Saturday, May 18, 2013

JOSE MOURINHO ASEMA HUU ULIKUWA MSIMU WANGU MBAYA"".

KOCHA wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho ametanabaisha kuwa msimu huu kwamba ni mbaya zaidi kwake katika maisha yake ya soka baada ya kushuhudia kikosi cvhake kikitoka kapa kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye muda wa nyongeza dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme. Madrid tayari walishalitema taji la La Liga kwa mahasimu wao Barcelona na kuenguliwa na Borussia Dortmund katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hivyo Kombe la Mfalme ndio ilikuwa karata ya mwisho kwa Mourinho msimu huu kuondoka taji lakini nalo lilishindikana. Mourinho amesema kwa makocha wengine nafasi ya pili aliyopo katika ligi, na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na kucheza fainali ya Kombe la Mfalme ni mafanikio lakini kwake umekuwa msimu mbaya zaidi. Kocha huyo pia alikwepa swali kwamba msimu ujao ana mpango wa kutimkia klabu ya Chelsea akidai kuwa kwasasa anachojua bado ana mkataba na Madrid, na pia hajakaa chini na rais wa klabu hiyo kuzungumzia mstakabali wake wa huko mbele.

ATHLETICO MADRID YATWAA UBINGWA YAICHALAZA REAL MADRID 2-1.

CLUB ya  soka ya  Atletico Madrid usiku wa jana ilifanikiwa kuifunga Read Madrid kwa goli 2-1 na kuchukua kombe la Copa del Rey katika fainal iliyopigwa Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Uhispania.
Read Madrid ndio iliyokua ya kwanza kupata goli kupita kwa Ronaldo katika dakika ya 14 kabla ya kiungo Diego Costa kuisawazishia Atletico dakika ya 35 nakufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka dakika 90 zinamalizika.
Alikuwa ni beki wa kibrazil Miranda alipeleka kilio kwa kikosi cha Jose Mourinho mara baada ya kufunga goli la pili na la ushindi kwa timu yake katika dakika ya 99 mara kuwa zimeongezwa dakika 120.
Fainali hiyo ya jana iligubikwa na vitendo vibaya vilivyooneshwa na wachezaji kutoka timu zote mbili na muhamuzi kutoa jumla ya kadi za njano 13 na nyekundu 2 kwa timu zote mbili.
Nyota wa Real Madrid Ronaldo ye akipata kadi nyekundu katika dakika ya 114 huku akiwa na kadi ya njano kabla na Fernandez wa Atletico pia akipewa nyekundu dakika ya mwisho ya 120 baada ya awali kuwa na kadi ya njano.

FERGUSON BALE WATWAA TUZO YA MSIMU WA BPL LIGI KUU UINGEREZA.

Meneja wa Manchester United,Sir Alex Ferguson na Mchezaji wa Tottenham Gareth Bale jana walipewa tuzo za msimu wa ligi kuu ya Uingereza.
Ferguson ameshinda tuzo ya kocha bora wa msimu huku Bale akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu huu unaomalizika kesho na tayari Man United imetwaa ubingwa huo.
Hii inakuwa tuzo ya 11 kwa Ferguson na akiwa ameshinda makombe 38 na United huku 13 yakiwa ya ligi kuu ya Uingereza.Pia akiwa ametangaza kustaafu baada ya kuifundisha timu hiyo kwa miaka 26 na Jumapili hii atakua anakamilisha mechi yake ya 1,500 tangu aanze kuifundisha timu hiyo.
Bale akiwa amefunga magoli 19 msimu huu huku akiwa amecheza michezo 29 amekuwa mchezaji wa kwanza wa Tottenham na raia wa Wales kutwaa tuzo hiyo.
Hii ni tuzo ya nne kwa mchezaji huyo kutoka Wales baada ya kuchukua ile ya mchezaji bora wa PFA,Mchezaji bora chipukizi na Mchezaji bora wa Chama cha Waandishi wa habari za soka nchini Uingereza.
Tottenham watakuwa na kazi kubwa ya kumbakiza Gareth Bale katika klabu hiyo kutokana na kiwango bora alichoonesha msimu huu kwani timu nyingi zimeonyesha nia ya kutaka kumnyakua.

BRAZIL YAJA NA ROBOTI KATIKA KUHAKIKISHA ULINZI MICHEZONI.

SERIKALI ya nchini Brazil imesema baadhi ya roboti za kuimarisha usalama zilizonunuliwa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 zitakuwa tayari kutumika wakati wa Kombe Shirikisho itakayoanza kutimua vumbi Juni mwaka huu. Kampuni ya iRobot imesema roboti 30 zitawasilishwa kabla ya mwisho wa mwaka pamoja na vipuri na vifaa vingine vya kusaidia katika kuzitumia. Serikali ilithibitisha Alhamisi kuwa baadhi zitakuwa tayari kutumiwa katika miji sita itakayokuwa wenyeji wa mechi za Kombe la Shirikisho. Kampuni hiyo imesema serikali ya Brazil iliyotia saini mkataba wa $7.2 milioni, ambao unahusisha magari madogo yasiyokuwa na dereva ambayo yanaweza kutumiwa kupeleleza, kupekua na kuondoa mabomu pamoja na shughuli nyingine za kudumisha utawala wa sheria. Michuano ya Kombe la Shirikisho ni ya kwanza katika msururu wa hafla za ngazi ya juu za michezo zitakazoandaliwa na Brazil, ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia na Olimpiki 2016 jijini Rio de Janeiro.

PATA MAKALA KUHUSU CLUB YA MAN UNITED KATIKA HARAKATI ZA SOKA.

                                                        SEHEMU YA KWANZA. 
Manchester United ni klabu ya kandanda  ndani ya nchi ya Uingereza, ambacho ni mojawapo ya vilabu maarufu sana ulimwenguni makao  yake yapo Old Trafford eneo la Greater Manchester. Klabu hii ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa Ligi ya Primia mwaka 1992, na kimeshiriki mara nyingi katika soka la Uingereza tangu mwaka wa 1938, isipokuwa msimu wa 1974-75. Mahudhurio ya wastani  ya klabu  hii yamekuwa ya juu kuliko timu nyingine yoyote katika  soka la Uingereza kwa misimu yote isipokuwa sita tangu 1964-65.
Manchester United ndiyo bingwa wa sasa wa Uingireza na ndio wasshiriki wa Kombe la Dunia la Vilabu, baada ya kushinda Ligi ya Primia 2008-09 na Kombe la Dunia la FIFA. Klabu hicho ni miongoni mwa vilabu vyenye ufanisi mkubwa katika historia ya kandanda la Uingereza na kimeshinda mataji makubwa 22 tangu Alex Ferguson alipochukua wadhifa wa meneja wake mnamo Novemba 1986. Mwaka wa 1968 ilikuwa klabu cha kwanza kushinda Kombe la Uropa kwa kuifunga  Benfica 4-1. Walishinda kombe la pili la Ulaya kama sehemu ya ushindi wa mataji matatu mwaka 1999, na la tatu mwaka wa 2008, kabla ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka 2009. Kilabu hicho kinashikilia rekodi mbili ya kushinda mataji mengi ya Ligi ya Uingereza mara 18 na pia kushikilia rekodi kwa wingi wa kutwaa kombe la FA ikiwa imeshinda mara 11.
Tangu mwisho wa mwaka ya 1990, kilabu hicho kimekuwa mojawapo ya vilabu tajiri duniani kilicho na mapato ya juu kuliko kilabu chochote,na sasa kinatajwa kama kilabu chenye thamani zaidi katika mchezo wowote, na makisio ya thamana ya takriban bilioni £ 1.136 (bilioni € 1.319 ) Aprili 2009.Manchester United ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa kundi la vilabu la G-14 la Vilabu kuu vya kandanda Uingereza ambalo halipo tena, na European Club Association ,muungano uliochukua nafasi yake.
Alex Ferguson amekuwa meneja wa kilabu hicho tangu 6 Novemba 1986 alipojiunga na kilabu hicho kutoka Aberdeen baada ya kung'atuka kwa Ron Atkinson. Nahodha wa kilabu wa sasa ni Garry Neville, aliyechukua nafasi ya Roy Keane Novemba 2005.

Friday, May 17, 2013

IFAHAMU KWA UZURI MAN UNITED KATIKA HARAKATI ZA SOKA ULIMWENGUNI

MANCHESTER UNITED
MATAJI VIKOMBE ILIVYOTWAA:
UBINGWA:
LIGI KUU:VPL
1992–93, 1993–94, 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13
DARAJA LA 1:
1907–08, 1910–11, 1951–52, 1955–56, 1956–57, 1964–65, 1966–67
DARAJA LA 2:
1935–36, 1974–75
VIKOMBE:
FA CUP: 11
1908–09, 1947–48, 1962–63, 1976–77, 1982–83, 1984–85, 1989–90, 1993–94, 1995–96, 1998–99, 2003–04
LIGI CUP: 4
1991–92, 2005–06, 2008–09, 2009–10
FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 19
1908, 1911, 1952, 1956, 1957, 1965, 1967, 1977, 1983, 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011
ULAYA:
EUROPEAN CUP / UEFA CHAMPIONS LEAGUE: 3
1967–68, 1998–99, 2007–08
UEFA CUP WINNERS' CUP: 1
1990–91
EUROPEAN SUPER CUP: 1
1991
DUNIA:
INTERCONTINENTAL CUP: 1
1999
FIFA CLUB WORLD CUP: 1
2008
MATAJI YAKE: SIR FERGUSON-
-PREMIER LEAGUE: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999,
2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013.
-FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
-LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
-UEFA CHAMPIONS LEAGUE: 1999, 2008
-UEFA CUP WINNERS CUP: 1991
-FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
-UEFA SUPER CUP: 1992
-FIFA INTER-CONTINENTAL  CUP: 1999
-FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011

Endelea kupata taarifa zaidi kupitia mkali wa dimba tz.blogspot.com ambayo inakuletea makala kamili kuhusu Club hii bora kabisa duniani ya manchester united kaa mkao wa kuburudika kimichezo zaidi karibu wewe mdau wa blog hii>>>>>>>

KOMBE LA DUNIA: DROGBA , YAHAYA TOURE WAWEKWA PEMBEENI

KOCHA WA IVORY COAST Sabri Lamouchi, ametangaza Kikosi chake cha Wachezaji 26 kwa ajili ya Mechi za KUNDI C la kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka 2014 watakazocheza Mwezi ujao dhidi ya Gambia na Tanzania na hawamo Maveterani Didier Drogba na Kolo Toure.
Drogba, mwenye Miaka 35 ambae sasa anacheza huko Uturuki na Galatasaray, pia hakuchukuliwa kwenye Kikosi cha Ivory Coast kilichocheza Mechi ya KUNDI C ya Kombe la Dunia Mwezi Machi walipocheza na Gambia.
Hadi sasa Drogba ameichezea Nchi yake Mechi 96 na kufunga Bao 60.
MSIMAMO:
KUNDI C
1 Côte d'Ivoire Mechi 3 Pointi 7
2 Tanzania Mechi 3 Pointi 6
3 Morocco Mechi 3 Pointi 2
4 Gambia Mechi 3 Pointi 1
RATIBA/MATOKEO:
02/06/12: Ivory Coast 2-0 Tanzania; Gambia 1-1 Morocco
08-12/06/12: Morocco 2-2 Ivory Coast; Tanzania 2 Gambia 1
22-26/03/13: Ivory Coast 3 Gambia 0; Tanzania 3 Morocco 1
07-11/06/13: The Gambia v Ivory Coast; Morocco v Tanzania [Juni 8]
14-18/06/13: Tanzania v Ivory Coast; Morocco v The Gambia
06-10/09/13: Ivory Coast v Morocco; Gambia v Tanzania