PEDRO ASEMA LAZIMA TUVUNJE REKODI YA REAL MADRIDI
WINGA Machachali wa klabu ya
Barcelona, Pedro Rodriguez amedai kuwa yeye na wachezaji wenzake wana
nia ya kufikia rekodi ya Real Madrid ya alama 100 baada ya kufanikiwa
kunyakuwa taji la La Liga mwishoni mwa wiki iliyopita. Barcelona
walikabidhiwa taji lao la 22 la ligi wakati mahasimu wao Madrid
waliposhindwa kuwafunga Espanyol na kutoa sare ya 1-1 na wako katika
nafasi nzuri ya kuvunja rekodi hiyo ya Madrid kama wakishinda mechi zao
zilizobakia. Mchezaji
huyo amesema kwasasa nguvu zao wanazielekeza katika kusaka alama 100
ingawa amekiri kuwa itakuwa kazi ngumu kutokana na timu watakazocheza
nazo. Nyota huyo
pia alisisitiza kuwa msimu huu umekuwa wa mafanikio kwao pamoja na
kuenguliwa na Bayern Munich katika nusu fainali ya michuano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya.