. Kudhihirisha umuhimu wake, alifunga bao safi na kuwavusha watanzania hatua inayofauta. Kazi nzuri kijana.
Kwa matokeo ya leo, Taifa stars imefuzu hatua ya mwisho ya mtoano kwa wastani wa mabao 3-2 kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika.
Hii inatokana na ushindi wa bao 1-0 iliopata uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa kwanza na matokeo ya 2-2 mjini Harare jioni hii.
Kwa maana hiyo, Taifa Stars inajiandaa kuutafuna mfupa wa Msumbiji katika hatua ya mwisho ya mtoano.
Msumbiji walifuzu hatua hiyo kwa wastani wa mabao 5-0 baada ya juzi kutoka suluhu ya bila kufungana na Sudan Kusini Ugenini, wakati waliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 mjini Maputo.
Msumbiji wana historia ya kuwaharibia Taifa stars katika michezo muhimu ya mashindano, hivyo ni jukumu la wachezaji na kocha Nooij kupanga mikakati kabambe ya kuwanyamazisha `Mamba hao weusi`.
Mechi nyingine iliyomalizika jioni hii ni baina ya Lesotho na Liberia na kushuhudia Lesotho wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
 

Kikosi chaTaifa Stars; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mwinyi Kazimoto, Simon Msuva/Said Mourad dk78, Amri Kiemba/Frank Domayo dk62, John Bocco, Thomas Ulimwengu/Mrisho Ngassa dk88 na Erasto Nyoni.
Jumapili Juni 1
Zimbabwe 2 Tanzania 2 [2-3]
Lesotho 2 Liberia 0 [2-1]
14:30 Congo v Namibia [0-1]
15:00 Benin v Sao Tome And Principe [2-0]
15:00 Chad v Malawi [0-2]
16:00 Equatorial Guinea v Mauritania [0-1]
 Nchi ambazo zimeingia Makundi moja kwa moja: Nigeria, Ghana, Ivory Coast, Zambia, Burkina Faso, Mali, Tunisia, Algeria, Angola, Cape Verde, Togo, Egypt, South Africa, Cameroon, DR Congo, Ethiopia, Gabon, Niger, Guinea, Senegal and Sudan.
 KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Taifa stars vs Msumbiji

Mechi ya kwanza 18–20 Julai
 mechi ya pili1–3 Agosti