Friday, June 27, 2014

RASMI:COUTINHO WA YANGA AWASILI DAR

Coutinho (kushoto) akiwa na msemaji wa Yanga Baraka Kizuguto
Kiungo mshambuliaji Mbrazil Andrey Macrcel Ferreira Coutinho amewasili leo na tayari kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha Young Africans kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2014/2015

MAXIMO ATAMBULISHWA RASMI YANGA,NA HUU NDIO MKATABA ALIOPEWA

Uongozi wa klabu ya Yanga umemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari Kocha mbrazil Marcio Marcel Maximo  kama ndio
kocha atakayeweza kukinoa kikosi cha timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara.
Utambulishwaji huo ulifanywa katika makao makuu ya Klabu hiyo jijini Dar es salaam na kuuzuliwa na waandishi wa habari wengi pamoja na wanachama waliokuwa nje kwa ajili ya kumshuhudia kocha huyo.
Wakala aliyefahamika kwa jina moja la Ally ndiye aliyeweza kufanikisha mipango hiyo ya kumleta maximo.
"nawashukuru wana Yanga kwa uvumilivu wao kwani kwa miaka mitatu sasa nawasiliana na Marcio Maximo " aliseama Ally na kuongeza kuwa mtazamo wa kocha huyo ni kuinua vipaji na kuwataka wana Yanga wavumilie na kumpa muda kwa ajili ya kupata mafanikio.

Maximo amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuifundisha Yanga na amekuja na msaidizi wake Leonardo Neiva.
Naye Maximo amesema kuwa sio rahisi kuipandisha timu ya Yanga na kupata mafanikio makubwa bali kwa kushirikiana kila kitu kitafanikiwa.
"Wakati nakuja kwa mara ya kwanza nilikuwa nasikia Yanga na Simba,lakini niliporejea tena kwa mara ya pili sasa nasikia Azam, mbeya City na virabu vingine" alisema kocha huyo huku akikubali kuwa upinzani ni mkubwa.
Kocha Marcio Maximo  anaaza kazi rasmi Siku ya Jumatatu na na atakuwa na msaidizi wake Leonardo Neiva ambapo watajihusisha sana na Vijana pamoja na timu ya wakubwa.

BRAZIL KOMBE LA DUNIA 2014 HATUA YA 16 BORA DIMBANI KESHO.

Michuano ya Kombe la Dunia huko Brazil sasa zimeingia Hatua ya Mtoano na zipo Timu 16 zinazowania kutinga Robo Fainali.

KOMBE LA DUNIA

RAUNDI YA PILI YA MTOANO
Saa za Bongo
JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
19:00 usiku
49
Brazil v Chile
Mineirão
Belo Horizonte
23:00 usiku
50
Colombia v Uruguay
Maracanã
Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
19:00 usiku
51
Netherlands v Mexico
Castelao
Fortaleza
23:00 usiku
52
Costa Rica v Greece
Pernambuco
Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
19:00 usiku
53
France v Nigeria
Nacional
Brasilia
23:00 usiku
54
Germany v Algeria
Beira-Rio
Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
19:00 usiku
55
Argentina v Switzerland
Corinthians
Sao Paulo
23;00 usiku
56
Belgium v USA
Fonte Nova
Salvador

Sunday, June 15, 2014

STARS KWENDA BOTSWANA JUNI 24 KUJIWINDA DHIDI YA MSUMBIJI.

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini wiki ijayo kwenda Botswana kuweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na mchezo dhidi ya Msumbiji kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco.
Wachezaji wote wa Taifa Stars waliruhusiwa kurejea makwao jana kwa ajili ya kujiandaa na safari hiyo na watakutana tena kesho.
 Stars inayofundishwa na Mholanzi, Mart Nooij itaondoka nchini Juni 27 kwenda Gaborone, ambako itaweka kambi ya mazoezi hadi Julai 7 itakaporejea nchini.  
Taifa Stars itamenyana na Msumbiji ‘Mambas’ katika hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco baada ya kuitoa Zimbabwe juzi kwa jumla ya mabao 3-2, ikianza kwa ushindi wa 1-0  nyumbani na kumaliza kwa sare ya 2-2 juzi mjini hapa.
Mechi yake kwanza itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu. 
Stars pia inatarajiwa kuwa na mchezo wa kujipima nguvu na Uganda kabla ya kumenyana na Msumbiji.

TFF YASIMAMISHA UCHAGUZI SIMBA YAITAKA UENDE KAMATI YA MAADILI.



RAIS wa TFF, Jamal Malinzi, ametangaza kusimamishwa Uchaguzi Mkuu wa Simba hadi Klabu hiyo itakapounda Kamati ya Maadili kwa mujibu wa Katiba ya TFF.
Uchaguzi Mkuu Simba ulipangwa kufanyika Juni 29 na uamuzi huu wa TFF uliotangazwa Leo kwenye Mkutano wake na Wanahabari unaitaka Simba kuunda Kamati ya Maadili ifikapo Juni 30 na Kamati hiyo ndio itakayoshughulikia masuala yote ya Maadili kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.
Uamuzi huu wa TFF unaendelea kumweka Madarakani Mheshimiwa Ismail Aden Rage hadi hapo Uchaguzi utakapofanyika baada ya Katiba yao kurekebishwa na kujumuisha Kamati ya Maadili.
Uchaguzi wa Simba umekumbwa na vuta nikuvute Klabuni hasa baada ya Mgombea Michael Wambura kuenguliwa kugombea Urais na Kamati ya Uchaguzi ya Simba na yeye kukata Rufaa TFF ambako Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake Wakili Julius Lugaziya, ilimpitisha na kuamua aruhusiwe kugombea.
Hivi karibuni, Yanga walipitisha uundwaji wa Kamati ya Maadili ya Klabu yao ili kutii amri ya TFF kwenye Mkutano Mkuu wao huko Bwalo la Polisi –Oysterbay, Jijini Dar es Salaam.
Lakini hatua hiyo ililazimu Mkutano huo kumwongezea muda wa Mwaka mmoja Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuf Manji, ili aweze kukamilisha masuala ya marekebisho ya Katiba yao na kujumuisha Kamati ya Maadili na pia kuweza kuandaa Mkutano wa Uchaguzi baada ya Katiba mpya kupitishwa na TFF.

Saturday, June 7, 2014

MASHABIKI WA YANGA MBEYA WAUTAKA UONGOZI WA YANGA KUMUELEZA MAXIMO KUZIBA PENGO LA KAVUMBAGU

Mashabiki na wadau wa soka mkoani mbeya wameutaka Uongozi wa Yanga sc kuhusu wameutaka uongozi huo kupendekeza kumweleza kocha mpya anayetarajiwa kuja kuinoa yanga kocha Marcio Maximo kumpata mshambuliaji mahiri wa kuziba nafasi ya Didier Kavumbagu, kabla ya kuanza kukinoa kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi ya Tanzania Bara.

Wakizungumza na mtandano wa mkali wa dimba kupitia sayari ya michezo wames
ema kuwa kutokana habari zilizo tolewa katika Mkutano Mkuu wa marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika salama na furaha kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay huku wanachama wakipitisha kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.
katika kikao cha wanachama wa club ya yanga kilicho fanyika Juni 1 mwaka huu uongozi wa yanga Ulimtangaza kuwa Maximo kama kocha anayetarajiwa kuinoa Yanga.

Wamesema kuwa Maximo anatakiwa kutazama mchezaji sahihi atakae ziba pengo la mshambuliaji Didier Kavumbagu kwa ajili ya kuunda upya timu hiyo licha ya kuwa na Wachezaji wengi katika safu ya Ushambuliaji.
 Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kutoka ndani ya yanga Taarifa zinasema mazungumzo na Kocha Maximo yamefikia sehemu nzuri kwa ajili ya kuja Tanzania kuinoa Yanga SC.

TFF YATOA RAMBIRAMBI MISIBA YA KANALI MWANAKATWE NA GEBO PETER!

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wake (wakati huo ikiitwa FAT), Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe kilichotokea leo asubuhi (Juni 7 mwaka huu) katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam.
TFF_LOGO12
Kwa mujibu wa binti wa marehemu, Sophia, baba yake alianguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Lugalo ambapo ndipo umauti ulipomfika wakati madaktari wakimpatia matibabu.
Kanali Mwanakatwe alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1993 mjini Kibaha mkoani Pwani.
Baada ya kuondoka FAT, aligombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kufanikiwa kushinda katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1997.
Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini na Afrika kwa ujumla kwani, Kanali Mwanakatwen enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi, na mkufunzi wa utawala wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Pia aliwahi kuwa Kamishna wa CAF.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kanali Mwanakatwe, DRFA, na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake nyumbani kwake Mbezi Beach karibu na hoteli ya Giraffe wakati ndugu wakisubiriwa kutoka mikoani. TFF tunasubiri taratibu hizo ili tujipange jinsi ya kushiriki katika msiba huo.
Sisi sote ni waja wake Mola. Hakika kwake tutarejea.