Rais
wa Simba, Evans Aveva amemaliza utata wa usajili wa wachezaji wa kigeni
uliokuwa umeigubika klabu hiyo kwa kusema Mkenya Donald Mosoti ndiye anabaki na Mrundi Butoyi
Hussein wamempiga chini huku Yanga nao wakimpiga chini Emmanuel Okwi raia wa
Uganda.
Simba
na Yanga zimelazimika kufanya uamuzi mgumu wa kupunguza idadi ya wachezaji wa
kigeni ambao wamezidi katika klabu zao kwa sababu usajili wa wachezaji katika
klabu za Ligi Kuu Bara unamalizika leo saa 6 usiku.
Mrundi huyo alimvutia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia
Hans Poppe akiichezea Telecom ya Djibouti katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda mwezi huu.
Maana yake wachezaji wa kigeni katika kikosi cha Simba SC watakuwa mabeki
Mganda Joseph Owino, Mkenya Mosoti, Warundi kiungo Pierre Kwizera, mshambuliaji
Amisi Tambwe na Mkenya Mkenya Paul Kiongera.
Kwa
upande wa Yanga ambapo nayo ilikuwa na wachezaji sita wa kigeni ambapo awali
Hamis Kiiza ambaye ni raia wa Uganda
ndiye aliyekuwa anadaiwa kuachwa, lakini habari za ndani kutoka katika klabu ya
Yanga zinasema panga limemwangukia Emmanueli Okwi ambaye hadi jana asubuhi
alikuwa hajajiunga na timu.