
Thursday, June 6, 2013
GALLIANI ASEMA HATUNA MPANDO NA KAKA KUJA MILAN.

ETO"O ATWAA MCHEZAJI BORA WA LIGI NCHINI URUSI.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi Samuel Eto’o ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa msimu wa 2012-2013. Eto’o ambaye amewahi kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora Afrika mara nne, alikabidhiwa tuzo hiyo baada ya kuisadia timu yake kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wan chi hiyo. Akihojiwa mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Eto’o ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo amedai kufurahishwa na hatua hiyo na kuwashukuru mashabiki wa soka nchini humo pamoja na waandishi wa habari kwa kuwa nyuma yake wakati wote. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 atakosa mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 wa timu ya taifa ya nchi yake dhidi ya Togo utakaochezwa Juni 9 mwaka huu kutokana na majeraha yanayomsumbua.
![]() Eto'o in 2011. | |||
Kuhusu yeye | |||
---|---|---|---|
Full name | Samuel Eto'o Fils | ||
Date of birth | 10 March 1981 (age 32) | ||
Place of birth | Douala, Cameroon[1] | ||
Height | 1.80 m (5 ft 11 in)[2] | ||
Playing position | Striker | ||
Timu | |||
Current club | Anzhi Makhachkala | ||
Number | 9 | ||
academy | |||
1992–1997 | Kadji Sports Academy | ||
Timu za ukubwa | |||
Years | Team | mechi | (Goli)" |
1997–2000 | Real Madrid | 3 | (0) |
1997–1998 | → Leganés (mkopo) | 30 | (4) |
1999 | → Espanyol (mkopo) | 0 | (0) |
2000 | → Mallorca (mkopo) | 19 | (6) |
2000–2004 | Mallorca | 120 | (48) |
2004–2009 | Barcelona | 145 | (108) |
2009–2011 | Internazionale | 67 | (33) |
2011– | Anzhi Makhachkala | 43 | (21) |
SPAIN BADO NAMBA MOJA UBORA DUNIANI - FIFA
Mabingwa wa Dunia timu ya taifa ya Spain bado ndio inaendelea kushika namba moja katika Listi ya viwango vya FIFA vya Ubora Duniani iliyotolewa leo ikifuatiwa na timu ya taifa ya ujerumani ambapo nafasi ya tatu inashikiliwa na Argentina ambapo nafasi ya nne ikishikiliwa na Croatia, huku Tanzania Taifa star ikipanda Nafasi 7 kutoka 116 hadi 109.
Katika 10 Bora, Netherlands imepanda mpaka Nafasi ya 5, Portugal kushuka Nafasi moja hadi ya 6, Colombia, wameshuka Nafasi 2 na wapo nafasi ya 7 huku timu ya taifa ya England ikiporomoka Nafasi 2 na sasa wako Nafasi ya 9.
Kwa Nchi za Afrika, Côte d'Ivoire ndio ipo Nafasi ya juu kabisa ikiwa Nafasi ya 13 ikifuatiwa na Ghana iliyokatika Nafasi ya 20.
Brazil, ambayo imeathirika kwa kucheza Mechi za Kirafiki tu kwa Miaka miwili, imeporomoka Nafasi 2 hadi Nafasi ya 22 lakini kushiriki kwao katika Mashindano rasmi ya FIFA ya kugombea Kombe la Mabara yatakayochezwa Nchini brazil kuanzia Juni 15 kama watafanya vizuri basi itawaletea faida nzuri na sana katika harakati za kupanda chati.
Toleo jingine la Listi ya FIFA ya Ubora Duniani litatolewa Julai 4.
25 BORA:
1 Spain
2 Germany
3 Argentina
4 Croatia
5 Netherlands
6 Portugal
7 Colombia
8 Italy
9 England
10 Ecuador
11 Russia
12 Belgium
13 Côte d'Ivoire
14 Switzerland
15 Bosnia-Herzegovina
16 Greece
17 Mexico
18 France
19 Uruguay
20 Denmark
21 Ghana
22 Brazil
23 Mali
24 Czech Republic
25 Chile
NCHI ZINAZOIZUNGUKA TANZANIA:
104 Qatar
105 Lithuania
106 Ethiopia
107 Niger
108 Saudi Arabia
109 Malawi
109 Tanzania {imepanda nafasi 7]
111 Kuwait
112 Tajikistan
113 Suriname
114 Korea DPR
115 Benin 308
116 Northern Ireland
JESUS AONGEZEWA MKATABA MPYA NDANI YA KLABU YA BENFICA.
KLABU ya Benfica ya Ureno imetangaza kumuongezea mkataba mpya kocha wake Jorge Jesus atakao dumu nao klubuni hapo mpaka katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2015. Kulikuwa na wasiwasi kama kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 anaweza kubakia katika klabu hiyo baada ya kumaliza msimu na kuambulia patupu. Hata hivyo Jesus sasa amemaliza utata huo kwa kusaini miaka miwili zaidi na klabu hiyo inayotoka katika jijini Lisbon. Jesus alianza kuinoa Benfica kuanzia mwaka 2009 na kuingoza kushinda taji moja la Ligi Kuu na matatu ya Kombe la Ligi la nchi hiyo.
PEREZ. AWEKA WAZI KUWA ZIDANE HANA UZOEFU WA KUTOSHA KUWA KOCHA.
Florentino Perez rais wa klabu ya Real Madrid ametanabaisha na kusema kuwa Zinedine Zidane ana vigezo vyote vinavyohitajika kuchukua nafasi ya Jose Mourinho lakini anadhani bado anahitaji uzoefu zaidi kabla ta kukabidhiwa mikoba hiyo. Perez amesema Zidane ana kila kitu ambacho kocha anatakiwa kuwa nacho na kazi hiyo anaiweza lakini bado anahitaji uzoefu ili kukabidhiwa majukumu makubwa kama hayo. Kwasasa chaguo la kwanza la Madrid katika kutafuta mbadala wa Mourinho ni kocha wa Paris Saint-Germain Carlo Ancelotti ingawa Perez alishindwa kuliongelea kwa kuogopa kuwachukiza PSG ambao bado wamemng’ang’ania kocha huyo. Zidane ambaye ameichezea Madrid kuanzia mwaka 2001 mpaka 2006 kwasasa ni mkurugenzi wa michezo na kocha wa vijana wa klabu hiyo.

WASIFU WA ZIDANE

Taarifa kuhusu yeye
| |||
---|---|---|---|
Full name
|
Zinedine Yazid Zidane
| ||
Date of birth
|
23 June 1972 (age 40)
| ||
Place of birth
|
Marseille, France
| ||
Height
|
1.85 m (6 ft 1 in)
| ||
Playing position
| |||
Timu za Ujana
| |||
1982–1983
|
US Saint-Henri
| ||
1983–1986
|
SO Septèmes-les-Vallons
| ||
1986–1989
| |||
Timu za Ukubwa
| |||
Mwaka
|
Timu
|
Mechi
|
Goli
|
1989–1992
|
61
|
(6)
| |
1992–1996
|
139
|
(28)
| |
1996–2001
|
151
|
(24)
| |
2001–2006
|
155
|
(37)
| |
Total
|
506
|
(95)
| |
Timu ya Taifa
| |||
1988–1989
|
4
|
(1)
| |
1989–1990
|
6
|
(0)
| |
1990–1994
|
20
|
(3)
| |
1994–2006
|
108
|
(31)
|
MARTINEZ ACHUA NAFASI YA DAVID MOYES KUIFUNDISHA EVERTON.
MENEJA wa zamani wa klabu ya Wigan Athletic, Roberto Martinez ameteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Everton akichukua mikoba ilioachwa wazi na David Moyes aliyekwenda Manchester United. Martinez mwenye umri wa miaka 39 alifanikiwa kutwaa taji la Kombe la FA msimu huu, lakini aliomba kuondoka baada ya kuihakikishia timu hiyo nafasi ya kubakia katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Mwenyekiti wa Wigan, Dave Whelan alimruhusu kocha huyo raia wa Hispania kuondoka na tayari wako katika mchakato wa kutafuta kocha mwingine wa kuziba pengo hilo. Martinez ambaye pia amewahi kuinoa Swansea City alijiunga na Wigan Juni mwaka 2009 na Aston Villa walitaka kumchukua mwaka 2011 lakini aliamua kubakia Wigan mpaka msimu huu alipoamua kuelekea Everton.
Tuesday, June 4, 2013
PEREZ AWEKA WAZI KUWA RONALDO ATABAKI REAL MADRID"
Florentino Perez rais wa club ya Real
Madrid ametanabaisha kuwa ana mategemeo kuwa mshambuliaji nyota wa klabu
hiyo Cristiano Ronaldo atabakia Santiago Bernabeu katika kipindi chote
cha maisha yake ya soka. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Ureno, mapema mwaka jana alidokeza kuwa hakuwa
anafurahia maisha ya Madrid na toka wakati huko amekuwa akihusishwa na
mpango wa kurejea Manchester United pamoja na Paris Saint-Germain-PSG. Lakini
Perez amedai kuwa atafanya kila awezalo ili nyota huyo aweze kuwa na
furaha katika klabu hiyo na kumalizika muda wake wa kucheza soka akiwa
hapo. Perez pia
aluzungumzia mustakabali ya mshambuliaji mwingine Gonzalo Higuain na
kudai kuwa hakuna yoyote aliyemwambia kwamba mchezaji huyo ataondoka
kwani klabu hiyo haijamuweka sokoni katika kipindi cha usajili. Ambapo
aliongeza kuwa kama mchezaji mwenyewe ndio anataka kuondoka basi klabu
itakayomhitaji itatakiwa kuwalipa lakini mpaka sasa ahkuna klabu yoyote
iliyojitokeza kumtaka mchezaji huyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)