Timu ya Tanzania Taifa Stars inataraji kwenda
Morocco kukipiga na wenyeji wake katika mechi ya kirafiki ndani ya tarehe za
Fifa.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Celestine amesema wamepokea mwaliko na tayari Kocha Mart Nooij ameishatangaza kikosi chake.
Mwesingwa amesema Septemba 5 ni tarehe ambayo
iko ndani ya tarehe za Fifa, hivyo maandalizi yanaanza na kocha ameishaita
kikosi.
Stars katika mechi yake ya mwisho, Stars ilichapwa
kwa mabao 2-1 ikiwa ugenini nchini Msumbuji na kutolewa katika mbio za kuwania
kucheza michuano ya Mataifa Afrika.