Tuesday, May 28, 2013

TORRES VS CASILLAS WAITWA TIMU YA TAIFA

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amemuita golikipa Iker Casillas na mshambuliaji Fernando Torres katika kikosi cha wachezaji 26 ambacho kitaanza maandalizi ya Kombe la Shirikisho linalotarajiwa kuanza mwezi ujao nchini Brazil. Orodha hiyo ya wachezaji 26 itapunguzwa na kufikia 23 baada ya mzunguko wa mwisho wa mechi za Ligi Kuu nchini Hispania mwishoni mwa wiki ijayo. Hispania ambao ni mabingwa wa Dunia na Ulaya wana mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Haiti Juni 8 na Ireland siku tatu baadae kabla ya kuelekea nchini Brazil. Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Hispania imepangwa katika kundi B sambamba na Uruguay, Tahiti na Nigeria ambapo mchezo wa ufunguzi utachezwa Juni 16 dhidi ya Uruguay. 
Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu nane inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 15 mpaka 30. 
Goalkeepers: Iker Casillas (Real Madrid), Victor Valdes (Barcelona), Pepe Reina (Liverpool)

Defenders: Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Jordi Alba (Barcelona), Ignacio Monreal (Arsenal), Raul Albiol (Real Madrid), Javi Garcia (Manchester City)

Midfielders: Javi Martinez (Bayern Munich), Xavi (Barcelona), Andres Iniesta (Barcelona), Sergio Busquets (Barcelona), Santi Cazorla (Arsenal), Xabi Alonso (Real Madrid), Benat Etxebarria (Real Betis)
Forwards: Cesc Fabregas (Barcelona), David Villa (Barcelona), David Silva (Manchester City), Roberto Soldado (Valencia), Pedro (Barcelona), Juan Mata (Chelsea), Jesus Navas (Sevilla), Fernando Torres (Chelsea).

Monday, May 27, 2013

FRANK RIBERY ATANABAISHA KULALA NA KOMBE LA UEFA LIGI.

WINGA maarufu wa klabu ya Bayern Munich, Franck Ribery ametanabaisha kuwa alichukua Kombe la Ligi ya Mabingwa na kwenda nalo kitandani kufuatia ushindi wa timu yao wa mabao 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund. Bayern wamefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo mara tatu katika kipindi cha  miaka minne lakini walifanikiwa kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza toka mwaka 2001 kwa ushindi waliopata katika Uwanja wa Wembley Jumamosi. Na Ribery alibainisha hilo katika sherehe za kulitembeza kombe hilo mtaani huko Ujerumani kwamba alichukua kombe hilo na kwenda nalo nyumbani. Nyota huyo raia wa Ufaransa amesema alikuwa macho mpaka alfajiri na baadae kwenda kulala akiwa na mke wake pamoja na kombe hilo. Bayern sasa wana nafasi ya kushinda matatu matatu kwa mkupuo kama wakifanikiwa kushinda taji la DFB Pokal Juni mosi mwaka huu.

BENITEZ ATAKA KUIFUNDISHA TIMU INAYOSHIRIKI LIGI YA MABINGWA ULAYA.

MENEJA wa muda wa klabu ya Chelsea Rafael Benitez ametanabaisha kuwa anataka kufundisha timu inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza kazi yake katika klabu hiyo.
Katika kipindi kifupi kijacho Benitez ataondoka Stamford Bridge akiwa ameisimamia klabu hiyo kwa mara ya mwisho Jumamosi iliyopita wakati walipocheza na Manchester City katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jijini New York Marekani.
Kocha huyo raia wa Hispania ameiongoza Chelsea kushinda taji la Europa League pamoja na kuisadia kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kuajiriwa kwa muda mfupi kuziba nafasi ya Roberto Di Matteo Novemba mwaka jana. 
Banitez anaondoka Chelsea kumpisha Jose Mourinho na kocha huyo sasa anaweza kuangalia mstakabali wake wa kuhusishwa na tetesi za kwenda Napoli na Paris Saint-Germain ambapo klabu zote hizo zinakidhi matakwa yake ya kushiriki Ligi ya Mabingwa.

RADAMEL FALCAO HATIMAYE ATUA KATIKA CLUB YA MONACO

STRAIKA MAHIRI wa Atletico Madrid, Radamel Falcao, atapimwa afya yake kwenye Klabu ya Monaco ambayo imepanda Daraja Msimu huu kurudi Ligue 1 ya France na Uhamisho wake unatarajiwa kugharimu Dau la Pauni Milioni 51.
Habari hizi zimevuja huko Spain na kudaiwa kuwa Atraika huyo kutoka Colombo atapimwa afya yake siku ya Jumatatu Mei 27.
Monaco, ambayo imenunuliwa na Tajiri wa Kirusi Dmitry Rybolovlev, tayari imeshawanunua Mastaa wa FC Porto Joao Moutinho na James Rodriguez kwa Dau la Jumla ya Pauni Milioni 60 na kutua kwa Falcao kutawafanya watatu hao wakutane tena kwani waliwahi kuchezea Klabu moja.
Kuhama kwa Falcao kulidokezwa na Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ambae ameshasema hatakuwa na kinyongo ikiwa Falcao, mwenye Miaka 27, atahama.
Hivi Juzi, Kocha Msaidizi wa Monaco, Jean Petit, alidokeza wanatarajia Falcao na Wachezaji wengine wanne au watano wa kiwango chake kununuliwa na Klabu yao.
Mwezi Desemba 2011, Dmitry Rybolovlev alinunua Hisa za Asilimia 60 za Klabu ya Monaco na kuanza kuibadili wakati huo ikiogelea Daraja la chini huko France, Ligue 2, na Mwezi Mei 2012 alimteua Kocha wa zamani wa Chelsea Claudio Ranieri kuiongoza Monaco na amefanya hilo kwa mafanikio kwa kuirudisha Monaco Daraja la juu huko France.

NEYMAR HATIMAYE SASA ATUA FC BARCELONA

CLUB ya soka FC Barcelona imefikia Makubaliano na Klabu ya Brazil, Santos, ya kumsaini Neymar ambapo leo Jumatatu Mei 27 atasaini Mkataba ili kukamilisha Dili hiyo ya Uhamisho.
Klabu ya Barcelona imetoa Taarifa rasmi ya kuthibitisha kufikia makubaliano ya kumsaini Nyota huyo wa Brazil mwenye Miaka 21.
WASIFU:
Neymar da Silva Santos Junior
KUZALIWA: 5 Februari 1992, Nchini Brazil
Santos: Mechi 229 Magoli 138
Brazil: Mechi 32 Magoli 20
Na Mwenyewe Neymar alitoa Ujumbe kwenye Mtandao wa Instagram uliosema  kuwa jumatatu nasaini Mkataba na Barcelona. Nataka kuwashukuru Mashabiki wa Santos kwa Miaka hii 9 ya ajabu.
Juzi Klabu ya Santos ilitoa Taarifa kuwa imepokea Ofa mbili za kumnunua Neymar na ilisadikiwa zimetoka toka mbili kati ya Klabu za Barcelona, Real Madrid au Chelsea.
Mkataba wake na Santos ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa Msimu ujao, Mwezi Juni 2014.
Neymar anatarajiwa kujiunga na Barcelona mara baada ya kuiwakilisha Brazil kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yatakayochezwa Nchini Brazil kuanzia Juni 15 hadi 30.
Neymar ndie ameiongoza Santos kupata mafanikio makubwa tangu Nguli Pele aache kuichezea Klabu hiyo kwenye Miaka ya 1970 kwa kuisaidia kutwaa Kombe la Brazil Mwaka 2010, Copa Libertadores Mwaka 2011 na Ubingwa wa Jimbo la Sao Paolo kwa mara 3 mfululizo.
Nayo Klabu ya Santos imesema kuwa ilijaribu kila njia ili Neymar abaki kwao lakini Ofa za nje zimewafanya wasiweze kushindana.
Hata hivyo, Santos imekataa kutaja Dili hiyo ya Uhamisho imegharimu kiasi gani kwa vile kila upande umekubaliana kuwa iwe siri.
             
WASIFU WA NEYMAR
Taarifa kuhusu yeye
Full name Neymar da Silva Santos Júnior
Date of birth 5 February 1992 (age 21)
Place of birth Mogi das Cruzes, Brazi
Height 1.74 m (5 ft 9 in)
Playing position Mshambuliaji
Club ya sasa
Current club Santos
Number 11
Timu za ujana
1999–2003 Portuguesa Santista
2003–2009 Santos
Timu ya ukubwa
Years Team Mechi Goli
2009– Santos 103 (54)
Timu ya Taifa
2009 Brazil U17 3 (1)
2011 Brazil U20 7 (9)
2012 Brazil U23 7 (4)
2010– Brazil 32 (20)

AGUERO BADO NIPO NIPO MAN CITY MPAKA 2017.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester City, Sergio Aguero ameongeza mkataba wa mwaka mmoja ambao utamuweka katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza mpaka mwaka 2017. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 12 katika mechi 30 za ligi alizocheza msimu uliopita na kufunga bao la ushindi dhidi ya Queens Park Rangers lililowapa taji la ligi katika msimu wa 2011-2012. Mara baada ya kusaini mkataba huyo Aguero aliuambia mtandao wa klabu hiyo kwamba anajisikia furaha na kuhitajika hivyo atafanya kila awezalo ili aendelee kufanya kazi vyema na kuipa mataji klabu hiyo. Vyombo vya habari nchini Uingereza vilikuwa vikiripoti kuwa mchezaji huyo anaweza kutimkia Real Madrid lakini tetesi hizo zitakwisha baada ya kuwa mchezaji mwingine wa timu hiyo kuongeza mkataba baada ya Gael Clichy, Yaya Toure na David Silva kufanya hivyo.

KLOPP ASEMA TUTAIMARISHA KIKOSI FAINALI ZIJAZO

MENEJA wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp ametanabaisha kuwa ataimarisha kikosi chake na kufikia fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kipigo walichopata dhidi ya Bayern Munich. Dortmund walipoteza mchezo huo ulizikutanisha timu zote kutoka Ujerumani kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Wembley baada ya bao la dakika za mwisho lililofungw ana Arjen Robben. Lakini kocha huyo ametamba kuwa pamoja na kushindwa katika fainali hiyo ya Wembley lakini anaamini atafikia fainali nyingine katika kipindi kifupi kijacho. Klopp amesema kwasasa ana kazi kubwa ya kuimarisha kikosi chake baada ya wachezaji kadhaa tegemeo kutaka kuondoka mwishoni mwa msimu huu lakini anaamini mpaka kufikia msimu mpya tayari atakuwa na kikosi imara. Kiungo tegemeo wa klabu hiyo Mario Gotze tayari imeshathibitishwa kwenda Bayern Msimu ujao huku mshambuliaji wake nyota Robert Lewandowski naye akijipanga kuelekea huko.