Simba wameweka kambi visiwani
Zanzibar (Unguja) chini ya kocha mkuu mpya, Mzambia, Patrick Phiri
akisaidiwa na kocha msaidizi, kiungo wa zamani wa klabu hiyo na timu ya
taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’ na
kocha wa makipa, Idd Pazzi ‘Father’.
Monday, August 18, 2014
SIMBA YAENDELEA NA TIZI ZANZIBAR
FIFA KUBORESHA MAKAO MAKUU YA TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) yaliyoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala ili
yawe katika kiwango cha kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na vitendea kazi
na miundombinu ikiwa ni pamoja na upanuzi wa ofisi.
Hatua hiyo itaiwezesha TFF kuwa na
mazingira bora ya kufanya shughuli zake kwa ufanisi. Vilevile kupitia
programu zake mbalimbali ikiwemo ile ya Goal, FIFA imeahidi kushirikiana
na TFF katika kuendeleza mradi wa kiuchumi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume.
YANGA YATUA PEMBA KUWEKA CHIMBO LA VPL SEPT 20,2014
Msafara wa watu 35 ukiwa na wachezaji 27 na benchi la Ufundi 8 wa timu ya Young Africans
tayari umeshawasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya mwisho
kujiandaa na mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.
Kocha mkuuu Marcio Maximo na kikosi chake wamefikia katika hoteli ya
kitalii ya Pemba Misali iliyopo eneo la Wesha na watakua wakijifua kwa
muda wa takribani siku 10 kabla ya kurejea jijini Dar es salaam mwisho wa mwezi huu.

Kikosi
cha Young Africans kitakua kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani
mjini Chake Chake na siku ya alhamis wanataraji kucheza wa kwanza wa
kirafiki dhidi ya timu ya Chipukizi ya kisiwani Pemba.
Kulingana na program ya bench
la Ufundi kisiwani Pemba, Young Africans inatarajia kucheza michezo
mitatu ya kirafiki na timu za kutoka Visiwa vya Pemba na Unguja na
baadae kurejea Dar es salaam kwa michezo mwili ya kimataifa kabla ya
kucheza mchezo wa Ngao ya Hisani septemba 13, 2014.
Wachezaji waliondoka kuelekea Pemba ni:
Walinda Mlango:
Juma Kaseja, Ally Musatfa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida"
Walinzi wa Pembeni:
Juma Abdul, Salum Telea, Oscar Joshua, Edwad Charles na Amos Abel
Walinzi wa Kati:
Kelvin Yondani, Nadir Haroub "Cannavaro", Rajab Zahir na Pato Ngonyani.
Viungo:
Mbuyu Twite, Said Juma "Makapu", Omega Seme, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Hamis Thabit.
Viungo wa Pembeni:
Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Nizar Khalfani na Andrey Coutinho.
Washambuliaji:
Geilson Santos "Jaja", Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Hamis Kizza na Hussein Javu
Benchi la Ufundi walioko Kisiwani Pemba ni:
Kocha Mkuu : Marcio Maximo
Kocha wasaidizi Leonado Neiva, Salvatory Edward
Kocha wa Makipa: Juma Pondamali
Daktari wa timu: Dr Suphian Juma
Meneja wa timu: Hafidh Saleh
Mchua Misuli: Jaco Onyango
Mtunza Vifaa: Mahmod Omar "Mpogolo"
Saturday, August 16, 2014
MAN UNITED YAPOLEA KIPONDO NYUMBANI 2-1 SWANSEA CITY
MENEJA mpya wa klabu ya
Manchester United ameanza vibaya kampeni zake za Ligi Kuu baada ya
kushuhudia kikosi chake kikitandikwa mabao 2-1 dhidi ya Swansea city katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Old Trafford
mchana wa leo.
Wageni Swansea ndio waliokuwa wa kwanza kuchukuliwa wavu
wa United kwa bao lililofungwa na Ki Sung-yueng katika dakika ya 28
lakini bao hilo lilisawazishwa muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha
pili kupitia kwa nahodha wake Wayne Rooney.

United walionekana
kushindwa kabisa kutengeneza mipango ya kusawazisha bao hilo hatua
ambayo mashabiki wake walionnekana kukata tamaa na kuanza kuondoka
mapema uwanjani kabla ya mchezo kumalizika.
Mashabiki wa United duniani
kote kabla ya mchezo walionekana kuwa na imani kubwa na kikosi chao toka
alipotua Van Gaal akichukua mikoba ya David Moyes ambaye alifanikiwa
kushinda mechi zake zote za kirafiki alizocheza.
AZAM FC YAIFUMUA 4-1 ADAMA CITY KOMBE LA KAGAME CUP
Mabingwa wa tanzania bara 2013-2014
azam fc imekamilisha hayau ya makundi imemaliza katika klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuichalaza mabao 4-1 Adama City ya
Ethiopia Uwanja wa Nyamirambo mjini hapa.
Kwa matokeo hayo Azam FC ya Tanzania Bara, imekwea kileleni mwa Kundi A kwa kufikisha pointi nane baada ya mechi nne, ikishinda mbili na sare mbili na hatimaye kutinga hatua ya bRobo Fainali.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika
timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, Azam wakitangulia kupitia kwa Nahodha
John Bocco ‘Adebayor’ akiunganisha krosi ya Khamis Mcha ‘Vialli’ kabla ya
Desaleny Debesh kuisawazishia Adama dakika ya 39.
Refa Mohamed Hassan kutoka Somalia alikataa bao la Kipre Herman Tchetche dakika ya 42, akidai kipa alibughudhiwa na kipindi cha pili Azam iliingia na moto mkali na kufanikiwa kuongeza mabao matatu.
Kocha Mcameroon Joseph Marous Omog alifurahia matokeo hayo na akasema sasa anajipanga kwa Robo Fainali.
Kikosi cha Azam FC; Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Gardiel Michael/Said Mourad dk51, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Khamis Mcha ‘Vialli’/Farid Mussa dk61, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Mudathir Yahya dk72, John Bocco ‘Adebayor’, Didier Kavumbangu na Kipre Tchetche.
MAXIMO ATOA NENO KWA PATRIC PHIRI KUHUSU VPL SEPT 20
Maximo alichukua nafasi ya Mholanzi, Hans van Der Pluijm
huku Phiri akiwa amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Simba baada ya
kuchukua mikoba iliyoachwa na
Mcroatia, Zdravko Logarusic aliyetimuliwa Jumapili iliyopita.
Katikamkutano na waandishi wa habari, Maximo amesema kuwa
amemkaribisha kocha huyo ambaye anafahamu kuwa ni mzuri lakini amemtaka
kutambua ushindani uliopo wa ligi ya Tanzania.
Maximo amesema napenda kumwambia kocha mpya wa Simba (Patrick
Phiri), karibu Tanzania lakini
ajue kuwa ligi ina ushindani wa hali ya juu japo natambua kuwa yeye ni kocha
mzuri na anayeifahamu ligi ya hapa”, alisema Maximo.
Phiri ametua nchini siku chache zilizopita na kusaini
mkataba wa mwaka
mmoja kuinoa Simba, hii ikiwa ni mara ya tatu tofauti kuionoa
timu hiyo.
Kwa upande mwingine, Maximo alisema kuwa kikosi chake
kinaendelea vizuri na mazoezi ambapo kinamchanganyiko wa vijana na wakongwe
ambao wengine walikuwa kwenye timu zao za Taifa.
Maximo aliongeza kuwa beki aliyesajiliwa na timu hiyo,
Edward Charles ni mchezaji mzuri anayeamini ataisaidia Yanga kwa muda mrefu
kutokana na umri wake kuwa mdogo.
Maximo anatarajia kutaja majina ya wachezaji ataokwenda
nao kwenye kambi kisiwani Pemba na watakaa huko kwa takribani siku kumi na
baadae kurudi Dar tayari kwa kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Subscribe to:
Posts (Atom)