MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imeendelea tena jana na kushuhudia timu za Barcelona, Bayern Munich, Paris Saint-Germain-PSG na FC Porto nazo zikitinga hatua ya timu 16 bora baada ya kushinda michezo yao. Katika michezo ya michuano hiyo iliyochezwa juzi mabingwa watetezi Real Madrid na Borussia Dortmund nao walitangulia katika hatua hiyo baada ya kushinda mechi zao. Barcelona wao walifanikiwa kusonga mbele baada ya kuitandika Ajax Amsterdam kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na nyota wake Lionel Messi wakati Bayern Munich wao waliichapa kwa mara nyingine AS Roma kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Allianz Arena. PSG wao walisonga mbele baada ya kuitandika Apoel kwa bao 1-0 huku Porto nao wakicharuka na kuichapa Athletic Bilbao kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na nyota wa Colombia Jackson Martinez na Mualgeria Yacine Brahimi.
Wiki hii imekuwa mbaya kwa timu za Uingereza kwani baada ya Liverpool kuiweka rehani nafasi yao ya kusonga mbele kwa kufungwa na Madrid kwa bao 1-0 huku Arsenal wakitoa sare nyumbani na Anderlecht, Chelsea nao wameingia katika mkumbo huo baada ya kugawana alama na Maribor kwa kutoka sare ya bao 1-1. Kwa upande wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu hali yao ndio imezidi kuwa mbaya baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi katika Uwanja wa Etihad na kuweka matumaini yao ya kusonga mbele katika mashaka.
Thursday, November 6, 2014
MESSI AFIKIA REKODI YA RAUL BAO 71 AMBWAGA RONALDO UEFA
Mshambuliaji Mahiri wa Argetina na Barcelona Lionel Messi amefanikiwa kuifikia rekodi ya nyota wa zamani wa Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Raul Gonzalenz alikuwa akishikilia rekodi ya kufunga mabao 71 na kuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Cristiano Ronaldo alionekana ndiye atakuwa wa kwanza kumfikia Raul,lakini mabao mawili aliyofunga Messi wakati Barcelona ikiichalaza Ajax magoli 2-0 kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, yamekwamisha ndoto za Ronaldo.
Wafungaji Bora: wa Kihistoria Uefa.
Lionel Messi: Magoli 71 Mechi 90-Barcelona.
Raul: Magoli 71 Mechi 142-Real Madrid na Shalke 04.
C'Ronaldo: Magoli 70 Mechi 107-Man united na R'Madrid
Ruud van Nistelrooy: Magoli 56 Mechi 73-Psv Eindhoven,Man U na R'Madrid.
Thierry Henry: Magoli 50 Mechi 112-Arsenal,Barca,Los angel marekani.
JESHI LA POLISI MBEYA LAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUUZA NYAMA YA MBWA
KATIKA tukio la kushangaza mwanaume mmoja amekamatwa na polisi wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kuuza nyama ya Mbwa.
Mtuhumiwa huyo amefahamika kwa jina la Ahad Jesikaka mwenye umri wa miaka 20, mkazi wa kijiji cha Ngyekye, kata ya Matema, wilayani humo.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amesema kuwa amewauzia kitoweo hicho watu wawili.
Amewataja walionunua nyama hiyo ni Enock Nsemwa mwenye miaka 25, na Anyandile Mbwilo mwenye umri wa miaka 29, wote wakazi wa Ngyekye.
Hata hivyo anatoa wito kwa jamii kuwa makini hususuni wanaponunua vyakula ili kujiepusha na madhara ya kiafya.
MWANAFUNZI WA DARASA LA 5 AFARIKI KWA VIBOKO NCHINI KENYA
Mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya msingi ya Kiuu Kenya amefariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu wake kwa kufeli somo lake la Kiswahili.

Mama wa mwanafunzi huyo Grace Muthoni amesema mtoto wake alienda shule Jumatatu asubuhi na aliporudi alianza kulalamika maumivu ya kichwa na shingo, siku iliyofuatia alimpeleka Zahanati ya Wilaya ya Nyagiti level 4.
Siku ya pili alilazimika kumrudisha Hospitali baada hali yake kuzidi kuwa mbaya daktari akashauri ahamishiwe katika Zahanati ya Muran’ga Level 4 kwa matibabu zaidi wakati akisubiri gari la wagonjwa akafariki dunia.
Mama huyo amesema uchunguzi wa awali unaonyesha mtoto wake alipigwa na Mwalimu na kupata majeraha kichwani na shingoni, mwili wake umehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi kubaini sababu za kifo chake.
Mwalimu anayedaiwa kumpiga Mwanafunzi huyo alikimbia kujificha shimoni baada ya kusikia taarifa za kifo, huku Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Joseph Mwenda akikanusha uvumi kwamba mtoto huyo alifia shuleni.
Wednesday, November 5, 2014
REAL MADRID,DORTMUND ZATINGA HATUA YA 16 BORA UEFA
Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uefa hatua ya makundi iliendelea tena jana huku tukishuhudia klabu mbili za Borussia Dortmund na Real Madrid zikifanikiwa kutinga hatua inayofuata ya timu 16 bora. Dortmund wanaonolewa na Jurgen Klopp pamoja na kusuasua katika Bundesliga lakini katika michuano hiyo wamekuwa wakionyesha kiwango kizuri baada ya kuigaragaza Galatasaray kwa mabao 4-1 hivyo kuwa wameshinda mechi zao zote nne katika kundi D.
Madrid wao wametinga hatua hiyo baada ya kuikabili Liverpool na kuitandika bao 1-0 katika Uwanja wa Santiago Bernabeu na kufikisha alama 12 katika kundi B mbele ya FC Basel waliopo nafasi ya pili ambao nao waliichapa Ludogorets Razgrad kwa mabao 4-0.
Kwa upande mwingine ushindi wa mabao 2-0 waliopata Atletico Madrid dhidi ya Malmo umewapaisha mpaka kileleni mwa kundi A huku Olympiakos wakiwa nafasi ya pili pamoja na kutandikwa na Juventus kwa mabao 3-2. Kundi C Bayer Leverkusen wamejiimarisha kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya Zenit Saint Petersburg, Benfica wao walifufua matumaini yao ya kusonga mbele baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Monaco. Arsenal wao wameendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Dortmund baada ya kushindwa kulinda ushindi wake na kujikuta wakitoa sare ya mabao 3-3 na Anderletch katika Uwanja wa Emirates.
Madrid wao wametinga hatua hiyo baada ya kuikabili Liverpool na kuitandika bao 1-0 katika Uwanja wa Santiago Bernabeu na kufikisha alama 12 katika kundi B mbele ya FC Basel waliopo nafasi ya pili ambao nao waliichapa Ludogorets Razgrad kwa mabao 4-0.

BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA NEKTA LATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA 7 UFAULU WAONGEZEKA.
BARAZA la mitihani la taifa Nekta, limetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba mwaka huu, ambapo kiwango cha ufaulu kimeongezeka kutoka asilimia 50 nukta sita moja ya mwaka jana hadi kufikia asilimia 56, nukta tisa, tisa mwaka huu.

Watahiniwa waliofanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka huu walikuwa ni zaidi ya laki saba na 92, elfu sawa na asilimia 98, ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mitihani hiyo.
WAZIRI NYALANDU ASEMA VITENDO VYA UJANGILI VISIPODHIBITIWA TAIFA LITAANGAMIA.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema vitendo vya ujangili dhidi ya wanyama wakiwamo tembo, mbali na kuonekana kupungua nchini, lakini kasi yake isipodhibitiwa, taifa litaangamia.
Waziri Nyalandu ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kitaifa uliowashirikisha viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na wadau wa maendeleo kuhusu kujadili namna ya kudhibiti uharibifu dhidi ya rasilimali za nchi zikiwamo wanyama na misitu, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Waziri Nyalandu,amesema kukithiri kwa vitendo hivyo kunachangiwa na madai ya kuongezeka kwa soko haramu la rasilimali za nchi zikiwamo nyara za serikali katika nchi za Vietnam, Japan, Korea, China na Thailand.
Waziri Nyalandu ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kitaifa uliowashirikisha viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na wadau wa maendeleo kuhusu kujadili namna ya kudhibiti uharibifu dhidi ya rasilimali za nchi zikiwamo wanyama na misitu, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Waziri Nyalandu,amesema kukithiri kwa vitendo hivyo kunachangiwa na madai ya kuongezeka kwa soko haramu la rasilimali za nchi zikiwamo nyara za serikali katika nchi za Vietnam, Japan, Korea, China na Thailand.
Hata hivyo Nyalandu amewataka watu wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria zikiwamo silaha aina ya gobore, kuzisalimisha haraka kwa hiari, vinginevyo watakumbwa na operesheni ya nyumba kwa nyumba na kuwalazimu wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Subscribe to:
Posts (Atom)