Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) chini ya Rais wake, Jamal Malinzi, limeomba kuadaa mashindano ya Kombe la
Taifa Africa (Afcon).
TFF imechukau uamuzi huo baada ya Caf kuifuta Libya iliyopanga kuandaa michuano hiyo mwaka 2017 kutokana na vurugu.
TFF imesema inaamini kuna miundombinu ya kutosha kuandaa michuano hiyo na tayari barua imetumwa Caf.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine amesema barua ya maombi kwenda imeshatumwa.