Wednesday, November 19, 2014

MWOMBEKI ATUA RUVU SHOOTING DIRISA DOGO LA USAJILI

Maafande wa Ruvu shootingi wa kibaha Mkoani Pwani imefanikiwa kumnasa aliyekuwa Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Betram Mwombeki  na kumpatia kitanzi cha  mkataba wa mwaka mmoja.
Straika huyo msimu uliopita alikuwa akiitumikia Simba akitokea Pamba na aliweza kufanya vyema katika mzunguko wa kwanza lakini wa pili hakuweza kupata nafasi ya uhakika, hivyo akaumaliza msimu akiwa na mabao manne tu.

Akizumgumza na mkali wa dimba Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amethibitisha hilo huku akidai kuwa wakati ukifika ataweka hadharani huku akihitaji siku muda ili kulitanabaisha hadharani.
Baada ya kuondoka Simba, Mwombeki alikwenda Oman na kufanya majaribio katika kikosi cha Oman Club FC linachoshiriki daraja la kwanza. Lakini mambo yalikwenda kombo.