Monday, August 25, 2014

KUFUATIA KIFO CHA MCHEZAJI ALGERIA YASIMAMISHA LIGI

SHIRIKISHO la Soka nchini Algeria limesimamisha Ligi Kuu kufuatia kifo cha mchezaji wa Cameroon Albert Ebosse ambaye alipigwa na jiwe lililorushwa na mashabiki. Uamuzi huo umefikiwa jana katika kikao kilichofanyika jana. Ebosse mwenye umri wa miaka 24 alipigwa na jiwe kichwani wakati akitoka uwanjani baada ya timu yake ya JS Kabylie kufungwa na USM Alger huko Tizi Ouzou juzi. Tayari mamlaka inayohusika imeshaufungia Uwanja wa 1st Novemba 1954 kulikotokea tukio hilo. Shirikisho hilo pia limeamua kutoa ubani wa dola 100,000 kwa familia ya Ebosse kiwango ambacho kinaaminika angeweza kukipata katika kipindi cha mkataba wake huku wachezaji wa Kabylie nao wakitoa mishahara yao ya mwezi kama rambirambi ya kufariki kwa mwenzao. Imegundulika kuwa uwanja wa 1st Novemba 1954 ulikuwa katika matengenezo wakati wa mchezo huo na mashabiki walitumiwe mawe ya ujenzi yaliyokuwa yamewekwa maeneo hayo.

Albert Ebossé Bodjongo
Taarifa binafsi
Full nameAlbert Dominique Ebossé Bodjongo Dika
Date of birth6 October 1989
Place of birthDoualaCameroon
Date of death23 August 2014 (aged 24)
Place of deathTizi OuzouAlgeria
Height1.85 m (6 ft 1 in)
Playing positionForward
Timu ya ukubwani
YearsTeamMechiGoli
2008–2010Coton Sport FC
2010–2011Unisport Bafang
2011–2012Douala AC10(9)
2012–2013Perak FA16(11)
2013–2014JS Kabylie32(19)
Timu ya taifa
2009Cameroon U20