FA YAWEKA SHERIA KALI KATIKA SUALA ZIMA LA UBAGUZI
SHIRIKISHO la Soka la
Uingereza-FA linatarajia kutoa adhabu mpya ya mechi tano kwa mchezaji
atakayekutwa na hatia ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi mchezaji
mwenzake msimu ujao. Katika
kikao hicho cha mwaka cha FA kimedai katika taarifa yake kuwa kama
mtuhumiwa akirudia kosa moja kwa moja atapewa adhabu ya mechi 10 zaidi. Klabu
pia inaweza kutozwa faini ikiwa wachezaji wawili au zaidi watakutwa na
hatia ya kufanya vitendo hivyo katika kipindi cha miezi 12. Mwenyekiti
wa FA David Bernstein amesema wamefikia uamuzi huo kwasababu wanataka
kila mchezaji acheze soka akiwa salama na katika mazingira mazuri. Beki
wa Chelsea John Terry alifungiwa mechi nne na kutozwa faini ya paundi
220,000 kwa kumfanyia vitendo vya ubaguzi beki wa Queens Park Rangers
Anton Ferdinand Octoba mwaka 2011 wakati mshambuliaji wa Liverpool yeye
alifungiwa mechi nane na faini ya paundi 40,000 msimu uliopita kwa
kumbagua Patrice Evra wa Manchester United.