
Wachezaji wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli ya JB Belmont
waliwasili jana (Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) kwa nyakati tofauti.
Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Oktoba 10 mwaka
huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya
mwisho kesho (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioko kwenye kikosi cha Benin ni Stephane Sessegnon
(West Bromwich Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel
Suanon (Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg,
Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudou (JS
Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa).
Steve Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont
Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote
(Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na
Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou
(ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore
(USS Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo
(Oktoba 10 mwaka huu) itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
saa 10 jioni.
Wakati huo huo, makocha wa Taifa Stars, Mart Nooij na wa Benin
Didier Nicolle Olle watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Oktoba 11
mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika Jengo la PPF Tower.
FDL YAANZA KUTIMUA VUMBI

Kundi A litakuwa na mechi kati ya Kimondo FC na Villa Squad
itachezwa Uwanja wa Vwawa mjini Mbozi wakati Majimaji itaumana na Ashanti
United (Uwanja wa Majimaji, Songea).
Nyingine ni Kurugenzi Mafinga na Tessema FC kwenye Uwanja wa
Mufindi huku Friends Rangers ikioneshana kazi na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Kundi B ni Panone itaikabili Kanembwa JKT (Uwanja wa Ushirika,
Moshi), Oljoro JKT itapambana na Polisi Dodoma (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri
Abedi, Arusha), Polisi Mara na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Musoma).
Mechi nyingine ni kati ya Toto Africans na Mwadui itakayofanyika
Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza na Geita Gold na Burkina Faso (Uwanja wa
Waja, Geita).
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO
LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)