MESSI ASEMA TULICHEZA KWA WAKATI MGUMU BILA VILANOVA
MSHAMBULIAJI nyota Duniani wa
kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amekiri kuwa
ilikuwa ni ngumu kupambana na mazingira yaliyokuwepo wakati Tito
Vilanova alipolazimika kuondoka katikati ya msimu huu. Vilanova
aliondoka na kuliacha benchi la ufundi la klabu hiyo kwa zaidi ya miezi
mitatu baada kukutwa na saratani ya koo Desemba 2012 ambapo Muargentina
huyo anafurahia kwamba timu hiyo imeweza kunyakuwa taji pamoja na
kumkosa kiongozi wao. Messi
amesema amefurahi timu yake kunyakuwa taji hilo ingawa amekiri haikuwa
kazi rahisi kunywakuwa taji hilo haswa kipindi ambacho walimkosa
Vilanova aliyekwenda kwa matibabu kwani mabadiliko ya wazi yalionekana
katika kikosi chao. Nyota
huyo aliendelea kusema kuwa kutolewa kwao na Bayern Munich katika nusu
fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imekuwa ni changamoto kwao
kwani watajipanga na kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi. Amesema
kwasasa timu na makocha wengi wamefanikiwa kung’amua aina ya mchezo
wanaocheza hivyo kuwadhibiti lakini amedai kuwa haina maana timu hiyo
inapaswa kubadilisha aina mchezo wao wa pasi nyingi kwani ndio
unaowatambulisha duniani kote.