Thursday, November 27, 2014

FIFA YATOA LISTI YA UBORA DUNIANI TANZANIA YAPOROMOKA NAFASI 2 SAS YA 112.

SHIRIKISHO la soka Duniani FIFA Leo hii imetoa Listi ya Ubora Duniani na Mabingwa wa Dunia Germany wameendelea kushika Namba Moja huku Tanzania ikiporomoka Nafasi 2 na kukamata Nafasi ya 112.
Kulikuwa hamna mabadiliko yeyote ya Timu 7 za juu lakini England, iliyokuwa Nafasi ya 20, imepanda Nafasi 7 na sasa kukamata Nafasi ya 13.
Barani Afrika, Ageria imeendelea kuwa juu kabisa ikiwa Nafasi ya 18 baada kushuka Nafasi 3 ambapo Listi ya Ubora Duniani inayofuata itatolewa Tarehe 18 Desemba 2014.
20 BORA HII HAPA.
1.Germany               
2.Argentina   
3.Colombia    
4.Belgium      
5.Netherlands
6.Brazil
7.Portugal               
8.France
9.Spain          
10.Uruguay                
11.Italy           
12.Switzerland 
13.England                
14.Chile           
15.Romania                
16.Costa Rica  
17.Czech Republic      
18.Algeria       
19.Croatia       
20.Mexico

UONGOZI WA LIPULU FC YATUPIA VIRAGO BENCHI LA UFUNDI


Timu ya Lipuli FC ya Iringa kupitia uongozi wake umeamua kutitupilia virago benchi lake lote la ufundi kutokana na matokeo yasiyoridhisha ya timu yake katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
          
Mwenyekiti wa timu hiyo Abuu Changawa amesema wamefikia hatua hiyo baada ya timu yao kuwa na mwendo wa konokono katika ligi hiyo wakiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi A.

Pamoja na kwamba wapo katika nafasi ya tatu kwenye         msimamo wa kundi letu, matokeo ya timu yetu hayaridhishi. Tumekuwa tukishinda 1-0 na kutoka sare ndiyo maana tumeaona tuachane na watendaji wote wa benchi la ufundi,” amesema Majeki.

Lipuli FC, aliyowahi kuifundisha Shadrack Nsajigwa (sasa kocha msaidizi Yanga), imekusanya pointi 21 katika mechi zote 11 za raundi ya kwanza ya FDL, pointi moja nyuma ya Friends Rangers walioko nafasi ya pili na tatu nyuma ya Majimaji FC wanaoshika usukani wa kundi hilo.

Aidha, Majeki amesema kuanzia Alhamisi wataanza msako wa kukamata watu wote wanaojihusisha na biashara haramu ya kutengeneza na kuuza jezi zenye nembo ya klabu yao kwa kuwa hadi sasa hakuna kampuni wala mtu aliyeidhinishwa kutengeneza na kuuza jezi zenye 

EMERSON AANZA TIZI LA KUJIUNGA NA YANGA CHINI YA MAXIMO.

Mbrazil, Emerson Roque ambae anacheza nafasi ya Kiungo leo ameanza kujifua katika kikosi cha Yanga.

Taarifa zilizopo Emerson atafanya majaribio kwa wiki mbili, ambapo leo imekuwa siku ya kwanza.
                 
Katika mazoezi hayo ya Yanga kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam kulikuwa na ulinzi mkali.

Emerson ambaye inaelezwa atachukua nafasi ya mshambuliaji, Jaja alionekana kama vile amezoeana na wachezaji wengine wa Yanga.


Pamoja naye, kiungo Coutinho na Kocha Marcio Maximo, nao walianza mazoezi yao kwa mara ya kwanza baada ya kurejea nchini, jana.

Wednesday, November 26, 2014

BARCA,MADRID,BAYERN YATAWALA ORODHA YA MABEKI FIFPRO WORD XI 2014


KLABU za Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich zimetawala orodha ya mabeki wateule katika kikosi cha dunia cha FIFPro World XI 2014 chama cha wachezaji wakulipwa, baada majina 12 ya wachezaji wao kuingia katika orodha kati ya majina 20 yaliyoteuliwa.
Wachezaji wote wanne walioshinda nafasi ya kuwemo katika kikosi hicho mwaka jana wamejumuishwa wakiwemo Dani Alves, Philipp Lahm, Sergio Ramos na Thiago Silva. Leighton Baines, Ashley Cole, Dante na Nemanja Vidic ndio ambayo hayamo katika orodha hiyo ukilinganisha na ya mwaka jana. 
Kwa upande wa Madrid wamo Dani Carvajal, Pepe, Ramos, Raphael Varane na Marcelo wakati Barcelona wamo Jordi Alba, Alves, Javier Marscherano na Gerard Pique huku Bayern wakiwa na David Alaba, Lahm na Jerome Boateng. 
Mabeki wengine wnakamilisha orodha hiyo ni pamoja na David Luiz na Thiago Silva wa Paris Saint-Germain, Pablo Zabaleta na Vincent Kompany wa Manchester City, Branislav Ivanovic na Filipe Luis wa Chelsea, Diego Godin wa Atletico Madrid na Mats Hummels wa Borussia Dortmund. 
Majina manne ya washindi wa beki bora wa dunia yataamuliwa kwa kupiga kura miongoni mwa wachezaji ambapo zaidi ya wachezaji wa kulipwa 20,000 wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo.

CAF YAZINDUA MPIRA AINA YA MARHABA KUTOKA ADIDAS KWA AJILI YA AFCON 2015


SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas wametoa mpira wa Marhaba kuwa maalumu kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika huko Guinea ya Ikweta mwakani.
Mpira huo unatarajiwa kutambulishwa rasmi Desemba 3 mwaka huu katika shughuli za upangaji ratiba za michuano hiyo ambazo zitakazofanyika jijini Malabo. 
Mpira huo umebuniwa kwa rangi za aina mbalimbali ambazo zinawakilisha uwanda mpana wa bara la Afrika kuanzia jangwa la sahara, rangi ya ang’avu ya samawati katika anga la bahari ya Hindi na Atlantic. 
Mpira huo wa Marhaba umefanyiwa vipimo vyote stahiki na kuthibitishwa kuwa unaweza kutumika katika hali yeyote katika michuano hiyo.


SERIKALI YATOA SH. BILIONI 5 KIANZIO UJENZI WA JENGO LA MAABARA YA UPASUAJI.

JUMLA  ya shilingi  bilioni tano  zimetolewa  na serikali  kama kianzio cha ujenzi wa jengo la upasuaji  ujenzi wa maabara pamoja na kununua dawa katika hospitali teule ya rufaa  ya Tumbi mkoani Pwani.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Aggrey Mwanri mjini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu ambapo amekiri kuwa miundombinu ya hospitali hiyo haiendani na mahitaji yaliyopo.

Amesema kuwa ili kukabiliana na hali hiyo serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya upanuzi wa hospitali hiyo, ambapo inakadiriwa shilingi bilioni 30 zilitumika kwa ajili ya shughuli za ujenzi huo kwa mwaka 2010.

ASKARI POLISI WILAYA CHUNYA ATIWA NGUVUNI KWA TUHUMA ZA MAUAJI.

ASKARI polisi wa kitengo cha usalama barabarani Wilayani Chunya Mkoani Mbeya, PC  Zeferin Didas Focas mwenye umri wa miaka (34) amefukuzwa kazi kwa tuhuma za kuhusika na mauji ya raia Abisai Wadi mwenye miaka 22.
Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kufukwa kazi kwa askari huyo baada ya husika na mauji ya raia huyo yaliyotokea  katika Kata ya Igalula barabara ya Itindi Mkwajuni  Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Amesema,  askari huyo akiwa na mwezie aliisimamisha pikipiki iliyokuwa imempakia abiria nyuma ambapo dereva huyo alikaidi, ndipo askari huyo alichukua jiwe na kuitupia pikipiki hiyo iliyokuwa katika mwendo kasi  na kumpata abiria huyo.
Amesema, jiwe hilo linasemekana lilimkuta abiria aliyepakizwa kwenye poikipiki hiyo lakini haikuwekwa wazi kwamba jiwe hilo lilimpata katika sehemu ipi ya mwili wa marehemu huyo.

Amesema, askari huyo ambaye kwa sasa anatambulika kwa namba ya X6710 anatarajiwa kufikishwa mahakamani  ili kujibu tuhuma za mauji zinazomkabili mbele yake.