SHARAPOVA AJIWEKA PEMBENI MICHUANO YA ITALIAN OPEN.
MWANARIADHA nyota wa kike wa
mchezo wa tenisi, Maria Sharapova amejitoa katika michuano ya wazi ya
Italia kabla ya mchezo wake wa robo fainali dhidi ya Sara Errani wa
Italia kutokana na matatizo ya kimwili. Sharapova
ambaye ni raia amejitoa mapema kwenye michuano hiyo ili aweze kupona
haraka kwa ajili ya kutetea taji lake la michuano ya wazi ya Ufaransa
baadae mwezi huu. Kwa
upande mwingine mwanadada anayesshika namba moja katika orodha za ubora
Serena Williams wa Marekani ameendeleza wimbi lake la ushindi baada ya
kumchakaza bila huruma Dominika Cibulkova wa Slovakia kwa 6-0 6-1 na
kutinga robo fainali ya michuano hiyo. Williams
ambaye ameshinda mechi 21 mfululizo sasa atachuana na Carla Suarez
Navarro wa Hispania kutafuta nafasi ya kutinga nusu fainali ya michuano
hiyo.