
Msako huo katika msikiti wa Swafaa
mtaani Kisauni unakuja baada ya msako mwingine wa Jumatatu ambapo polisi
pia walipata silaha gutu ndani ya msikiti ambao wanasema hutumika kutoa
mafunzo yenye itikadi kali.
Mtaa wa Kisauni ndiko vijana
waliokuwa wamejihamu kuwadunga visu watu wanne na kuwaua. Pia
waliwashambulia kwa silaha nyingine gutu.
Waziri wa usalama wa
ndani, Joseph Ole Lenku anasema kuwa msako huo ulifanywa katika misikiti
ambayo hutumiwa na watu wanaoeneza itikadi kali za kiisilamu kwa vijana
ambao inadaiwa wanajiunga na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al
Shabaab nchini Somalia.
Viongozi wa kiisilamu wamelanaani misako
hiyo katika msikiti wakisema kuwa itachochea zaidi vijana kuendeleza
itikadi kali za kidini.