Sunday, July 20, 2014

MUJICA ASEMA SUAREZ ANAHITAJI DAKTARI SAIKILOGIASI KIFUNGO

RAIS wa Uruguay, Jose Mujica, bado ameendelea ameponda Kifungo cha Mchezaji wa Nchi hiyo Luis Suarez cha Miezi Minne alichopewa na FIFA na badala yake anahitaji msaada wa Madaktari wa Magonjwa ya Akili.
Suarez alifungiwa Miezi Minne kutojishughulisha na chochote kuhusu Soka na pia kufungiwa Mechi 9 za Uruguay baada kupatikana na hatia ya kumuuma Meno Beki wa Italy, Giorgio Chiellini, wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy huko Brazil hapo Juni 24.
Akiongea na Gazeti la Brazil, Folha de Sao Paulo, Rais Mujica, ambae ndie anasifika ya kuwa Rais ‘maskini’ kupita yeyote Duniani kwa uamuzi wake wa kuishi kwenye Banda la Shambani kwake badala ya Ikulu akilindwa na Polisi Wawili tu na Mbwa wake Manuela mwenye Miguu Mitatu, amesema: “Anatoka Familia fukara na akili yake ni Miguu yake. Ni bora kumpeleka Hospitali ambako atapata msaada
wa Daktari wa Magonjwa ya Akili!”
Rais Mujica amefafanua: “Ni wehu kumfungia Mtu asishiriki lolote kuhusu Soka! Hata Serikali haina mamlaka ya kumzuia Mtu asiingie Uwanja wa Mpira bila kupata Saini ya Jaji! Lakini FIFA wanakuja wanamfungia Miezi Minne bila hata kuwa na Jopo la Kisheria!”
Hivi sasa Suarez ameihama Klabu yake Liverpool ya England na kutua Barcelona ya Spain.
Na Rais Mujica amenung’unika: “Sasa tutamuona Suarez akicheza pamoja na Neymar na Messi lakini sijui lini itakuwa hivyo!”

SALAH UPO UWEZEKANO WA KUWEPO CHELSEA MATATANI AITWA KWAO MISRI

Mohamed Salah Mchezaji wa Chelsea huenda asiichezee tena Chelsea kwa Kipindi cha Miaka Mitatu baada ya kuitwa Nchini kwao ili aende Jeshini kwa Mujibu wa Sheria.
Taarifa kutoka Misri zimedai kuwa Salah, mwenye Miaka 22 na ambae alijiunga na Chelsea Mwezi Januari Mwaka huu kutoka Basle ya Uswisi, ameruhisiwa kuishi Nchini Uingereza kwa sababu anajihusisha na Masomo.
Hivi sasa imeripotiwa kuwa Wizara ya Elimu ya Juu ya Misri imefuta Masomo hayo na kumtaka arudi Misri mara moja ili atumikie Jeshini kwa Mujibu wa Sheria kwa Kipindi cha kuanzia Mwaka Mmoja hadi Mitatu.
Hata hivyo, Mchambuzi wa Soka kutoka Misri alisema vitu hivyo ni kawaida huko kwao na mara nyingi Mastaa wanaowakilisha vyema Nchi zao huruhusiwa kuendelea na shughuli zao bila bughudha.
Hivi sasa, Chama cha Soka cha Misri, Makocha wa Timu ya Taifa ya Misri na Maafisa wa Wizara ya Elimu ya Juu ya Misri, wameandaa Kikao ili kuangalia nini cha kufanya kuhusu Salah.
Vile vile, Meneja wa Timu ya Taifa ya Misri, Shawky Gharib, amemwomba Waziri wa Vijana kusaka suluhisho la tatizo hilo ili kumruhusuSalah arejee Misri Mwezi Septemba kuichezea Nchi hiyo kwenye Mechi za Makundi za kuwania Nafasi za kucheza Fainali za AFCON 2015 huko Morocco Mwakani.
Ikiwa hali ya sasa itaendelea Salah akirudi kwao tu hataruhusiwa kutoka nje ya Nchi hadi atumikie Jeshi kwa Kipindi hicho cha Mwaka mmoja hadi mitatu.


Mohamed Salah
Personal information
Full name Mohamed Salah Ghaly
Date of birth 15 June 1992 (age 22)
Place of birth Basion, El Gharbia, Egypt
Height 1.75 m (5 ft 9 in)
Playing position Winger
Timu ya sasa
Current team
Chelsea
Number 15
Timu za vijana
2006–2010 El Mokawloon
Timu za ukubwani
Years Team Mechi (Goli)
2010–2012 El Mokawloon 41 (11)
2012–2014 Basel 47 (9)
2014– Chelsea 10 (2)
Timu ya taifa
2010–2011 Egypt U20 11 (3)
2011–2012 Egypt U23 11 (4)
2011– Egypt 29 (17)

Friday, July 18, 2014

SIO NDOKI NG"O MAN CITY - TOURE NIPO SANA

KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure amesema kuwa hana mpango wa kuondoka kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu na kudai ataendelea kuwepo hapo kwa msimu mwingine unaokuja. Toure aliiambia luninga ya Sky Sport kuwa mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wema kwake na kwa familia hivyo ameona ni bora abaki kwa ajili yao.  kuhamia katika vilabu mbalimbali toka wakala wake Dimitry Seluk Vyombo vya habari vimekuwa vikimhusisha kiungo huyoalipoandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa nyota huyo hajatulia. Seluk alitoa madai kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast hakupewa utambulisho rasmi na klabu katika siku yake ya kuzaliwa wakati wa safari yao ya Abu Dhabu huku Toure mwenyewe akiunga mkono kauli hiyo. Toure amesema kwasasa mambo yote yako sawa na baada ya tetesi nyingi kuzungumziwa juu yake anaaka kufanya kitu kwa ajili ya mashabiki. Nyota huyo alijiunga na City akitokea Barcel
ona mwaka 2010 na haraka alijitengenezea jina na kua mchezaji tegemeo wa timu hiyo aliyoisaidia kushinda Kombe la FA mwaka 2011 na mataji mawili ya Ligi Kuu mwaka 2012 na 2014.

MALINZI ATOA NENO KUHUSU SUALA LA UPANGAJI MATOKEO.

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini-TFF, Jamal Malinzi amekemea vikali wimbi la upangaji matokeo mechi za kimataifa lililoibuka huko katika nchi za bara la Asia ambapo sasa inasemekana limeshafika mpaka Afrika. 

Malinzi ametoa kauli hiyo katika futari aliyoandaa jana kwa wadau mbalimbali wa michezo kikiwemo kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys katika ofisi za shirikisho hilo, Dar es Salaam. Malinzi amesema ana uhakika kuwa balaa hilo la upangaji mechi za kimataifa limeingia Afrika huku wanaofanya shughuli hizo wakiwashawishi viongozi, makocha na hata wachezaji ili matokeo yapatikane wanavyotaka wao.

 Malinzi amesema sio suala la kuficha tena kuhusu janga hilo na kuwaomba wadau na viongozi wa dini waliokuwepo katika shughuli hiyo kuungana ili kuwakemea vijana wao kuhusu suala hilo. Mojawapo ya viongozi mbalimbali waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida, Katibu Mkuu wa zamani wa TFF enzi hizo ikiitwa FAT Said El Maamry na viongozi mbalimbali wa timu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la kwanza Tanzania bara.

WIKIENDI BURUDANI MWANZO MWISHO AFCON 2015-MOROCCO

RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumamosi Julai 19
16:00 Uganda v Mauritania
16:30 Botswana v Guinea-Bissau
19:30 Sierra Leone v Seychelles
Jumapili Julai 20
16:00 Lesotho v Kenya
16:00 Tanzania v Mozambique
17:30 Congo v Rwanda
18:00 Benin v Malawi
MAKUNDI:
KUNDI A
-Nigeria
-South Africa
-Sudan
-Mshindi Congo/Rwanda
KUNDI B
-Mali
-Algeria
-Ethiopia
Mshindi Benin/Malawi
KUNDI C
-Burkina Faso
-Angola
-Gabon
-Mshindi Lesotho/Kenya
KUNDI D
-Ivory Coast
-Cameroun
-Congo DR
-Mshindi Sierra Leone/Seychelles
KUNDI E
-Ghana
-Togo
-Guinea
Mshindi Uganda/Mauritania
KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Mshindi Tanzania/Msumbiji
KUNDI G
-Tunisia
-Egypt
-Senegal
-Mshindi Botswana/Guinea-Bissau

UEFA YAWEKA HADHARANI MAJINA 10 KUWANIA MCHEZAJI BORA ULAYA!

Katika kuelekea katika michuano ya Uefa champions Ligi Jana UEFA imetoa Majina ya wanandinga 10 Wanao gombea Tuzo yao ya Mchezaji Bora wa Mwaka na Mshindi atatangazwa hapo Agosti 28 wakati wa Droo ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Awali Majina ya Wachezaji 35 yalipigiwa Kura na hao 10 ndio kuibuka kidedea.
Lakini Majina hayo 10 yatachujwa kwa Kura hapo Agosti 14 na kubakisha Majina Matatu yatakayopigiwa Kura na kutangazwa Mshindi hapo Agosti 28.
WASHINDI WALIOPITA:
2010–11 Lionel Messi [Barcelona]
2011–12 Andrés Iniesta [Barcelona]
2012–13 Franck Ribéry [Bayern Munich]
Wapigaji Kura ya Tuzo hii ni Jopo la Wanahabari maalum toka Nchi zote Wanachama wa UEFA.
Miongoni mwa Majina makubwa ambayo hayamo kwenye Listi hii ya Wachezaji 10 ni yale ya Zlatan Ibrahimovic, Gareth Bale na Neymar.
JAMES-RODRIGUEZ-COLOMBIALakini yapo Majina ya Wachezaji Watatu toka Kikosi kilichochukua Kombe la Dunia cha Germany Jumapili iliyopita huko Brazil na pia yupo James Rodriguez alietwaa Buti ya Dhahabu huko Brazil kwa kuwa Mfungaji Bora wa Kombe la Dunia akiichezea Nchi yake Colombia.
Bila kustajabisha, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, ni miongoni mwa Wagombea.
Tuzo hii ilianzisha na UEFA Mwaka 2011 ili kuziba pengo la Ballon d'Or ambayo iliunganishwa na Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na pia kuibadili ile Tuzo ya zamani ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Klabu.
LISTI YA WAGOMBEA 10:
-Diego Costa [Spain, Atletico Madrid]
-Angel Di Maria [Argentna, Real Madrid]
-James Rodriguez [Colombia, AS Monaco]
-Luis Suarez [Liverpool (Sasa Barcelona), Uruguay]
-Philipp Lahm [Germany, Bayern Munich]
-Thomas Muller [Germany, Bayern Munich]
-Manuel Neuer [Germany, Bayern, Munich]
-Arjen Robben [Germany, Bayern Munich]
-Cristiano Ronaldo [Portugal, Real Madrid]
-Lionel Messi [Argentina, Barcelona]

KIINGILIO MECHI YA STARS, MSUMBIJI 7,000/- VITI MAALUM (VIP) 30,000/-

Viingilio kwa mechi ya Taifa Stars na Msumbiji itakayochezwa keshokutwa (Jumapili) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni sh. 7,000 na sh. 30,000 kwa viti maalumu 4,500 tu.
Kuanzia kesho asubuhi (Jumamosi) tiketi za kielektroniki zitauzwa pia katika magari maalumu kwenye vituo vya Buguruni Shell, Dar Live Mbagala, Ferry Magogoni, Kigamboni, OilCom Chang’ombe, OilCom Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa (Kariakoo), TCC Club Chang’ombe na Uwanja wa Taifa.
TFF-TANZANIA-MSUMBIJIAidha tiketi zinapatikana kupitia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha bonyeza 4,  bonyeza tena 4 kisha weka namba ya kampuni 173399 kisha ingiza 7000 kama namba ya kumbukumbu ya malipo, kisha andika tena 7000 kwenye weka kiasi, kasha weka namba ya siri na baadaye bonyeza  1 kukubali.
Utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo vya kuchukua tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo yako.
Vituo vya MaxMalipo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre, Tabata Segerea na kituo cha daladala Makumbusho), Sheer Illussions (Millennium Tower na Mlimani City), maduka makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na Upanga).
Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station (Mbezi Beach), Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA (Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na Uwanja wa Karume.
TFF-MPESA-MALIPO
SEMINA ELEKEZI AIRTEL RISING STARS
Semina elekezi ya michuano ya Airtel Rising Stars kwa mikoa sita inafanyika kesho (Julai 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Washiriki wa semina hiyo ni kutoka mikoa ya Mbeya (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Mwanza (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Morogoro (Katibu), Ilala (Katibu na mwakilishi wa wanawake).
Temeke (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Kinondoni (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Dar es Salaam (Mwenyekiti na Katibu), na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kitakachowakilishwa na mwakilishi wa wanawake.
Washiriki wengine katika semina hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ni wajumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana ya TFF.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)