Thursday, July 4, 2013

GIGGS NAYE AWA KOCHA MCHEZAJI SAFU YA BENCH LA UFUNDI.

KLABU ya Manchester United imemtangaza kiungo wake mkongwe Ryan Giggs kuwa kocha mchezaji wa klabu hiyo. Giggs mwenye umri wa miaka 39, aliongeza mkataba wa mwaka mmoja Machi mwaka huu na sasa ataunganisha na majukumu yake mapya yA Kocha mchezaji wa kikosi cha kwanza cha United. Katika taarifa yake Moyes amesema amefurahishwa na Giggs kuikubali nafasi hiyo ya kuwa mchezaji na pia kocha na uzoefu wake wakipindi kirefu utasaidia kuifanya United kuendeleza ubora wake. Giggs ambaye ni raia wa Wales alianza kuchomoza katika timu ya wakubwa ya United mwaka 1991 na kufanikiwa kushinda mataji 13 ya Ligi Kuu nchini Uingereza, manne ya Kombe la FA na medali mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
RYAN GIGGS NA MAN U
-UMRI: 39
-MECHI: 941
-MAGOLI: 168
-MATAJI YA LIGI: 13
-FA CUP: 4
-LIGI CUP: 4
-UEFA CHAMPIONZ LIGI: 2

HISPAIN BADO NAMBARI MOJA DUNIANI VIWANGO VYA FIFA

LICHA wa kutandikwa na Brazil katika  Michuano ya Kombe la Mabara hatua ya fainali Mabingwa wa Dunia Spain bado wameendelea kukamata Nambari moja katika Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotoka leo huku Brazil wakipanda Nafasi 13 na kushika Nafasi ya 9 lakini England  imeporomoka Nafasi 6 hadi kufikia Namba 15 na Tanzania imeshuka Nafasi 12 na sasa ipo ya 121.
Ivory Coast ndiyo Nchi ambayo iko juu kupita zote Afrika na inakamata Nafasi ya 13.
Brazil, ambao Jumapili iliyopita walitwaa Kombe la Mabara, wamerudi 10 Bora na sasa wapo Nafasi ya 9.
Listi nyingine itatolewa Agosti 8.
20 BORA:
Spain
Germany
Colombia (Imepanda Nafasi 4)
Argentina (Imeshuka 1)
5 Holland
Italy (Imepanda 2)
Portugal (Imeshuka 1)
Croatia (Imeshuka 4)
9 Brazil (Imepanda 13)
10 Belgium (Imepanda 2)
11 Greece (Imepanda 5)
12 Uruguay (Imepanda 7)
13 Ivory Coast
14Bosnia-Herzegovina (Imepanda 1)
15 England (Imeshuka 6)
16Switzerland (Imeshuka 2)
17 Russia (Imeshuka 6)
18 Ecuador(Imeshuka 8)
19 Peru (Imepanda 11)
20 Mexico (Imeshuka 3).

WACHINA WAKABIDHI UWANJA WA TAIFA KWA SERIKALI.

UWANJA_WA_TAIFA_DARSerikali ya Tanzania hatimaye imekabidhi Uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam na wachina ikiwa ni awamu ya Kwanza.
Makabidhiano hayo ya Uwanja huo uliochukua Miaka 7 kujengwa yalifanyika Jana kwa kutia saini na kubadilishana Vyeti kati ya Balozi wa China Nchini Tanzania, Li Youqing, na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Mkinga.
Akizungumza, Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella Mukangara, aliishukuru China kwa msaada wao mkubwa wa Fedha na Ujenzi.
Pia, Waziri Mukangara, alisifu Usimamizi wa China wa Uwanja huo tangu ujenzi ulipokamilika na tangu Uwanja huo ulipofunguliwa rasmi hapo Tarehe 25 Februari 2009 na Rais wa zamani wa China, Hu Jintao, na Rais Jakaya Kikwete.
Uwanja wa Taifa, unaochukua Washabiki 60,000 wote wakiwa Vitini, umegharimu Shilingi Bilioni 56 na kati ya hizo China ilitoa Bilioni 33.4 na Tanzania ilitoa Fedha zilizobaki.
Uwanja huu ni wa kisasa na upo katika Viwango vinavyokubalika na FIFA na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki.
Serikali imedokeza kuwa hivi sasa wapo kwenye mazungumzo ya kutafuta Fedha ili kugharamia Ujenzi wa Awamu ya Pili na inatarajiwa Serikali ya China itahusishwa na pia Mkandarasi aliejenga Awamu ya Kwanaza, Beijing Construction Engineering Company Limited, ndio watashughulikia Awamu hii.
Baada ya kukamilika kwa Ujenzi wa Awamu ya Pili, Tanzania itakuwa iko tayari kuwa Mwenyeji wa Mashindano makubwa ya Michezo ya kila aina.

CHELSEA YAFIKIA MAKUBALIANO NA MARCO VAN GINKEL WA VITESSE FC YA UHOLANZI".

WAKALI wa Darajani Club ya soka ya Chelsea imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa klabu ya Vitesse Arnhem ya Uholanzi, Marco van Ginkel. Kiungo huyo mwenye miaka 20 ambaye ametokea katika shule ya watoto ya Vitesse kabla ya kupata namba katika kikosi cha kwanza April mwaka 2010 atajiunga na Chelsea baada ya kukamilisha taratibu za vipimo vya afya. Van Ginkel amekuwa akicheza katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 ya Uholanzi na mara moja ameshaitwa katika kikosi cha timu ya wakubwa akiingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Ujerumani Novemba mwaka jana. Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na meneja mpya wa Chelsea Jose Mourinho kufuatia kusajiliwa kwa mshambuliaji Andre Schuerrle ktoka Leverrkusen mwezi uliopita.

YONDAN AWA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU TZ 2012-2013

INJINI ya Yanga Sc beki Kevin Patrick Yondan amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 na kuzawadiwa kitita cha Sh. Milioni 5. Hata hivyo, katika hafla ya kutoa zawadi za washindi wa Ligi Kuu msimu uliopita kutoa wadhamini, Vodacom Tanzania zilizofanyika katika hoteli ya Double Tree, Dar es Salaam jana usiku, Yondan hakuwepo na tuzo yake alipokelewa na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, kutoka kwa mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara. Yondan ambaye alikuwa katika msimu wake wa kwanza Yanga SC, yuko kwenye kambi ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo dhidi ya Uganda Julai 13, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kipa chipukizi wa Tanzania Prisons FC ya Mbeya, David Burhan alishinda tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu na kupewa Sh. Milioni 5, wakati mfungaji bora, Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast wa Azam FC alipewa Milioni 5 pia na Fully Maganga wa JKT Mgambo alipewa tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu na kuzawadiwa Milioni 5. Kocha mpya wa Simba, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ ameshinda tuzo ya kocha bora kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa na Kagera Sugar msimu uliopita na kuzawadiwa Milioni 7.5 sawa na refa bora, Simon Mbelwa. Yanga SC pamoja na kuzawadiwa Sh. Milioni 70 za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, waliongezewa Milioni 15 kwa kuwa timu yenye nidhamu zaidi kwenye ligi hiyo msimu uliopita, hivyo kuondoka na jumla ya kiasi cha Sh. Milioni 85. Azam FC washindi wa pili kwa msimu wa pili mfululizo, walizawadiwa Sh. Milioni 35, Simba SC washindi wa tatu Milioni 25 na Kagera Sugar washindi wa nne walipewa Milioni 20. Kwa upande wa zawadi za wachezaji wa timu za vijana za klabu za Ligi Kuu, Hamisi Saleh (JKT Ojoro), Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Chande Magoja (Mgambo JKT), Tonny Kavishe (Mgambo JKT) na Rajab Zahir (Mtibwa Sugar), wote wamezawadiwa Sh. Milioni 1 kila mmoja. Zawadi za wachezaji wa timu za vijana, walizozawadiwa kwa kuzichezea mechi nyingi timu zao za wakubwa katika Ligi Kuu, zimetoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Rajab Zahir amesaini Yanga SC na tayari amejiunga nayo.

Wednesday, July 3, 2013

USAJILI WAPAMBA MOTO BARANI ULAYA

Stoke City wamemsaini Beki wa Kimataifa wa Timu ya Spain U-21 Marc Muniesa anaecheza Barcelona kwa Uhamisho wa bure.
Muniesa, Miaka 21, ni mmoja wa Wachezaji wa Spain ambayo ilitwaa Ubingwa wa EURO 2013 kwa U-21 hivi karibuni na anajiunga na Stoke kwa Mkataba wa Miaka minne.
Huyu ni Mchezaji wa pili kuchukuliwa na Meneja mpya wa Stoke, Mark Hughes, baada ya Wiki iliyopita kumsaini Erik Pieters kutoka PSV Eindhoven.
SWANSEA YAKUBALIANA NA LIVERPOOL KUHUSU JONJO
Swansea City imeafikiana na Liverpool Ada ya Pauni Milioni 6 ya kumhamisha Kiungo Jonjo Shelvey na Mchezaji huyo sasa atakutana na Swansea ili kukamilisha makubaliano ya Maslahi yake binafsi.
Jonjo Shelvey, Miaka 21, alisainiwa na Liverpool kutoka Charlton Athletics kwa Dau la Pauni 1.7 Miaka mitatu iliyopita lakini akiwa Anfield kupata namba kwake kumekuwa nadra na Meneja Brendan Rodgers amemruhusu kutafuta Klabu nyingine.
Shelvey aliichezea England kwa mara ya kwanza Novemba Mwaka jana ilipofungwa na Sweden na pia amecheza Mechi 17 za Ligi huko Anfield Msimu uliopita.
Jana Swansea ilitangaza kuwasaini Wachezaji watatu wengine ambao ni Alejandro Pozuelo, Miaka 21, kutoka Real Betis ya Spain, Kipa wa Miaka 17, Gregor Zabret kutoka Klabu ya Slovenia NK Domzale na Alex Gogic, Kiungo wa Miaka 19 kutoka Klabu ya Greece, Olympiakos.
ARSENAL_NA_MCHEZA_RAGAARSENAL YAMCHUKUA MCHEZA RAGA!
Katika azma yao ya kukiimarisha Kikosi chao kuwa na nguvu na Misuli inayostahili kwa ajili ya Msimu mpya, Klabu ya Arsenal imemuajiri Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Ireland wa Mchezo wa Raga, Jerry Flannery, kuwa Kocha wao mpya wa kujenga nguvu, musili na stamina kwa Wachezaji wao.
Flannery, Miaka 34, alistaafu mapema kucheza Raga baada ya kuumia Misuli za Mguu.
MOURINHO AZUNGUMZA NA MARCO VAN GINKEL
Chelsea imefanya mazungumzo na Kiungo wa Vitesse Arnhem, Marco van Ginkel, ili ahamie Stamford Bridge.
Van Ginkel, Miaka 20, ameshakutana na Jose Mourinho na Alhamisi ataongea na Klabu yake ya Uholanzi ili apate baraka za Uhamisho.
Marco van Ginkel alijiunga na Vitesse Arnhem akiwa na Miaka 7 tu na kupanda kwenye Vyuo vya Klabu hiyo hadi Aprili 2010 alipocheza Timu ya Kwanza kwa mara ya kwanza.
Van Ginkel anathaminiwa kuwa na Dau la Pauni Milioni 8 na Mkataba wake na Klabu yake unamalizika Juni 2015.
Ikiwa Uhamisho huu utakamilika, huu utakuwa ni usajili wa pili kwa Jose Mourinho baada ya Wiki iliyopita kumnasa Mchezaji wa Kimataifa wa Germany, Andre Schurrle, kutoka Klabu ya Bundesliga, Bayer Leverkusen.

MESSI ASEMA BARCELONA ILIFANYA SAHIHI KUMNASA NEYMAR

Mshambuliaji nyota duniani wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi anaamini kuwa klabu hiyo ilifanya jambo sahihi kumsajili Neymar katika kampeni yao ya kutetea taji La Liga na kufanya vyema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Neymar mwenye umri wa miaka 21 alikamilisha usajili wake uliogharimu kiasi cha euro milioni 57 akitokea Santos Juni mwaka huu ingawa hatahivyo wakosoaji wanadai Barcelona ilifanya makosa kutumia fedha nyingi kumsajili nyota huyo ambaye hajawahi kucheza Ulaya. 
Lakini baada ya kufunga mabao manne katika michuano ya Kombe la Shirikisho ilikiwemo bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa wa Dunia Hispania wakooaji hao watakuwa wameshapata majibu ya maswali yao na Messi anategemea nyota huyo kufanya makubwa zaidi atakapokuwa Barcelona. Messi amesema anategemea Neymar ataleta mchango mkubwa katika klabu hiyo kama akiendelea kucheza katika kiwango cha juu kama ilivyo kwa timu yake ya taifa na Santos. Barcelona ilifanikiwa kunyakuwa taji la La Liga msimu uliopita lakini walipata kipigo kikubwa kutoka Bayern Munich kwenye mechi za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo waling’olewa kwa kufungw ajumla ya mabao 7-0 katika mechi mbili walizocheza.