Thursday, May 9, 2013

BPL KAZI IPO 4 BORA NANI KUTINGA KUCHEZA UEFA CHAMPIONZ LIGI

Katika mechi iliyopigwa Uwanjani Stamford Bridge kati ya Chelsea na Tottenham Usiku  leo jumatano usiku chelsea imeweza kulazimiswa sare ya kufungana bao 2-2 katika mtange uliokuwa na upinzania wa hali ya juu kawa kila timu.
Hivyo sare imeleta ugumu zaidi  kwa Timu hizo pamoja na Arsenal katika harakati ya kutafuta Timu 2 zitakazoungana na Mabingwa Manchester United na Man City kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI 
Msimu ujao.


MATOKEO WAFUNGAJI
MAGOLI:
Chelsea 2
-Oscar Dakika ya 10
-Ramires 39
Tottenham 2
-Adebayor Dakika ya 26
-Sigurdsson 80
MSIMAMO-Timu 7 za juu:
KUMBUKA: MANCHESTER UNITED TAYARI BINGWA 
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Man Utd
36
42
85
2
Man City
36
31
75
3
Chelsea
36
34
69
4
Arsenal
36
31
67
5
Tottenham
36
18
66
6
Everton
36
14
60
7
Liverpool
36
25
55
TIMU 4 ZA JUU  HUINGIA KUCHEZA UEFA CHAMPIONZ LIGI NA YA 5 KUINGIA EUROPA LIGI
Ratiba Mechi muhimu:
*11 Mei - Aston Villa v Chelsea
*12 Mei - Stoke v Tottenham
*14 Mei - Arsenal v Wigan
*19 Mei - Chelsea v Everton
*Newcastle vArsenal
Tottenham v Sunderland
RATIBA YA BPL
Jumamosi Mei 11
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Aston Villa v Chelsea
Jumapili Mei 12
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Stoke v Tottenham
[Saa 11 Jioni]
Everton v West Ham
Fulham v Liverpool
Norwich v West Brom
QPR v Newcastle
Sunderland v Southampton
[Saa 12 Jioni]
Man United v Swansea
Jumanne Mei 14
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Wigan
[Saa 4 Usiku]
Reading v Man City
WEKUNDU WA MSIMBAZI WATWANGA JTK MGAMBO 1-0 U/TAIFA

KATIKA mechi ya VPL iliyopigwa leo katika dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es saalam
kati ya simba na Jkt Mgambo Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0
lililifungwa naHaruna Chanongo  katika Dakika ya 8 na kuipa ushindi.

wekundu hao wa msimbazia wamebakisha Mechi moja na Mahasimu wao Mabingwa Yanga 
hapo Mei 18 ikimbuke katika duru ya kwanza simba na yanga zilitoka sare ya kufungana bao 1-1
lakini kazi ipo ya kulipiza kipigo cha bao 5-0 za mwaka wa jana.
RATIBA:
Jumamosi Mei 11
Azam FC Vs Mgambo JKT
Kagera Sugar Vs Ruvu Shooting
Jumamosi Mei 18
Toto Africans Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs African Lyon
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
TZ Prisons Vs Kagera Sugar
Simba SC Vs Yanga SC
JKT Oljoro Vs Azam FC
Polisi Moro Vs Coastal Union
MSIMAMO:
KUMBUKA YANGA BINGWA
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
YANGA
25
17
6
2
45
14
31
57
2
AZAM FC
24
14
6
4
42
20
22
48
3
SIMBA SC
25
12
9
4
38
23
15
45
4
KAGERA SUGAR
24
11
7
6
25
18
7
40
5
MTIBWA SUGAR
25
10
9
6
29
24
5
39
6
COASTAL UNION
25
8
11
6
25
23
2
35
7
RUVU SHOOTING
24
8
7
9
21
23
-2
31
8
JKT OLJORO
25
7
8
10
21
26
-5
29
9
TANZANIA PRISONS
25
7
8
10
16
22
-6
29
10
JKT RUVU
25
7
5
13
21
38
-17
26
11
MGAMBO SHOOTING
24
7
4
13
16
24
-8
25
12
POLISI MOROGORO
25
4
10
11
13
23
-10
22
13
TOTO AFRICAN
25
4
10
11
21
33
-12
22
14
AFRICAN LYON
25
5
4
16
16
38
-22
19
-AFRICAN LYON IMESHUKA DARAJA

Wednesday, May 8, 2013

SIR KATIKA ULIMWENGU WA SOKA AMUA KUSTAFU MWENYEWE

                         SIR ALEX FERGUSON
Alex Ferguson.jpg
TAARIFA KUHUSU YEYE
Full nameSir Alexander Chapman Ferguson[1]
Date of birth31 December 1941 (age 71)
Place of birthGlasgowScotland
Playing positionForward
TIMU ANAYOFUNDISHA
Current clubManchester United (manager)

TIMU ZA UKUBWA
YearsTeamMechi(Goli)
1957–1960Queen's Park31(15)
1960–1964St. Johnstone37(19)
1964–1967Dunfermline Athletic89(66)
1967–1969Rangers41(25)
1969–1973Falkirk95(36)
1973–1974Ayr United24(9)
Total317(170)
TIMU YA TAIFA
1967Scottish League XI2(1)
1967Scotland XI7(9)

UKOCHA
1974East Stirlingshire
1974–1978St. Mirren
1978–1986Aberdeen
1985–1986Scotland
1986–2013Manchester United


MATAJI AKIWA NA TIMU HIZI
ST MIRREN
Scotland Kwanza Idara (1): 1976-1977

ABERDEEN
Scottish Premier Idara ya (3): 1979-80, 1983-84, 1984-85
Scotland Kombe (4): 1981-82, 1982-83, 1983-84, 1985-86
Scotland Kombe la Ligi (1): 1985-1986
Kombe la UEFA Cup Winners '(1): 1982-1983
UEFA Super Cup (1): 1983

MANCHESTER UNITED
Ligi kuu (13): 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13
Kombe la fa (5): 1989-90, 1993-94, 1995-96, 1998-99, 2003-04
Kombe la ligi (4): 1991-92, 2005-06, 2008-09, 2009-10
FA Charity / Community Shield (10): 1990 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011
Ligi ya mabingwa (2): 1998-99, 2007-08
Kombe la uefa cup winners '(1): 1990-1991
Uefa super cup (1): 1991
Intercontinental cup (1): 1999
Fifa club world cup (1): 2008
TUZO BINAFSI ALIZOTWAA
1.Lma Meneja wa Muongo (1): 1990
2.Lma Meneja wa Mwaka (3): 1998-99, 2007-08, 2010-11
3.Lma Maalum Usahihi tuzo (2): 2009, 2011
4.Ligi Kuu Meneja wa Msimu (10): 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11
5.Ligi Kuu Meneja wa Mwezi (27): Agosti 1993, Oktoba 1994, Februari 1996, Machi 1996, Februari 1997, Oktoba 1997, Januari 1999, Aprili mwaka 1999, Agosti 1999, Machi 2000, Aprili 2000, Februari 2001, Aprili 2003, Desemba 2003, 8.Februari 2005, Machi 2006, Agosti 2006, Oktoba 2006, Februari 2007, Januari 2008, Machi 2008, Januari 2009, Aprili 2009, Septemba 2009, Januari 2011, Agosti 2011, Oktoba 2012
9.UEFA Meneja wa Mwaka (1): 1998-1999
10.UEFA Timu ya Mwaka (2): 2007, 2008
11.Onze d'Or Kocha wa Mwaka (3): 1999, 2007, 2008
12.IFFHS Dunia Best Club Kocha (2): 1999, 2008
13.IFFHS Dunia Best Kocha wa karne ya 21 (1): 2012
14.Dunia soka Magazine Dunia Meneja wa Mwaka (4): 1993, 1999, 2007, 2008
15.Laureus World Sports tuzo kwa ajili ya Timu ya Mwaka (1): 2000
16.BBC Sports Personality wa Tuzo ya Kocha Mwaka (1): 1999
17.BBC Sports Personality Team wa Tuzo ya Mwaka (1): 1999
18.BBC Sports Personality wa Tuzo ya Mwaka Lifetime Achievement (1): 2001
19.Kiingereza Football Hall of Fame (Meneja): 2002
20.Ulaya Hall of Fame (Meneja): 2008
21.FIFA Rais tuzo: 2011
22.Ligi Kuu ya 10 Seasons Awards (1992-1993 - 2001-02)
23.Ligi Kuu ya 20 Seasons Awards (1992-1993 - 2011-12)
24.Meneja wa Muongo
25.Wengi Coaching Mwonekano (392 michezo)
26.FWA Tribute tuzo: 1996
27.PFA Usahihi tuzo: 2007
28.Mussabini medali: 1999
MAAGIZO NA TUZO MAALUM

1.Afisa wa Mpango wa Dola ya Uingereza (OBE): 1983
2.Kamanda wa Mpango wa Dola ya Uingereza (CBE): 1995
3.Knight Shahada (Kt.): 1999

YANGA KUJIWEKA SAWA KWA WATANI WA JADI SIMBA

WANDINGA wa Jangwani mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, kinatarajia kuingia  kambini kesho kutwa Ijumaa kwa lengo i ya kujiweka sawa na mechi dhidi ya watani wao Simba utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Mei 18.
Kwa mujibu wa habari tulizofanikiwa kuzipata kutoka ndani ya klabu hiyo, bado haijaamuliwa mahali timu itakapoweka machimbo  lakin sehemu hizi zinatazamwa sana kati ya Zanzibar na Bagamoyo mkoani Pwani.
Yanga kwa sasa inaendelea kujiweka  sawa katika dimba la uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola ulioko Mabibo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mtanange wao dhidi ya watani wao wa jadi simba sc mchezo utakaopigwa tarehe 18 mei 2013.
Vijana hao wa Jangwani, wametwaa ubingwa msimu huu baada kufikisha pointi 57 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

MIKOA YATAKIWA KUCHEZESHA COPA COCA-COLA WILAYANI

VYAMA vya Mpira wa Miguu vya mikoa vinatakiwa kuendelea na mashindano ya Copa Coca-Cola yanayoshirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15 katika ngazi ya wilaya wakati vikisubiriwa vifaa na fedha za uendeshaji kutoka kwa mdhamini.

Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano (roadmap), mashindano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wilaya yanatakiwa kufanyika na kukamilika ndani ya mwezi Mei mwaka huu ili baadaye kuendelea na hatua inayofuata.

Hivyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawataka wanachama wake (vyama vya mpira wa miguu vya mikoa) ambao wamejipanga kuendelea na mashindano wakati suala la vifaa na fedha likiendelea kufuatiliwa kwa mdhamini wa mashindano.

Vifaa na fedha zitapatikana wakati wowote baada ya taratibu husika kukamilika. Vifaa kwa ajili ya mashindano hayo vimeagizwa kutoka nje ya Tanzania.

Ni matumaini yetu kuwa tutakuwa na mashindano mazuri mwaka huu kulinganisha na msimu uliopita. Kampuni ya Coca Cola ilianza kudhamini mashindano hayo mwaka 2007, na tangu mwaka huo yamekuwa yakifanyika kila mwaka.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

KASEJA ASEMA SIWEZI KUZUNGUMZA LOLOTE KUHUSU MSIMBAZI

BAADA ya kuhusishwa na kuhamia katika klabu ya Ashanti, ambayo imepanda kucheza Ligi Kuu msimu ujao, Kipa namba moja wa timu ya Simba na ile ya Taifa, Juma Kaseja amesema ataweka wazi ni wapi ataenda baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu Kaseja amesema, ni mapema kuzungumzia hilo kwani ligi bado haijamalizika, ila atafanya hivyo mara tu ligi itakapomalizika.

 
Mkataba wangu unaisha mwezi Juni, hivyo wapenzi na mashabiki wangu kwa sasa watataka kujua nafanya nini, nawaahidi watajua hilo ligi itakapomalizika wakati mkataba wangu pia ukielekea ukingoni.
 
Kaseja amesema Mimi kama mchezaji nina malengo yangu, wasipate tabu nitasema mwenyewe na mtajua tu nini natarajia kufanya.
Aidha Kaseja kwa sasa ni mmoja wa wachezaji wakongwe hapa nchini na kutumainiwa katika kikosi cha Simba, na ameitumikia kwa mafanikio makubwa.

Hata hivyo mchezaji huyo alishawahi kufanya maamuzi magumu, kwa kuhamia kwa mahasimu wakubwa wa Simba, timu ya Yanga ambapo alicheza kwa msimu mmoja.

TIMU YA TAIFA YA BRAZIL KUZINDUA UWANJA WA MARICANA .

TIMU ya taifa ya Brazil inatarajiwa kuzindua rasmi uwanja wake uliokuwa katika matengenezo wa Maricana wakati watakapoikarinisha Uingereza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki mwezi ujao. Mapema ilifahamika kuwa kabla ya mchezo huo kungekuwa na mechi ya majaribio Mei 15 lakini halmashauri ya jiji la Rio de Janeiro liliahirisha mchezo huo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi. Uwanja huo ambao utatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho baadae mwezi ujao na Kombe la Dunia 2014 ulifunguliwa mwishoni mwa mwezi jana huku ukiwa umechelewa kwa miezi minne. Mechi baina ya Brazil na Uingereza mbayo itahezwa Juni 2 mwaka huu katika uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 78,000 ndio itakuwa pekee kabla uwanja huo haujatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho kuanzia Juni 15 hadi 30 mwaka huu. Ukarabati wa uwanja huo ambao umewahi kuweka historia ya kuingiza watu wengi zaidi wanaofikia 199, 858 katika mchezo wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 1950, umegharimu kiasi cha dola milioni 448 huku ukipunguzwa na kuwa na uwezo wa kuingiza watu 78,838 kwasasa.

FERGUSONA ATANGAZA RASMI KUTAAFU OLD TRAFORD


SIR ALEX FERGUSON Meneja wa klabu ya Manchester United,anatarajia kustaafu kuinoa klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu Katika mechi ya mwisho ya BPL dhidi ya West Bromich albion mei 18 mwaka huu baada ya kuifundisha kwa kipindi cha miaka 26 yenye mafanikio makubwa. Ferguson raia wa Scottland mwenye umri wa miaka 71 ameshinda mataji 38 tok alipochukua mikoba ya Ron Atkinson Novemba 1986, likiwemo taji la Ligi Kuu nchini Uingereza msimu huu. Mataji hayo yanajumuisha 13 ya ligi, mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, matano ya Kombe la FA na manne ya Kombe la Ligi. 
Ferguson amesema uamuzi huo wa kustaafu ni uamuzi ambao ameufikiria kwa kipindi kirefu na kujiridhisha kwamba sasa ni muda muafaka wa kufanya hivyo. Kocha huyo amesema amesema ilikuwa ni muhimu kwake kustaafu huku akiiacha klabu hiyo ikiwa imara na anaamini amefanya hivyo na anategemea itaendelea kuwa juu kwa kipindi kirefu kijacho kutokana na damu changa atakazoziacha.

FERGUSON-MATAJI YAKE:
-PREMIER LEAGUE: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999,
2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013.
-FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
-LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
-UEFA CHAMPIONS LEAGUE: 1999, 2008
-UEFA CUP WINNERS CUP: 1991
-FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
-UEFA SUPER CUP: 1992
-FIFA INTER-CONTINENTAL  CUP: 1999
-FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011