Monday, September 15, 2014

MOURINHO ASEMA AMTUPIA LAWAMA CRISIANO RONALDO

KOCHA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amemtupia lawama Cristiano Ronaldo kwa kushindwa kwake kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati akiinoa Real Madrid. 
Mourinho alijiunga na na Madrid mwaka 2010 baada ya kuisaidia Inter Milan kunyakuw ataji hilo lakini katika msimu mitatu aliyokuwa Santiago bernabeu alishindwa kabisa kupata mafanikio barani Ulaya akiwa ameambulia kuingoza timu hiyo mpaka hatua ya nusu fainali katika kipindi chote hicho. 

Mara ya mwisho Mourinho kukaribia kutinga fainali ya michuano ya hiyo ilikuwa msimu wa mwaka 2011-2012 wakati walipokwenda katika hatua ya changamoto ya mikwaju ya penati baada ya muda wa nyongeza katika nusu fainali ya pili lakini walitolewa baada ya nyota wake akiwemo Ronaldo, Kaka na Sergio Ramos kukosa penati muhimu. 

Akihojiwa Mourinho ametamba kuwa kushinda taji la michuano hiyo mara mbili kama imefanya kazi yake hiyo kuwa ya kipekee. 

Mourinho amesema amekuwepo katika nusu fainali kadhaa na baadhi imekuwa ngumu kukubali kushindwa kama goli walilofungwa na Liverpool wakati akiwa na Chelsea mwaka 2005 pamoja matuta ya mwaka 2011 wakati mchezaji wao tegemeo Ronaldo alipokosa penati ya kwanza.

WEKUNDU WA MSIMBAZI WAREJEA ZANZIBAR KUWEKA KAMBI KWA MARA YA PILI.

Klub ya simba wekundu wa Msimbazi , Simba SC wamerejea tena Visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya ligi kuu soka  Tanzania bara inayotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu.
20140913_160508Simba chini ya kocha Mzambia Patrick Phiri wataanza kampeni za kusaka ubingwa walioukosa kwa misimu miwili dhidi ya Wagosi wa ya, Coastal Union, septemba 21 mwaka huu uwanja wa Taifa , Dar es salaam.
Hii itakuwa mara ya pili Simba kujificha Zanzibar kwa sabababu ilikuwa huko kabla ya kuja Dar es salaam kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, septemba 6 mwaka huu uwanja wa Taifa na kuitandika 3-0.
Ijumaa ya wiki iliyopita, Simba ilicheza mechi ya pili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya URA ya Uganda na kulala bao 1-0.
jumamosi ya wiki iliyopita, Simba ilisafiri kwenda Mtwara ambapo ilicheza mechi ya kirafiki na Ndanda fc katika uwanja wa Nangwanda Sijaona na kutoka suluhu pacha ya bila kufungana.
Baada ya mechi hiyo, jana wachezaji walipewa mapumzikio, na leo jumatatu wanaanza mazoezi kabla ya kuelekea Zanzibar.
Simba wamekuwa wakiijenga timu upya chini ya kocha Phiri na usajili wao unawafanya wapinzani wawe na wasiwasi.
Wachezaji wa kigeni waliopo Simba wameonekana kuwa na ubora wa kutosha, hivyo kujenga imani kwa mashabiki wao.
Warundi, Amissi Tambwe, Pierre Kwizera, Mkenya, Paul Kiongera na Waganda Joseph Owino na Emmanuel Okwi wameonekana kuwa na msaada mkubwa kwa Simba.
Pia wapo wazawa waliosajiliwa kama, kipa Hussein Sharrif, Shaaban Kisiga, Elius Maguli,Joram Mgeveke, Tshabalala, na wengineo.
Wachezaji hawa wameonakana kuelewana na kucheza mpira mzuri kama walivyoonekana kwenye mechi dhidi ya Gor Mahia na URA.

MINZIRO ASEMA TUNAWAKATI MGUMU LIGI KUU LAKINI TUTAPAMBANA TU" WACHEZAJI 7 NJE

Maafande wa Jkt Ruvu kutoka kibaha mkoani pwani kushuka kitaanza Ligi Kuu Bara bila ya wanandinga wake saba wa kikosi cha kwanza.
Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Felix Minziro, amethibitisha kutokuwepo kwa wachezaji hao ambao wamekwenda kushiriki michuano ya Majeshi ya Afrika Mashariki iliyokuwa ikifanyika mjini Zanzibar.
Wachezaji wangu takribani saba wa kikosi cha kwanza, hawapo kwa sasa, hili linanipa wakati mgumu sana.
Minziro amesema ligi inaanza siku ya Jumamosi, uwepo wao una mchango mkubwa katika timu na wako Msumbiji kwa sasa kulitumikia jeshi katika masuala la michezo.

KAMATI YA SHERIA YAPITISHA USAJILI KLAB ZA VPL NA FDL MSIMU 2014

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imepitisha usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza huku wenye kasoro ndogondogo klabu zao zikitakiwa kuziondoa ili waweze kupatia leseni za kucheza ligi msimu huu wa 2014/2015.
Kasoro hizo ni kufikia makubaliano na klabu ambazo wachezaji husika wametoka, kuwafanyia uhamisho (transfer) na kulipa ada za uhamisho. Kamati vilevile ilibaini wachezaji wengi hawakufanyiwa uhamisho kama kanuni za ligi hizo zinavyoelekeza.
Hivyo, klabu ambazo hazitakuwa zimeondoa kasoro hizo kwa wachezaji wao leseni zao zitazuiliwa mpaka watakapokuwa wamekamilisha kila kitu. Ni wachezaji wenye leseni tu ndiyo watakaoruhusiwa kucheza mechi za ligi.

Klabu za African Lyon, African Sports, Ashanti United, Coastal Union, Kiluvya United, Majimaji, Mji Mkuu, Polisi Dodoma, Polisi Morogoro, Red Coast na Stand United ziliwawekea pingamizi wachezaji mbalimbali kwa kutofanyiwa uhamisho.
Kuhusu Ike Bright Obina wa Nigeria aliyewekewa pingamizi na African Lyon dhidi ya Coastal Union, Kamati imezitaka klabu hizo kufikia makubaliano, na zikishindwa mchezaji huyo atabaki African Lyon.

Kamati vilevile ilijadili malalamiko ya Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic dhidi ya klabu hiyo, na kuzipa pande hizo mbili siku 14 kufikia muafaka juu ya malalamiko hayo, na zikishindwa ndipo zirejee tena mbele ya Kamati.
Logarusic aliyewakilishwa na mwanasheria wake Dickson Sanga anailalamikia klabu hiyo kwa kuvunja mkataba kinyume cha taratibu, hivyo kutaka Simba imlipe dola 6,000 kwa kuvunja mkataba, na pia kulipa dola 50,000 ikiwa ni fidia maalumu ya madhara yaliyotokana na uvunjwaji huo.
BONIFACE WAMBURA
KNY KATIBU MKUU
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Friday, September 12, 2014

MCHEZO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA MBEYA CITY VS VIPERS FC

Jumamosi hii kwenye uwanja wa Sokoine  kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Mbeya City Fc na Vipers FC (Zamani Bunamwaya Fc)ya Uganda . 

Mchezo huo unamepangwa kuanza saa       10:00. 

Vipers Fc inatarajiwa kuwasili Mbeya jioni ya leo ikitokea Entebbe kupitia  Dar Es Salaam ambapo Kiingilio kitakuwa Sh.3000
Hii ikiwa ni mabadiliko kutoka kiingilio  kilichotangazwa  awali cha sh.  5000

DISMAS  TEN
OFISA HABARI
MBEYA CITY COUNCIL FC.

Thursday, September 11, 2014

TAZAMA WASHINDI WA LIGI KUU TZ BARA TANGU MWAKA 1965-HADI LEO

Hawa ni washindi wa Ligi Kuu Tanzania Bara tangu mwaka 1965. Katika rekodi hii klabu ya Yanga imetwaa taji hilo mara 24, Simba mara 18 na mtibwa mara 2, nyingine zote zilizopoa hapa zimetwaa mara moja. Tarehe 20 ligi itaanza tena ya msimu wa 2014/15, Je Unadhani timu gani ipo katika nafasi ya kushinda taji hilo msimu huu?
Washindi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Tangu 1965 hadi leo
    1965 Sunderland (Sasa Simba SC)
    1966 Sunderland
    1967 Cosmopolitan
    1968 Yanga
    1969 Yanga
    1970 Yanga
    1971 Yanga
    1972 Yanga
    1973 Simba SC
    1974 Yanga
    1975 Mseto SC
    1976 Simba SC
    1977 Simba SC
    1978 Simba SC
    1979 Simba SC
    1980 Simba SC
    1981 Yanga
    1982 Pan Africans
    1983 Yanga
    1984 Simba SC
    1985 Yanga
    1986 Tukuyu Stars
    1987 Yanga
    1988 Coastal Union
    1989 Yanga
    1990 Simba SC
    1991 Yanga
    1992 Yanga
    1993 Yanga
    1994 Simba SC
    1995 Simba SC
    1996 Yanga
    1997 Yanga
    1998 Yanga
    1999 Mtibwa Sugar
    2000 Mtibwa Sugar
    2001 Simba SC
    2002 Yanga
    2003 Simba SC
    2004 Simba SC
    2005 Yanga
    2006 Yanga
    2007 Simba SC
    2007/08 Yanga
    2008/09 Yanga
    2009/2010 Simba SC
    2010/2011 Yanga
    2011/2012 Simba SC
    2012/2013 Yanga
    2013/2014 Azam FC
    2014/2015 ??.

WEKUNDU WA MSIMBAZI KUTIFUANA NA URA YA UGANDA

Simba Wekundu wa msimbazi SC kesho wanatarajia kushuka dimbani kuonyeshana kazi katika Mechi ya pili ya kimataifa ya kirafiki chini ya kocha Patrick Phiri dhidi ya timu ya mamlaka ya ukusanyaji wa mapato nchini Uganda, URA katika uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam katika mtanange utakao anza majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika mashariki.

Wakati huo huo jumamosi jioni, Simba itakuwa na mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Ndanda fc katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mk
oani Mtwara katika maadhimisho ya ‘Ndanda fc Day’.