Saturday, May 18, 2013

PATA MAKALA KUHUSU CLUB YA MAN UNITED KATIKA HARAKATI ZA SOKA.

                                                        SEHEMU YA KWANZA. 
Manchester United ni klabu ya kandanda  ndani ya nchi ya Uingereza, ambacho ni mojawapo ya vilabu maarufu sana ulimwenguni makao  yake yapo Old Trafford eneo la Greater Manchester. Klabu hii ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa Ligi ya Primia mwaka 1992, na kimeshiriki mara nyingi katika soka la Uingereza tangu mwaka wa 1938, isipokuwa msimu wa 1974-75. Mahudhurio ya wastani  ya klabu  hii yamekuwa ya juu kuliko timu nyingine yoyote katika  soka la Uingereza kwa misimu yote isipokuwa sita tangu 1964-65.
Manchester United ndiyo bingwa wa sasa wa Uingireza na ndio wasshiriki wa Kombe la Dunia la Vilabu, baada ya kushinda Ligi ya Primia 2008-09 na Kombe la Dunia la FIFA. Klabu hicho ni miongoni mwa vilabu vyenye ufanisi mkubwa katika historia ya kandanda la Uingereza na kimeshinda mataji makubwa 22 tangu Alex Ferguson alipochukua wadhifa wa meneja wake mnamo Novemba 1986. Mwaka wa 1968 ilikuwa klabu cha kwanza kushinda Kombe la Uropa kwa kuifunga  Benfica 4-1. Walishinda kombe la pili la Ulaya kama sehemu ya ushindi wa mataji matatu mwaka 1999, na la tatu mwaka wa 2008, kabla ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka 2009. Kilabu hicho kinashikilia rekodi mbili ya kushinda mataji mengi ya Ligi ya Uingereza mara 18 na pia kushikilia rekodi kwa wingi wa kutwaa kombe la FA ikiwa imeshinda mara 11.
Tangu mwisho wa mwaka ya 1990, kilabu hicho kimekuwa mojawapo ya vilabu tajiri duniani kilicho na mapato ya juu kuliko kilabu chochote,na sasa kinatajwa kama kilabu chenye thamani zaidi katika mchezo wowote, na makisio ya thamana ya takriban bilioni £ 1.136 (bilioni € 1.319 ) Aprili 2009.Manchester United ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa kundi la vilabu la G-14 la Vilabu kuu vya kandanda Uingereza ambalo halipo tena, na European Club Association ,muungano uliochukua nafasi yake.
Alex Ferguson amekuwa meneja wa kilabu hicho tangu 6 Novemba 1986 alipojiunga na kilabu hicho kutoka Aberdeen baada ya kung'atuka kwa Ron Atkinson. Nahodha wa kilabu wa sasa ni Garry Neville, aliyechukua nafasi ya Roy Keane Novemba 2005.

Friday, May 17, 2013

IFAHAMU KWA UZURI MAN UNITED KATIKA HARAKATI ZA SOKA ULIMWENGUNI

MANCHESTER UNITED
MATAJI VIKOMBE ILIVYOTWAA:
UBINGWA:
LIGI KUU:VPL
1992–93, 1993–94, 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13
DARAJA LA 1:
1907–08, 1910–11, 1951–52, 1955–56, 1956–57, 1964–65, 1966–67
DARAJA LA 2:
1935–36, 1974–75
VIKOMBE:
FA CUP: 11
1908–09, 1947–48, 1962–63, 1976–77, 1982–83, 1984–85, 1989–90, 1993–94, 1995–96, 1998–99, 2003–04
LIGI CUP: 4
1991–92, 2005–06, 2008–09, 2009–10
FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 19
1908, 1911, 1952, 1956, 1957, 1965, 1967, 1977, 1983, 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011
ULAYA:
EUROPEAN CUP / UEFA CHAMPIONS LEAGUE: 3
1967–68, 1998–99, 2007–08
UEFA CUP WINNERS' CUP: 1
1990–91
EUROPEAN SUPER CUP: 1
1991
DUNIA:
INTERCONTINENTAL CUP: 1
1999
FIFA CLUB WORLD CUP: 1
2008
MATAJI YAKE: SIR FERGUSON-
-PREMIER LEAGUE: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999,
2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013.
-FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
-LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
-UEFA CHAMPIONS LEAGUE: 1999, 2008
-UEFA CUP WINNERS CUP: 1991
-FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
-UEFA SUPER CUP: 1992
-FIFA INTER-CONTINENTAL  CUP: 1999
-FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011

Endelea kupata taarifa zaidi kupitia mkali wa dimba tz.blogspot.com ambayo inakuletea makala kamili kuhusu Club hii bora kabisa duniani ya manchester united kaa mkao wa kuburudika kimichezo zaidi karibu wewe mdau wa blog hii>>>>>>>

KOMBE LA DUNIA: DROGBA , YAHAYA TOURE WAWEKWA PEMBEENI

KOCHA WA IVORY COAST Sabri Lamouchi, ametangaza Kikosi chake cha Wachezaji 26 kwa ajili ya Mechi za KUNDI C la kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka 2014 watakazocheza Mwezi ujao dhidi ya Gambia na Tanzania na hawamo Maveterani Didier Drogba na Kolo Toure.
Drogba, mwenye Miaka 35 ambae sasa anacheza huko Uturuki na Galatasaray, pia hakuchukuliwa kwenye Kikosi cha Ivory Coast kilichocheza Mechi ya KUNDI C ya Kombe la Dunia Mwezi Machi walipocheza na Gambia.
Hadi sasa Drogba ameichezea Nchi yake Mechi 96 na kufunga Bao 60.
MSIMAMO:
KUNDI C
1 Côte d'Ivoire Mechi 3 Pointi 7
2 Tanzania Mechi 3 Pointi 6
3 Morocco Mechi 3 Pointi 2
4 Gambia Mechi 3 Pointi 1
RATIBA/MATOKEO:
02/06/12: Ivory Coast 2-0 Tanzania; Gambia 1-1 Morocco
08-12/06/12: Morocco 2-2 Ivory Coast; Tanzania 2 Gambia 1
22-26/03/13: Ivory Coast 3 Gambia 0; Tanzania 3 Morocco 1
07-11/06/13: The Gambia v Ivory Coast; Morocco v Tanzania [Juni 8]
14-18/06/13: Tanzania v Ivory Coast; Morocco v The Gambia
06-10/09/13: Ivory Coast v Morocco; Gambia v Tanzania

PEDRO ASEMA LAZIMA TUVUNJE REKODI YA REAL MADRIDI

WINGA Machachali wa klabu ya Barcelona, Pedro Rodriguez amedai kuwa yeye na wachezaji wenzake wana nia ya kufikia rekodi ya Real Madrid ya alama 100 baada ya kufanikiwa kunyakuwa taji la La Liga mwishoni mwa wiki iliyopita. Barcelona walikabidhiwa taji lao la 22 la ligi wakati mahasimu wao Madrid waliposhindwa kuwafunga Espanyol na kutoa sare ya 1-1 na wako katika nafasi nzuri ya kuvunja rekodi hiyo ya Madrid kama wakishinda mechi zao zilizobakia. Mchezaji huyo amesema kwasasa nguvu zao wanazielekeza katika kusaka alama 100 ingawa amekiri kuwa itakuwa kazi ngumu kutokana na timu watakazocheza nazo. Nyota huyo pia alisisitiza kuwa msimu huu umekuwa wa mafanikio kwao pamoja na kuenguliwa na Bayern Munich katika nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

MESSI ASEMA TULICHEZA KWA WAKATI MGUMU BILA VILANOVA

MSHAMBULIAJI nyota Duniani wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amekiri kuwa ilikuwa ni ngumu kupambana na mazingira yaliyokuwepo wakati Tito Vilanova alipolazimika kuondoka katikati ya msimu huu. Vilanova aliondoka na kuliacha benchi la ufundi la klabu hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu baada kukutwa na saratani ya koo Desemba 2012 ambapo Muargentina huyo anafurahia kwamba timu hiyo imeweza kunyakuwa taji pamoja na kumkosa kiongozi wao. Messi amesema amefurahi timu yake kunyakuwa taji hilo ingawa amekiri haikuwa kazi rahisi kunywakuwa taji hilo haswa kipindi ambacho walimkosa Vilanova aliyekwenda kwa matibabu kwani mabadiliko ya wazi yalionekana katika kikosi chao. Nyota huyo aliendelea kusema kuwa kutolewa kwao na Bayern Munich katika nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imekuwa ni changamoto kwao kwani watajipanga na kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi. Amesema kwasasa timu na makocha wengi wamefanikiwa kung’amua aina ya mchezo wanaocheza hivyo kuwadhibiti lakini amedai kuwa haina maana timu hiyo inapaswa kubadilisha aina mchezo wao wa pasi nyingi kwani ndio unaowatambulisha duniani kote.

SHARAPOVA AJIWEKA PEMBENI MICHUANO YA ITALIAN OPEN.

MWANARIADHA nyota wa kike wa  mchezo wa tenisi, Maria Sharapova amejitoa katika michuano ya wazi ya Italia kabla ya mchezo wake wa robo fainali dhidi ya Sara Errani wa Italia kutokana na matatizo ya kimwili. Sharapova ambaye ni raia amejitoa mapema kwenye michuano hiyo ili aweze kupona haraka kwa ajili ya kutetea taji lake la michuano ya wazi ya Ufaransa baadae mwezi huu. Kwa upande mwingine mwanadada anayesshika namba moja katika orodha za ubora Serena Williams wa Marekani ameendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kumchakaza bila huruma Dominika Cibulkova wa Slovakia kwa 6-0 6-1 na kutinga robo fainali ya michuano hiyo. Williams ambaye ameshinda mechi 21 mfululizo sasa atachuana na Carla Suarez Navarro wa Hispania kutafuta nafasi ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

FA YAWEKA SHERIA KALI KATIKA SUALA ZIMA LA UBAGUZI

SHIRIKISHO la Soka la Uingereza-FA linatarajia kutoa adhabu mpya ya mechi tano kwa mchezaji atakayekutwa na hatia ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi mchezaji mwenzake msimu ujao. Katika kikao hicho cha mwaka cha FA kimedai katika taarifa yake kuwa kama mtuhumiwa akirudia kosa moja kwa moja atapewa adhabu ya mechi 10 zaidi. Klabu pia inaweza kutozwa faini ikiwa wachezaji wawili au zaidi watakutwa na hatia ya kufanya vitendo hivyo katika kipindi cha miezi 12. Mwenyekiti wa FA David Bernstein amesema wamefikia uamuzi huo kwasababu wanataka kila mchezaji acheze soka akiwa salama na katika mazingira mazuri. Beki wa Chelsea John Terry alifungiwa mechi nne na kutozwa faini ya paundi 220,000 kwa kumfanyia vitendo vya ubaguzi beki wa Queens Park Rangers Anton Ferdinand Octoba mwaka 2011 wakati mshambuliaji wa Liverpool yeye alifungiwa mechi nane na faini ya paundi 40,000 msimu uliopita kwa kumbagua Patrice Evra wa Manchester United.