Sunday, July 7, 2013

BOLT ATUMA SALAMU KWA WAPINZANI WAKE BAADA YA KUIBUKA NA USHINDI.

Usain Bolt Mwanariadha nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica,ametuma salamu kwa wapinzani wake baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi katika mbio za mita 200 za Diamond League zilizofanyika jijini Paris kwa kutumia muda wa sekunde 19.73 ukiwa ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Bolt ambaye anashikilia rekodi ya dunia katika mbio hizo alifabnikiwa mbio kirahisi na kuuzidi muda wa haraka zaidi uliowekwa kwa mwaka huu na Tyson Gay wa Marekani mwezi mmoja kabla ya mashindano ya riadha ya dunia yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi. Akihojiwa mara baada yam bio hizo Bolt amesema anajisikia vyema kwa kushinda mbio hizo lakini bado bado ana kazi ya kufanya kuhakikisha anakuwa katika kiwango chake ifikapo michuano ya dunia. Nafasi ya pili katika mbio hizo ilikwenda kwa Warren Weir wa Jamaica aliyetumia muda wa sekunde 19.92 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Christophe Lemaitre wa Ufaransa aliyetumia muda wa sekunde 20.07.

Thursday, July 4, 2013

ROONEY ATAKIWA KUWA SILISHA BARUA KWA MAN U

MSHAMBULIAJI Wayne Rooney atatakiwa kuwasilisha barua ya maandishi ya kuomba kuondoka ikiwa anataka kuachana na  Manchester United.
Mpachika mabao huyo wa Old Trafford, alirejea mazoezini jana huku mustakabali wake ukiwa bado haueleweki. Imefahamika hakuwa na Mkutano mahsusi na kocha mpya David Moyes juu ya suala lake. 
Hilo linaweza kutokea katika kituo cha mazoezi cha klabu, Carrington leo. Wawili hao walizungumza jana, lakini si kwa muda mrefu na msimamo wa United kwake bado haujabadilika.

Hajielewi: Mustakabali wa Wayne Rooney bao haueleweki licha ya jana kurejea mazoezini
Wamesema mshambuliaji huyo wa England hauzwi. Kuhusu tetesi za wapinzani wao katika Ligi Kuu, Arsenal kutaka rasmi kumsajili tangu wiki iliyopita, United bado haijawasiliana na yoyote anayemtaka Rooney.
Sakata hili linaweza kugeuka tu iwapo mshambuliaji mwenyewe ataamua kulazimisha kuondoka. BIN ZUBEIRY iliandika mwishoni mwa msimu uliopita kwamba, Rooney aliomba kuondoka kwa kocha aliyestaafu, Sir Alex Ferguson.
Ombi la kuondoka litamaanisha Rooney hatadai chochote katika Mkataba wake wa miaka miwili uliobakia ambao alikuwa analipwa Pauni 250,000 kwa wiki.

Moyes, bado anataka kumuongeza katika benchi lake la ufundi, beki wa zamani wa United, Phil Neville na ni matumaini Rooney atakubali kubaki msimu ujao kufanya na kazi na kocha wa zamani wa Everton, aliyeinua kipaji chake Goodison Park.
Huku Moyes akitarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari kwa mara ya kwanza kesho, ufafanuzi utakuja muda si mrefu.

Harudi: Angalau bado, kwa Cristiano Ronaldo
Wakati huo huo, mchezaji mwenzake wa zamani Rooney, Mreno Cristiano Ronaldo ameendelea kuweka wazi juu mapenzi yake na United. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid  amesema jana kwamba anataka kurudi Ligi Kuu, lakini hakusema lini.
"Nalikosa kweli soka la England. Kwangu ilikuwa moja ya miaka bora katika maisha yangu ya soka wakati nipo huko Manchester United. Ni klabu ambayo bado ipo moyoni mwangu. naikosa kweli kweli. Lakini kwa sasa maisha yangu yapo Hispania. Nafurahia kucheza huko pia. Mustakabali hatuwezi kuujua,"alisema Ronaldo.

ISCO ASEMA LENGO KUU NI KUISAIDIA MADRID KUTWAA UEFA

Baada ya kusajiliwa katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi na club ya Real Madrid Isco ametanabaisha na kusama kuwa lengo lake kubwa ni kukisaidia kikosi cha timu hiyo kinachonolewa na kocha Carlo Ancelotti kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Kocha aliyeoondoka Jose Mourinho ameinoa klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu na kuisadia klabu hiyo kufika nusu fainali ya ligi hiyo mara tatu lakini bado wamekuwa na kiu ya muda mrefu ya kulisubiria taji lao 10 katika michuano hiyo. Akijiunga na Madrid kwa mkataba wa miaka mitano kutokea Malaga, Isco sasa ana malengo ya kuiwezesha klabu hiyo kuendeleza historia yake kwa kunyakuwa taji hilo mapema iwezekanavyo. Akihojiwa katika utambulisho rasmi, Isco amesema watu wote wanahusiana na klabu hiyo wamekuwa na kiu ya taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na ni mategemeo yake kwamba msimu unaokuja taji hilo litatua Santiago Bernabeu.

GIGGS NAYE AWA KOCHA MCHEZAJI SAFU YA BENCH LA UFUNDI.

KLABU ya Manchester United imemtangaza kiungo wake mkongwe Ryan Giggs kuwa kocha mchezaji wa klabu hiyo. Giggs mwenye umri wa miaka 39, aliongeza mkataba wa mwaka mmoja Machi mwaka huu na sasa ataunganisha na majukumu yake mapya yA Kocha mchezaji wa kikosi cha kwanza cha United. Katika taarifa yake Moyes amesema amefurahishwa na Giggs kuikubali nafasi hiyo ya kuwa mchezaji na pia kocha na uzoefu wake wakipindi kirefu utasaidia kuifanya United kuendeleza ubora wake. Giggs ambaye ni raia wa Wales alianza kuchomoza katika timu ya wakubwa ya United mwaka 1991 na kufanikiwa kushinda mataji 13 ya Ligi Kuu nchini Uingereza, manne ya Kombe la FA na medali mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
RYAN GIGGS NA MAN U
-UMRI: 39
-MECHI: 941
-MAGOLI: 168
-MATAJI YA LIGI: 13
-FA CUP: 4
-LIGI CUP: 4
-UEFA CHAMPIONZ LIGI: 2

HISPAIN BADO NAMBARI MOJA DUNIANI VIWANGO VYA FIFA

LICHA wa kutandikwa na Brazil katika  Michuano ya Kombe la Mabara hatua ya fainali Mabingwa wa Dunia Spain bado wameendelea kukamata Nambari moja katika Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotoka leo huku Brazil wakipanda Nafasi 13 na kushika Nafasi ya 9 lakini England  imeporomoka Nafasi 6 hadi kufikia Namba 15 na Tanzania imeshuka Nafasi 12 na sasa ipo ya 121.
Ivory Coast ndiyo Nchi ambayo iko juu kupita zote Afrika na inakamata Nafasi ya 13.
Brazil, ambao Jumapili iliyopita walitwaa Kombe la Mabara, wamerudi 10 Bora na sasa wapo Nafasi ya 9.
Listi nyingine itatolewa Agosti 8.
20 BORA:
Spain
Germany
Colombia (Imepanda Nafasi 4)
Argentina (Imeshuka 1)
5 Holland
Italy (Imepanda 2)
Portugal (Imeshuka 1)
Croatia (Imeshuka 4)
9 Brazil (Imepanda 13)
10 Belgium (Imepanda 2)
11 Greece (Imepanda 5)
12 Uruguay (Imepanda 7)
13 Ivory Coast
14Bosnia-Herzegovina (Imepanda 1)
15 England (Imeshuka 6)
16Switzerland (Imeshuka 2)
17 Russia (Imeshuka 6)
18 Ecuador(Imeshuka 8)
19 Peru (Imepanda 11)
20 Mexico (Imeshuka 3).

WACHINA WAKABIDHI UWANJA WA TAIFA KWA SERIKALI.

UWANJA_WA_TAIFA_DARSerikali ya Tanzania hatimaye imekabidhi Uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam na wachina ikiwa ni awamu ya Kwanza.
Makabidhiano hayo ya Uwanja huo uliochukua Miaka 7 kujengwa yalifanyika Jana kwa kutia saini na kubadilishana Vyeti kati ya Balozi wa China Nchini Tanzania, Li Youqing, na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Mkinga.
Akizungumza, Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella Mukangara, aliishukuru China kwa msaada wao mkubwa wa Fedha na Ujenzi.
Pia, Waziri Mukangara, alisifu Usimamizi wa China wa Uwanja huo tangu ujenzi ulipokamilika na tangu Uwanja huo ulipofunguliwa rasmi hapo Tarehe 25 Februari 2009 na Rais wa zamani wa China, Hu Jintao, na Rais Jakaya Kikwete.
Uwanja wa Taifa, unaochukua Washabiki 60,000 wote wakiwa Vitini, umegharimu Shilingi Bilioni 56 na kati ya hizo China ilitoa Bilioni 33.4 na Tanzania ilitoa Fedha zilizobaki.
Uwanja huu ni wa kisasa na upo katika Viwango vinavyokubalika na FIFA na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki.
Serikali imedokeza kuwa hivi sasa wapo kwenye mazungumzo ya kutafuta Fedha ili kugharamia Ujenzi wa Awamu ya Pili na inatarajiwa Serikali ya China itahusishwa na pia Mkandarasi aliejenga Awamu ya Kwanaza, Beijing Construction Engineering Company Limited, ndio watashughulikia Awamu hii.
Baada ya kukamilika kwa Ujenzi wa Awamu ya Pili, Tanzania itakuwa iko tayari kuwa Mwenyeji wa Mashindano makubwa ya Michezo ya kila aina.

CHELSEA YAFIKIA MAKUBALIANO NA MARCO VAN GINKEL WA VITESSE FC YA UHOLANZI".

WAKALI wa Darajani Club ya soka ya Chelsea imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa klabu ya Vitesse Arnhem ya Uholanzi, Marco van Ginkel. Kiungo huyo mwenye miaka 20 ambaye ametokea katika shule ya watoto ya Vitesse kabla ya kupata namba katika kikosi cha kwanza April mwaka 2010 atajiunga na Chelsea baada ya kukamilisha taratibu za vipimo vya afya. Van Ginkel amekuwa akicheza katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 ya Uholanzi na mara moja ameshaitwa katika kikosi cha timu ya wakubwa akiingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Ujerumani Novemba mwaka jana. Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na meneja mpya wa Chelsea Jose Mourinho kufuatia kusajiliwa kwa mshambuliaji Andre Schuerrle ktoka Leverrkusen mwezi uliopita.