Thursday, June 6, 2013

PEREZ. AWEKA WAZI KUWA ZIDANE HANA UZOEFU WA KUTOSHA KUWA KOCHA.

Florentino Perez rais wa klabu ya Real Madrid ametanabaisha na kusema kuwa Zinedine Zidane ana vigezo vyote vinavyohitajika kuchukua nafasi ya Jose Mourinho lakini anadhani bado anahitaji uzoefu zaidi kabla ta kukabidhiwa mikoba hiyo. Perez amesema Zidane ana kila kitu ambacho kocha anatakiwa kuwa nacho na kazi hiyo anaiweza lakini bado anahitaji uzoefu ili kukabidhiwa majukumu makubwa kama hayo. Kwasasa chaguo la kwanza la Madrid katika kutafuta mbadala wa Mourinho ni kocha wa Paris Saint-Germain Carlo Ancelotti ingawa Perez alishindwa kuliongelea kwa kuogopa kuwachukiza PSG ambao bado wamemng’ang’ania kocha huyo. Zidane ambaye ameichezea Madrid kuanzia mwaka 2001 mpaka 2006 kwasasa ni mkurugenzi wa michezo na kocha wa vijana wa klabu hiyo.


      WASIFU WA  ZIDANE
Zinedine Zidane 2008.jpg
Taarifa kuhusu yeye
Full name
Zinedine Yazid Zidane
Date of birth
23 June 1972 (age 40)
Place of birth
Marseille, France
Height
1.85 m (6 ft 1 in)
Playing position
Timu za Ujana
1982–1983
US Saint-Henri
1983–1986
SO Septèmes-les-Vallons
1986–1989
Timu za Ukubwa
Mwaka
Timu
Mechi
Goli
1989–1992
61
(6)
1992–1996
139
(28)
1996–2001
151
(24)
2001–2006
155
(37)
Total
506
(95)
Timu ya Taifa
1988–1989
4
(1)
1989–1990
6
(0)
1990–1994
20
(3)
1994–2006
108
(31)

MARTINEZ ACHUA NAFASI YA DAVID MOYES KUIFUNDISHA EVERTON.

MENEJA wa zamani wa klabu ya Wigan Athletic, Roberto Martinez ameteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Everton akichukua mikoba ilioachwa wazi na David Moyes aliyekwenda Manchester United. Martinez mwenye umri wa miaka 39 alifanikiwa kutwaa taji la Kombe la FA msimu huu, lakini aliomba kuondoka baada ya kuihakikishia timu hiyo nafasi ya kubakia katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Mwenyekiti wa Wigan, Dave Whelan alimruhusu kocha huyo raia wa Hispania kuondoka na tayari wako katika mchakato wa kutafuta kocha mwingine wa kuziba pengo hilo. Martinez ambaye pia amewahi kuinoa Swansea City alijiunga na Wigan Juni mwaka 2009 na Aston Villa walitaka kumchukua mwaka 2011 lakini aliamua kubakia Wigan mpaka msimu huu alipoamua kuelekea Everton.

Tuesday, June 4, 2013

PEREZ AWEKA WAZI KUWA RONALDO ATABAKI REAL MADRID"

Florentino Perez rais wa club ya Real Madrid ametanabaisha kuwa ana mategemeo kuwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo atabakia Santiago Bernabeu katika kipindi chote cha maisha yake ya soka. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno, mapema mwaka jana alidokeza kuwa hakuwa anafurahia maisha ya Madrid na toka wakati huko amekuwa akihusishwa na mpango wa kurejea Manchester United pamoja na Paris Saint-Germain-PSG. Lakini Perez amedai kuwa atafanya kila awezalo ili nyota huyo aweze kuwa na furaha katika klabu hiyo na kumalizika muda wake wa kucheza soka akiwa hapo. Perez pia aluzungumzia mustakabali ya mshambuliaji mwingine Gonzalo Higuain na kudai kuwa hakuna yoyote aliyemwambia kwamba mchezaji huyo ataondoka kwani klabu hiyo haijamuweka sokoni katika kipindi cha usajili. Ambapo aliongeza kuwa kama mchezaji mwenyewe ndio anataka kuondoka basi klabu itakayomhitaji itatakiwa kuwalipa lakini mpaka sasa ahkuna klabu yoyote iliyojitokeza kumtaka mchezaji huyo.

KATIKA MISUKOSUKO YA HAPA NA PALE SASA ATUA COAST"


Baada ya kupata misukosuko ya hapa na pale katika Club ya wekundu wa msimbazi SC kiungo Haruna Moshi Shaaban ‘Boban hatimaye amefanikiwa kutua  ndani ya jiji la tanga kuichezea Coastal union mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
hivyo mpaka sasa Coastal union imekamilisha usajili wa wachezaji wanne wapya, akiwemo mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu, Abdallah Othman Ally. 
Ally anayecheza upande wa pembeni juu kushoto mwenye speed na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, amesaini Mkataba wa miaka miwili na Coastal Union ambayo tangu ipande tena Ligi Kuu mwaka juzi, imepania kurejesha makali yake. Mbali na Ally anayechezea pia timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.
Wagosi wa Kaya wamemrejesha kiungo waliyemuibua mwaka 2000 kabla ya kufuata maslahi Moro United, baadaye Simba SC na Geffle FF ya Sweden’.
Boban amerejea Tanga alipoanzia kucheza soka ya ushindani mwaka 2000 chini ya kocha maarufu zamani Mansour Magram, sasa marehemu akitokea sekondari ya Makongo, Dar es Salaam.
Aidha wagosi hao pia imesajili wachezaji wawili kutoka JKT Oljoro ya Arusha, kipa Said Lubawa na sentahafu Marcus Ndehele ambapo Mwenyekiti wa  Coastal Union Hemed Aurora hmed akizungumza na mtandao huu ametanabaisha na kusema kuwa bado wanatazama harakati za kuwanasa wachezaji watano zaidi kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi.  

Aidha Aurora ameongeza na kusema kuwa huu ni usajili wa uliokuwa na malengo na si wa kukurupuka na pia vilevile ni usajili unaotokana na mapendekezo ya benchi la ufundi la timu chini ya kocha mkuu, Ahmed Morocco ambaye alitaka wachezaji tisa ambao aliwapendekeza kwa majina yeye mwenyewe na sisi tumekuwa tukimfuata mmoja baada ya mwingine na kumalizana naye.
Hivyo kwa wakati huu bado tupo kwenye harakati za kumalizana na wengine watano ambpo Lengo letu ni kuhakikisha kocha anakuwa na timu atakayoridhika nayo kulingana na mapendekezo yake, hatutaki kuingilia kusajili hata mchezaji mmoja, alisema Aurora.
Mbali na hilo Aurora ameudokeza mtandao huu kuwa miongoni mwa wachezaji hao waliobaki mtazamo zaidi ni kumnasa beki aliepatwa na misukosuko kama ya Boban yaani beki mwenye nguvu na na uwezo wa kukaba Juma Nyoso.

Hata hivyo Aurora ameongeza na kusema kuwa mazoezi ya Coastal Union yataanza wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu, nje kidogo ya mji ambako kikosi kitapiga kambi kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya msimu mpya.

MAN CITY YAMNASA WINGA WA SEVILLA JESUS NAVAS.

Club ya soka ya Manchester City wamefikia makubaliano na Klabu ya Spain Sevilla ya kumnunua Winga wa Kimataifa wa Spain Jesus Navas.
Navas, mwenye Miaka 27, anategemewa kununuliwa kwa gharama ya Pauni Milioni 17.
Navas yumo kwenye Kikosi cha Spain kitakachocheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara huko Brazil kuanzia Juni 15.
Hadi sasa Man City haijatangaza nani Meneja wao mpya baada ya kumtimua Roberto Mancini ingawa wengi wanategemea Manuel Pellegrini, aliekuwa Malaga, ndio atachukua nafasi hiyo.

NEYMAR ASEMA MESS ATAENDELEA KUTISHA ZAIDI DUNIANI.

MSHAMBULIAJI nyota mpya wa klabu ya Barcelona, Neymar ametanabaisha anataka kumsadia nyota wa klabu hiyo Lionel Messi aendelee kung’ara duniani baada ya kukamilisha taratibu zote za uhamisho wake kutoka klabu ya Santos. Neymar mwenye umri wa miaka alikamilisha uhamisho wake wenye thamani ya euro million 57 na kumaliza utata wa miezi kadhaa juu ya mstakabali wa nyota huyo. Akihojiwa mara baada ya kutambulishwa rasmi mbele ya maelfu ya mashabiki katika uwanja wa Camp Nou, Neymar amesema anataka kuisaidia timu kwasababu Barcelona ni zaidi ya klabu na pia anataka kumsadia Messi aendelee kung’ara zaidi. Nyota huyo aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni ndoto zake kucheza katika klabu ambayo inahesabika kama mojawapo ya klabu bora duniani huku akizungukwa na wachezaji nyota. Neymar anaondoka Santos akiwa ameshinda Kombe la Brazil mwaka 2010, Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini mwaka 2011 huku akiwa amefunga mabao 138 katika mechi 229 alizocheza akiwa katika klabu hiyo.

TAIFA STAR YATUA MORROCO RASMI KWA MAANDALIZI YA MECHI ITAKAYO PIGWA JUNE 8.

Taifa Stars imewasili hapa Marrakech, Morocco leo- Juni 3 mwaka huu tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa Jumamosi- Juni 8 mwaka huu.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman ambayo pia Ivory Coast ilifikia ilipokuja kucheza hapa dhidi ya Morocco. Stars imetua na wachezaji 21 huku Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu waliokuwa Maputo, Msumbiji kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho na timu yao ya TP Mazembe watawasili kesho- Juni 4 mwaka huu saa 8 mchana.
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za hapa wakati nyumbani itakuwa ni saa 5 usiku.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Marrakech, Morocco