Uongozi wa klabu ya Yanga umemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari Kocha mbrazil Marcio Marcel Maximo kama ndio
kocha atakayeweza kukinoa kikosi cha timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara.
kocha atakayeweza kukinoa kikosi cha timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara.
Utambulishwaji huo ulifanywa katika
makao makuu ya Klabu hiyo jijini Dar es salaam na kuuzuliwa na waandishi
wa habari wengi pamoja na wanachama waliokuwa nje kwa ajili ya
kumshuhudia kocha huyo.
Wakala aliyefahamika kwa jina moja la Ally ndiye aliyeweza kufanikisha mipango hiyo ya kumleta maximo.
"nawashukuru wana Yanga kwa uvumilivu wao kwani kwa miaka mitatu sasa nawasiliana na Marcio Maximo "
aliseama Ally na kuongeza kuwa mtazamo wa kocha huyo ni kuinua vipaji
na kuwataka wana Yanga wavumilie na kumpa muda kwa ajili ya kupata
mafanikio.
Naye Maximo amesema kuwa sio rahisi
kuipandisha timu ya Yanga na kupata mafanikio makubwa bali kwa
kushirikiana kila kitu kitafanikiwa.
"Wakati nakuja kwa mara ya kwanza
nilikuwa nasikia Yanga na Simba,lakini niliporejea tena kwa mara ya pili
sasa nasikia Azam, mbeya City na virabu vingine" alisema kocha huyo
huku akikubali kuwa upinzani ni mkubwa.
Kocha Marcio Maximo anaaza
kazi rasmi Siku ya Jumatatu na na atakuwa na msaidizi wake Leonardo
Neiva ambapo watajihusisha sana na Vijana pamoja na timu ya wakubwa.