Thursday, August 14, 2014

PHIRI AJITIA KITANZI CHA MWAKA MMOJA MSIMBAZI.


Mzambia Patric Phiri hii leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kuitumikia club yake ya zamani kwa msimu mpya wa ligi kuu ya vodacom inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi September 20 mwaka huu raia huyo wa Zambia amesaini mkataba huo kwenye Hoteli ya Regency.
Phiri ameiambia mkali wa dimba tz kuwa mkataba huo unampa fursa kubwa katika kuitumikia Simba kwa matumaini makubwa.

Phiri maheshima ya Simba kwangu ni kubwa sana, ingawa nilikuwa nina mipango mingine, lakini nimekubali kurejea hivyo haitakuwa Kazi rahisi, lakini uzuri sasa tumeingia mkataba mpya wa kazi ninaamini mambo yatakwenda vizuri sana.
Phiri amesema heshima kuwa ya kwangu ni kubwa ambapo miaka ya nyumba nilikuwa Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010.
Patrick Phiri ni Kocha mkongwe ambapo sana katika soka la afrika ambapo amazaliwa Mei 3 mwaka 1956.
Kwa phiri hii na mara ya nne kufanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi zake.
Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.

 
Taarifa Binafsi
Date of birth 3 May 1956 (age 58)
Place of birth Luanshya, Northern Rhodesia
Paying position Forward (retired)
Timu za Vijana
Years Team Mechi Goli
1973–1974 Buseko FC

1974-1975 Rokana United
(21)
1975–1986 Red Arrows

Kuwa Kocha
1986-1991 Red Arrows
1992–1994 Ndeke Rangers
1995–1997 Lusaka Dynamos
1997 Mochudi Centre Chiefs
1997–2002 Nkana F.C.
2002–2003 Zambia
2003–2005 Simba
2006–2008 Zambia
2008–2011 Simba
2012 NAPSA Stars           

                                 

ANDREW CHARLES ASAINI MIWILI JANGWANI



Mlinzi wa kushoto wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Andrew Charles Manyama kutoka timu ya JKT Ruvu Stars leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2) tayari kwa kuitumikia timu ya Young Africans SC kuanzia msimu huu wa 2014/2015.

Andrew Charles Manyama beki wa kushoto wa timu ya Taifa Tanzania amekamilisha taratibu zote kutoka katika timu yake ya JKT Ruvu leo mchana na sasa kuanzia kesho ataonekana katika mazoezi ya kikosi cha kocha mkuu Marcio Maximo tayari kwa mikikimikiki ya VPL msimu huu.
Usajili wa Manyama unafanya idadi ya wachezaji wapya msimu huu kufikia watano (5) wakiwemo washambuliaji wabrazil Andrey Coutinho, Geilson Santos "Jaja", Kiungo mkabaji Said Juma "Makapu" na mlinzi wa kati Pato Ngonyani.

BASI LA TFF LAKAMATWA NA MADALALI WA MAHAKAMA

basiBasi la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekamatwa na madalali kwa amri ya mahakama kutokana na deni la sh milioni 140 ambalo tunadaiwa hadi litakapolipwa.
Amri hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya Punchline ya Kenya iliyokuwa ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia mwaka 2007. Hadi sasa tumeshalipa sh. milioni 70 katika deni hilo.
Jitihada zinafanyika ili kumaliza deni hilo. Pia tunachunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.
CAF YAZUIA MECHI ZAKE KUPISHA EBOLA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limezuia mechi zake kuchezwa Guinea, Liberia na Sierra Leone kutokana na kuripotiwa kuwepo kwa wagonjwa wengi wa Ebola katika nchi hizo.
tff_LOGO1
Ikiwa ni njia mojawapo ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo kupitia mkusanyiko wa watu, CAF imevitaka vyama vya mpira wa miguu vya nchi hizo kuchagua viwanja vingine huru kwa ajili ya timu zao zinazoshiriki michuano yake kwa kipindi hiki hadi katikati ya mwezi ujao.
CAF itafanya tathmini nyingine kuhusiana na ugonjwa huo kuanzia katikati ya Septemba ili kuona kama nchi hizo zinaweza kupokea timu ngeni kwa ajili ya mechi mbalimbali za michuano yake, na baadaye kufanya uamuzi wa kuruhusu au kuendelea kusimamisha.
Pia kutokana na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO), CAF imesema kwa nchi zenye virusi vya Ebola ni muhimu kwa vyama vyake vya mpira wa miguu kuufanyia vipimo vya afya msafara wa timu zao ili kuhakikisha wenye virusi vya ugonjwa huo hawasafiri.

Wednesday, August 13, 2014

PHIRI ATUA JIJINI DAR KUJIUNGA WA WEKUNDU WA MSIMBAZI

Mzambia Patric phiri atua jijini dar es salaam lengo likiwa ni kufanya mazungumzo ya kina na uongozi wa club hiyo ili kusaini Mkataba wa kuifundisha klabu yake ya zamani, Simba SC ambayo hivi karibuni ulimtupia virago alikuwa kocha mkuu Logarusic.

Akitua katika viwanja wa JK nyerere hii leo mashabiki wachache walitokeza kumpokea kocha huyo hivyo asilimia kubwa ya phiri ndie atakuwa kocha mkuu wa simba kwa msimu ujao wa ligi kuu vodacom tanzania bara unao tarajiwa kuanza kutimua vumbi mnamo september 20 mwaka huu.
Katika akifundisha simba Phiri aliwahi kuwa Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, Patrick Phiri anatarajiwa kutua Dar es Salaam wiki hii kwa ajili Mzaliwa huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi zake.

Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.

Kiboko ya Yanga anarudi; Patrick Phiri anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Ijumaa kusaini Simba SCMazungumzo yamekwishanyika na makubaliano yamefikiwa baina ya Phiri na Simba SC na sasa atakuja kufanya kazi tena Msimbazi, akisaidiwa na Nahodha wake enzi zake akifundisha timu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’.

Phiri ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi moja.

Lakini pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya kipekee Msimbazi.
Katika awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.

Kwa sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye watoto wawili, Melesianiah na Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green Buffaloes ya Ligi Kuu ya Zambia.

Phiri ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia kama mshambuliaji.

Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana. 
Akiwa kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka nchini mwake mwaka 1999.

HUKUMU YA SUAREZ CAS KUJULIKANA KESHO.

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Michezo-CAS imedai kuwa hatma ya rufani ya mshambuliaji nyta wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez kupinga adhabu aliyopewa kwa kumng’ata Giorgio Chiellini itajulikana kesho. Suarez alifungiwa mechi tisa za kimataifa na kutojishughulisha na mambo yoyote yahusuyo soka kwa miezi minne baada ya kufanya tukio hilo katika mchezo wao wa hatua ya makundi. Italia kwenye michuano ya Kombe la Dunia. Baada ya kushindwa rufani yake kwa Shirikisho la Soka Duniani-FIF, mshambuliaji huyo wa Barcelona alipeleka kesi hiyo CAS ambayo ilisikiliza shauri hilo Ijumaa iliyopita. Katika taarifa yake CAS ilithibitisha kuwa itatoa uamuzi wake kuhusiana na rufani hiyo kesho.