Thursday, May 29, 2014

FABIANSKI AKUBALI KUTUA SWANSEA CITY

GOLIKIPA wa Arsenal, Lukasz Fabianski amekubali kujiunga na Swansea City wakati mkataba wake na klabu hiyo utakapomalizika mwezi ujao. Golikipa huyo wa kimataifa wa Poland alikataa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ili kumzuia asiondoke na sasa ameamua kuhamia katika Uwanja wa Liberty unatumiwa na Swansea. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao, Arsenal walithibitisha kuondoka kwake na kumshukuru golikipa huyo kwa mchango wake aliotoa katika kipindi ch
ote alichokuwepo na kumtakia kila la kheri huko anapokwenda. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Arsenal akitokea Legia Warsaw mwaka 2007 na kucheza mechi 78 katika kikosi cha kwanza katika mashidano toka alipojiunga nao.

ARSENAL MORATA KINDA MSHAMBULIAJI WA MADRID MWENYE UMRI WA MIAKA 21.

MAOFISA wa klabu ya Arsenal, wamesafiri kwenda Hispania kwa matumaini ya kumamilisha dili kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata. Mshambuliaji huyo amekuwa akiwindwa na Arsene Wenger kwa muda mrefu na klabu imeamua kuanza harakati za kumsajili nyota huyo mwenye miaka 21 mapema, kwani Juventus nao pia wanamuwinda.
Madrid wako tayari kumuuza lakini wanatarajiwa kusisitiza kutaka dau lao walilomnunulia kitu ambacho kinaonekana kitakuwa kigingi kikubwa kwa timu zinazomuhitaji. Arsenal walijaribu kumsajili kinda huyo wa kimataifa wa Hispania majra ya kiangazi mwaka jana na safari hii wanaamini uhakika wa kupata namba katika kikosi cha kwanza atakaoupata utawasaidia kumvutia kwao. Morata amefunga mabao tisa katika mechi 28 alizocheza akiwa na Madrid msimu huu na alitokea benchi katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika Jumamosi na kuisadia timu yake kuisambaratisha Atletico Madrid. Arsenal pia wanamtaka mshambuliaji mwingine wa Madrid Karim Benzema lakini Carlo Ancelotti anamtaka nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kusaini mkataba mpya na timu hiyo.

CECAFA NILE BASIN CUP MBEYA CITY ROBO FAINALI KUUMANA NA WAKALI KUTOKA UGANDA

Timu ya Soka ya Mbeya city katika hatua ya Robo fainali itashuka dimbani kuonyeshana kazi na wababe kutoka Uganda, Victory University katika Robo Fainali ya michuano ya Nile Basin Jumamosi ya Mei 31, Uwanja wa Khartoum Sudan.
Hiyo itakuwa robo Fainali ya kwanza siku hiyo itakayoanza Saa 11:30 jioni na kufuatia na mchezo mwingine kati ya wenyeji El Ahli Shandi dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini.
Awali, kesho zitachezwa Robo Fainali mbili za kwanza kati ya AFC Leopards ya Kenya na Defence  ya Ethiopia Saa 11:30 kabla ya wenyeji El Merreikh kuumana na Academie Tchite ya Burundi.
Mbeya City ilitinga Robo Fainali za michuano ya Nile Basin inayoendelea nchini Sudan kufuatia sare ya bila kufungana na Enticelles ya Rwanda usiku wa jana Uwanja wa Khartoum.
Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City imaliz
e na pointi nne baada ya mechi tatu, ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya AFC Leopards ya Kenya walioongoza kundi kwa pointi zao tisa.
Enticelles imemaliza nafasi ya pil
i kwa pointi zake mbili na Academie Tchite ya Burudi imemaliza mkiani mwa Kundi B kwa pointi moja iliyovuna kwenye sare na timu ya Rwanda.
Michuano hii inayoshirikisha mabingwa wa Kombe la FA au washindi wa pili wa Ligi Kuu za nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), inafanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu, Sudan wakiwa wenyeji wa kwanza.
CECAFA imeanzisha mashindano hayo kwa lengo la kuongeza changamoto kwa klabu za ukanda wake. 
MSIMAMO WA:
KUNDI ‘A’

P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts.
Al-Merreikh
3
2
1
0
7
2
+5
7
Victoria University
3
2
1
0
4
0
+4
7
Malakia
3
1
0
2
5
5
0
3
Police
3
0
0
3
0
9
-9
0
KUNDI ‘B’

P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts.
AFC Leopards
3
3
0
0
5
1
+4
9
Mbeya City
3
1
1
1
4
4
0
4
AcademieTchite
3
1
1
2
3
4
-1
3
Entincelles
3
0
0
2
0
3
-3
1
KUNDI ‘C’

P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts.
Al-Shandy
2
2
0
0
4
1
+3
6
Defence
2
1
1
0
2
3
-1
3
Dkhill
2
0
0
2
2
4
-2
0
ROBO FAINALI
TAREHE
M/No.
MECHI
MAHALA
SAA
30/05/14
16
AFC Leopards Vs Defence
MERREIKH
6:30pm

17
Al-MerreikhVs AcademieTchite
MERREIKH
8:30pm





31/05/14
18
Victoria University Vs Mbeya City
MERREIKH
5:30pm

19
Ahly Shandi Vs Malakia
MERREIKH
8:00pm





NUSU FAINALI
Jumatano Juni 2
[20]. Mshindi 16 Vs Mshindi 17
[21]. Mshindi 18 Vs Mshindi 19
Jumatano Juni 4
Mshindi wa Tatu
22]. Aliefungwa 20 Vs Aliefungwa 21
FAINALI[
23] Mshindi 20 Vs Mshindi 21

MKUTANO MKUU WA UONGOZI WA YANGA NA WANACHAMA NI JUMAPILI


Baraka Kizuguto - Afisa Habari Young Africans SC
Mkutano Mkuu wa Wanachama wa mabadiliko ya baadhi ya Vipengele kwenye Katiba utafanyika siku ya jumapili Juni Mosi 2014 katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi - Oysterbay kuanzia majira ya saa 3 kamili asubuhi huku wanachama wote hai wa klabu ya Young Africans wakiombwa kujitokeza kwa wingi.
Akiongea na waandshi wa habari makao makuu ya klabu, Afisa Habari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto amesema mkutano huo wa siku ya jumapili ni kwa ajili ya marekebisho ya katiba kama maagizo ya Shirikisho la Soka nchini TFF ilivyoagiza.
"Jumapili tunafanya makutano wa marekebisho ya katiba lengo ni kuhakikisha wanachama wanapata nafasi ya kutoa maoni yao na kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea Yanga kupeleka katiba yake TFF na kisha kwa msajili ili shughuli zote za klabu ziweze kufanyika kwa kufuata katiba mpya" alisema Kizuguto.
Mara baada ya mabadiliko hayo nadhani tutakua tayari kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi kwani tulikuwa tunasubiria marekebisho ya Katiba tu, TFF na msajili wakishaiptisha Katiba basi tutakua tayari kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi.
Watakoruhusiwa kuhudhuria mkutano mkuu siku ya jumapili ni wanachama wa Yanga SC walio hai tu, kwa maana ambao wamelipia ada zao za uanachama mpaka kufikia kwa mwezi ujao wa Juni 2014.
Wanachama ambao bado hawajalipia Ada zao za uanchama wanaombwa kulipia mapema kabla ya siku ya mkutano, malipo yote yanafayika kwenye Idara ya Fedha makao makuu ya klabu kila siku muda wa kazi na siku ya jumamosi saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana.

SAMATTA NA ULIMWENGU WAPATA KIBALI KWA TP MAZEMBE


Klabu ya TP Mazembe hatimaye imewaruhusu wachezaji wake Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kujiunga na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo tayari imewasili Harare, Zimbabwe kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika.

Taifa Stars itacheza na Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ katika mechi ya marudiano raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.  
Mechi hiyo itachezwa Jumapili (Juni 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Harare.Samatta na Ulimwengu watawasili Harare kesho Saa 3.40 usiku kwa ndege ya Kenya Airways na watajiunga na TP Mazembe mara baada ya mchezo huo ambapo Juni 2 mwaka huu, wakienda moja kwa moja Ndola, Zambia ambapo timu yao imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek Juni 7.