Mabingwa wa ligi kuu Msimu uliopita Azam fc Azam FC imekubali kumuuza
mshambulizi wake bora zaidi, Muivory Coast, Kipre Tchetche kwa timu ya
Kelntan FC ya nchini Malasyia ambapo nafasi yake ikitarajiwa kuzibwa na mshambulizi wa mali, Mohammed Traore.
Tunaweza kusema toa kifaa pata kifaa wakati mwingine huzaa
majibu mabaya kutokana na uwezo wa mtu alieondoka hatari sana i nahitaji maamuzi kumtoa mtu kama kipre.
Hivyo kitendo cha kumuuza, Kipre mwenye kasi na kumsaini mchezaji anayetegemea
kutengenezewa mipira tu kinaweza kuifanya timu hiyo kupooza kabisa katika
safu ya ushambulizi.
Didier Kavumbagu, John Bocco, Gaudensi Mwaikimba, Leonel Saint wote
hawa ni washambuliaji ambao hawana kasi sana uwanjani tofauti na Kipre alikuwa na uwezo binafsi
katika uchezaji wake, alikuwa akishambulia vizuri kutokea pembeni ya
uwanja na alikuwa hatari kutokana na kasi yake.
Benchi la ugfundi la
timu hiyo linakabiliwa na changamoto kubwa, lakini watalazimika kukubali
changamoto kuishi bila msaada wa mabao ya Kipre’ mchezaji
ambaye alijiunga na Azam FC miaka minne iliyopita na kushinda tuzo ya
ufungaji bora msimu wa 2012/14 huku akishinda tuzo ya mchezaji bora wa
msimu uliopita.