Wednesday, November 19, 2014

KIMBE ASEMA DEUS KASEKE BADO NI MALI YA MBEYA CITY

Uongozi wa Mbeya City umesema kuwa bado inatambua kuwa Deus Kaseke ni mwanandinga wao na kukanusha uvumi wa kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kujiunga na Simba ama Yanga kupitia dirisha dogo lililoanza kufunguliwa mnamo Nov 15/2014.
Kiungo huyo mshambuliaji wa kikosi hicho cha Mbeya City, hivi karibuni jina lake limeoneka kuchukuwa nafasi katika vyombo vya habari ikionyesha kwamba mchezaji huyo anakwenda Msimbazi Simba sanjari na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Ame Ali ambapo mpaka sasa mtibwa imekanusha kupitia afisa habari wake Tobias kifaru akisema hawana mpango wakuuza mchezaji lakini kama kunatimu inataka mcheza ifike katika mashamba ya miwa.
Aidha taarifa hizo zimekuwa zikidai kuwa mchezaji huyo huenda akamwaga wino katika klabu ya Yanga kwa ajili ya kukipiga katika duru la pili .
Akiweka bayana kupitia Kapu la habari .blogspot.com Katibu mkuu wa klabu ya Mbeya ciity Emmanuel Kimb amesema mpaka sasa uongozi huo haujapata  ofa yoyote kutoka kwenye vilabu hivyo.
Amesema,  hivyo mchezaji Deus Kaseke anaendelea kuwa mchezaji halali wa klabu ya Mbeya City lakini Kimbe, hakuwa tayari kuweka wazi mkataba walioingia na mchezaji huyo.
Katibu huyo ameweka wazi kuwa Mpaka sasa bado klabu  hiyo inauhalali wa kuendelea kumtumia mchezaji Deus Kaseke kwani mkataba wake haujamalizika na pia uongozi haujapokea ofa yoyote kutoka klabu za Yanga na Simba.
Sanjari na hayo Timu ya mbeya city inatarajia kuingia kambini mwishoni mwa mwezi huu kujiweka sawa michezo inayofuata ya ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara itakayo Endelea Dec 26/2014.
Timu hiyo ambayo itafungua dimba na timu ya Ndanda kutoka Mkoani Mtwara, mchezo unaotaraji kupigwa kwenye dimba la kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine Jijini Mbeya kwa sasa mbeya city ipo nafasi ya mwisho ya 14 ikiwa na point 5 katika Msimamo ya ligi hiyo kwa Mechi Saba zilizochezwa.
Tazama Matokeo ya Mbeya  city:
    Mechi                                  Dimba
1. Mbeya City 0-0  Jkt Ruvu  Sokoine
2. Mbeya City1-0  Coastal     Sokoine
3. R'Shooting 0-0   Mbeya     Mabatini
4. Mbeya City0-1  Azam       Sokoine
5. Mbeya City 0-2  Mtibwa   Sokoine
6. Mgambo Jkt 2-1 Mbeya    Mkwakwani
7. Stand United1-0  Mbeya    Kambarage