Friday, May 17, 2013

KOMBE LA DUNIA: DROGBA , YAHAYA TOURE WAWEKWA PEMBEENI

KOCHA WA IVORY COAST Sabri Lamouchi, ametangaza Kikosi chake cha Wachezaji 26 kwa ajili ya Mechi za KUNDI C la kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka 2014 watakazocheza Mwezi ujao dhidi ya Gambia na Tanzania na hawamo Maveterani Didier Drogba na Kolo Toure.
Drogba, mwenye Miaka 35 ambae sasa anacheza huko Uturuki na Galatasaray, pia hakuchukuliwa kwenye Kikosi cha Ivory Coast kilichocheza Mechi ya KUNDI C ya Kombe la Dunia Mwezi Machi walipocheza na Gambia.
Hadi sasa Drogba ameichezea Nchi yake Mechi 96 na kufunga Bao 60.
MSIMAMO:
KUNDI C
1 Côte d'Ivoire Mechi 3 Pointi 7
2 Tanzania Mechi 3 Pointi 6
3 Morocco Mechi 3 Pointi 2
4 Gambia Mechi 3 Pointi 1
RATIBA/MATOKEO:
02/06/12: Ivory Coast 2-0 Tanzania; Gambia 1-1 Morocco
08-12/06/12: Morocco 2-2 Ivory Coast; Tanzania 2 Gambia 1
22-26/03/13: Ivory Coast 3 Gambia 0; Tanzania 3 Morocco 1
07-11/06/13: The Gambia v Ivory Coast; Morocco v Tanzania [Juni 8]
14-18/06/13: Tanzania v Ivory Coast; Morocco v The Gambia
06-10/09/13: Ivory Coast v Morocco; Gambia v Tanzania