Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars), Rogasian
Kaijage amewaita kambini wachezaji 30 ikiwa ni mwendelezo wa kuijenga na
kuiimarisha timu hiyo.
Twiga
Stars itakuwa na kambi ya siku kumi kuanzia Jumapili (Mei 26 mwaka huu) ambapo
baadaye inatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya wachezaji kurudi
kwenye klabu zao.
Kambi
hiyo ni mwendelezo wa programu iliyopendekezwa na kocha kuijenga na kuiimarisha
timu hiyo kwa vile haina mashindano mwaka huu, na itakuwa kambi ya pili baada
ya ile iliyofanyika Machi mwaka huu.
Wachezaji
walioitwa na klabu zao kwenye mabano ni Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza
Mwadini (Zanzibar), Belina Julius (Lord Barden), Ester Chabruma (Sayari), Ester
Mayala (TSC Academy), Eto Mlenzi (JKT), Evelyn Sekikubo (Mburahati Queens) na
Fatuma Bushiri (Mburahati Queens).
Fatuma
Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Omari (Sayari), Flora Kayanda (Tanzanite),
Hamisa Athuman (Marsh Academy), Hellen Peter (JKT), Maimuna Said (JKT), Mwajuma
Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba
(Mburahati Queens) na Mwapewa Mtumwa (Sayari).
Nabila
Ahmed (Marsh Academy), Pulkeria Charaji (Sayari), Rehema Abdul (Lord Barden),
Rukia Khamis (Uzuri Queens), Semeni Abeid (Tanzanite), Sharida Boniface
(Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari), Therese Yona (TSC Academy),
Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).
RCL
KUENDELEA KUTIMUA VUMBI KESHO
Raundi
ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaendelea kesho (Mei 26 mwaka huu)
kwa mechi sita za kwanza zitakazochezwa katika miji sita tofauti.
Abajalo
ya Dar es Salaam na Kariakoo ya Lindi zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Dar es Salaam wakati Machava FC ya Kilimanjaro itakuwa mwenyeji wa
Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Nayo
Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye
Uwanja wa Namfua mjini Singida huku Polisi Jamii ya Bunda mkoani Mara
ikimenyana na Biharamulo FC ya Kagera kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
mjini Musoma.
Mjini
Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi
Warriors ya Katavi wakati Njombe Mji itaikaribisha Kimondo SC ya Mbeya kwenye
Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Leo
(Mei 25 mwaka huu) Friends Rangers ya Kinondoni, Dar es Salaam inacheza na
African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Azam Chamazi. Mechi za marudiano
zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.
Timu
zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na
9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)