Sunday, December 7, 2014
DIAMOND AWASILI WASHINGTON, DC TAYARI KWA SHOW YA SHEREHE YA UHURU
Diamond akiwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Dulles muda huu tayari kwa makamuzi ya sherehe ya Uhuru itayofanyika muda si mrefu Sheraton, ya Downtown Silver Spring, Maryland.
Diamond akimsalimia mwenyeji wake hayupo pichani mara tu alipowasili Dulles.
Kutoka kushoto ni Dj Romy Jones, Diamond na mmoja wa waratibu wa sherehe ya Uhuru Bwn. Phanuel Ligate
Saturday, December 6, 2014
TIMU NNE ZA TZ BARA ZAALIKWA KUSHIRIKI KOMBE LA MAPINDUZI.
Timu nne za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC, Mtibwa
Sugar FC, Simba SC na Yanga SC zimealikwa kushiriki michuano ya Kombe la
Mapinduzi itakayofanyika Zanzibar Januari mwakani.
Kenyan Premier League (KPL) side AFC Leopards has for the second year in
a row landed an invite to take part in the Mapinduzi Cup in January 2015.
Jumla ya timu 11 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo mwakani kama
ilivyothibitishwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Zanzibra (ZFA), Kassim Haji
Salum katika mkutano na waandishi wa habari visiwani hapa jana Ijumaa.
Endapo klabu za Azam, Mtibwa, Simba na Yanga zitashiriki michuano hiyo,
ni wazi kwamba ratiba ya VPL italazimika kupanguliwa kwa mara ya tatu msimu huu
baada ya kufanyiwa marekebisho na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Agosti na
Oktoba mwaka huu.
Mashindano ya Kombe la Mapinduzi hufanyika kuanzia Januari 1-12/13 kila
mwaka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mapinduzi tukufu ya Zanzibar.
Ratiba ya VPL mwanzoni mwa mwaka ujao inaonesha kuwa Azam FC itawaalika
Mtibwa Sugar FC kwenye Uwanja wa Azam jijini Dar es Salaam Januari 3, Yanga SC
itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya
Januari 3 huku Simba SC itaalikwa na Mgambo Shooting Stars kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga Januari 4.
Salum aliweka wazi kuwa barua za mwaliko zinapaswa kujibiwa na klabu
kufikia Jumatatu Desemba 15, mwaka huu na mashindano yataanza rasmi Alhamisi
Januari Mosi, mwakani ambapo mbali na klabu nne za VPL, mabingwa watetezi KCCA ya Uganda pia
wamealikwa.
Timu nyingine zilizoalikwa ni pamoja na mabingwa wa Zanzibar KMKM,
Polisi, JKU, Mtende Rangers, Shaba FC na AFC Leopards ya Ligi Kuu ya Kenya
inayonolewa na Kocha James Nandwa ikishiriki kwa mara ya pili baada ya kualikwa
tena mwaka huu.
Mechi ya fainali itapigwa Uwanja wa Jumanne Januari 13 na Simba SC, ikiwa chini ya Kocha Mcroatia
Zdravko Logarusic ilifungwa bao 1-0 dhidi ya KCCA katika mechi ya fainali mwaka
huuWAWA BEKI MPYA WA AZAM FC ASEMA AMEKUJA KUTENGENEZA HESHIMA NA KUJIUZA KATIKA TIMU ZA ULAYA.
Pascal Wawa Beki mpya wa kati wa Azam FC ambae anaendelea na mazoezi na
kikosi hicho ameweka wazi na kusema kuwa kilichomleta Tanzania ni
kutengeneza heshima yake na timu kwa ujumla.
Raia huyo wa Ivory Coast ambaye majina ya wachezaji wa Yanga, Mrisho
Ngassa na Juma Kaseja ndiyo yapo kwenye akili yake kutokana na namna
anavyowafahamu.
Wawa anaamini Azam ndiyo itakuwa njia yake ya kutoka kwenda kucheza soka
la kulipwa Ulaya baada ya kushindwa kufanikisha malengo yake hayo katika klabu
ya El Merreikh ya Sudan alikocheza kwa miaka minne
Wawa amesema kwanza amekuja kucheza mpira Azam kwa malengo makubwa
mawili, kwanza ni kujitangaza ili nisonge mbele na kupata timu katika nchi
zilizoendelea Ulaya baada ya kuona nimecheza Sudani kwa miaka minne bila
mafanikio.
Pili ni kuifanya Azam ifikie malengo yaliyokusudiwa kwa kufanya vizuri
kwenye michuano ya kimataifa, lakini yote hayo nataka kuyakamilisha kwa vitendo
kimya kimya.
Wawa aliwahi kuja Tanzania kwa vipindi tofauti, kwanza akiwa na Ivory
Coast iliyoshiriki CHAN mwaka 2010 na iliyocheza Kombe la Chalenji jijini Dar
es Salaam pia amekuja na El Merreikh kwa vipindi tofauti kucheza mashindano ya
Kombe la Kagame. Wawa ni Muivory Coast wa tatu kutua kikosini hapo baada ya
Kipre Tchetche na Kipre Bolou
MSHAMBULIAJI SAIDI BAHANUZI ATUA POLISI MOROGORO KWA MKOPO
Timu ya yanga african wazee wa jangwani imemtoa mshambuliaji
Said Rashid Bahanuzi kwa mkopo katika klabu ya Polisi Morogoro.
Bahanuzi amechagua kwenda
Polisi badala ya timu zote zilizokuwa zikimuhitaji, Stand United na Ruvu
Shooting kwa kuwa anaamini huko ni sehemu sahihi kwenda kufufua makali yake.
Mshambuliaji huyo wa zamani
wa Mtibwa Sugar amejikuta katika wakati mgumu Yanga SC, baada ya kung’ara kwa
msimu mmoja tu, 2012.
Bahanuzi aliingia kwa
kishindo Yanga SC akiiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kagame la Kagame 2012 naye pia kuwa mfungaji bora.
Baada ya hapo, Bahanuzi
akaanza vizuri pia kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kabla ya kuumia
katikati ya msimu na kuwa nje hadi msimu uliofuata.

Hao ni Waholanzi Ernie
Brandts na Hans van der Pluijm pamoja na huyu wa sasa, Mbrazil Marcio
Maximo.
Tangu amejiunga Yanga SC,
Said Bahanuzi amecheza mechi 48 na kufunga mabao 15, matatu kwa penalti.
WAGANDA WAMSHANGAA ZARI THE BOSS LADY KUMZIMIA DIAMOND PLATNUMZ
![]() |
Diamond vs Zari |
Mitandao ya kijamii na
vyombo vya habari vya Uganda vimemgeuka nyota wa vipindi vya runinga na
Mwanamuziki Zari ‘The Boss Lady’ kwa madai kwamba amemganda mwanamuziki wa
Tanzania Diamond Platnumz.
Gazeti la udaku la Red
Pepper, mitandao ya ugvision.com, bigeye.ug na mingineyo, imedai kuwa nyota
huyo amemganda mwanamuziki huyo tangu alipopata upenyo wa kurekodi naye singo
jijini Dar es Salaam.
![]() |
Mama Diamond,Diamond na Zari |
Mitandao hiyo imeponda kuwa
Zari ana tabia ya kuwanadi wanaume anaotoka nao.
![]() |
Zari akiwa na Tuzo za Diamond Channeo o' |
Diamond ambaye alinyakua
tuzo tatu za Channel O 2014, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla
inayoandaliwa na Zari, ijulikanayo kama ‘Zari All White Ciroc Party’,
itakayofanyika Desemba 18, mwaka huu.
YANGA KUIVAA EXPRESS LEO SAA KUMI JIONI UWANJA WA TAIFA
Klabu ya soka ya Yanga, ya Jijini Dar es Salaam leo jioni itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya
Soka ya The Express Kutoka nchini Uganda, mchezo utakaochezwa majira ya saa 10
jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika dimba la Uwanja Taifa Jijini Dar es
salaam.
Yanga itapambana na The Express kama sehemu ya mchezo wa maandalizi ya
kujipima nguvu kuelekea pambano la mtani jembe siku ya jumamosi tarehe
13/12/20014 dhidi ya timu ya Simba SC jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa kesho kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo
anatarajiwa kukitumia kikosi chake chote kwa lengo la kutazama maendeleo ya
vijana wake kabla ya mchezo wa Nani Mtani Jembe wiki ijayo.
Mpaka sasa klabu ya Young Africans imefanya usajili wa mchezaji mmoja tu
Emerson De Oliveira kutoka nchini Brazil ambaye anachukua nafasi ya
mshambuliaji Geilson Santana "Jaja" ambaye ameomba kuachwa kutokana
na kushindwa kurejea nchini kwa masuala ya kifamilia.
Wananchama, mashabiki na wapenzi wa Yanga kutoka matawi mbalimbali
wanaombwa kuhudhuriwa kwa wingi uwanjani, ili kutoa hamasa ya ushindi kwa
wachezaji siku ya jumamosi katika uwanja mkuu wa taifa, jijini Dar es salaam.
Yanga inashiriki ligi kuu ya Tanzania bara ikiwa inashika nafasi ya pili
sawa na Azam FC kwa kulingana pointi na magoli ya kufunga na kufunga,
inajaindaa pia na mzunguko wa nane wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya
kimataifa kombe la Shirkisho baranai Afrika mapema mwakani.
Subscribe to:
Posts (Atom)