Thursday, May 1, 2014
TFF YATEUA WAKILI KUCHUNGUZA USAJILI WA DOMAYO AZAM FC .
KatiKa harakati za usajili wa
mwanzo
tukio lililotokea jana (Aprili 30 mwaka huu) kwenye kambi ya timu ya Taifa
(Taifa Stars) iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya likihusisha usajili wa baadhi ya
timu, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemteua Wakili
Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo mzima wa tukio hilo.

Taarifa ya TFF ya leo asubuhi imesema kwamba, baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua.
TFF imesema katika taarifa
yake inatoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata kanuni
na taratibu katika utendaji wao.
Viongozi wa Azam FC jana walikwenda kwenye kambi ya Taifa Stars kukamilisha taratibu za usajili na kiungo Frank Domayo, aliyemaliza Mkataba wake Yanga SC.
Baada ya kufanikiwa kumsainisha Mkataba wa miaka miwili, wasimamizi wa kambi waliwaitia Polisi viongozi wa Azam FC ambao hata hivyo baadaye waliachiwa. Lakini inadaiwa fomu za usajili zilichanwa.
Azam si klabu ya kwanza kusajili mchezaji katika kambi ya timu ya taifa, kwani vigogo wa s
Mwaka jana Simba SC walisaini Mkataba mpya na kiungo wao, Amri Kiemba akiwa katika kambi ya Taifa Stars, hoteli ya Tansoma mjini Dar es Salaam.
Yanga SC iliwasajili Domayo kutoka JKT Ruvu, Kevin Yondan kutoka Simba SC wote wakiwa katika kambi ya Taifa Stars Dar es Salaam miaka miwili iliyopita.
Wednesday, April 30, 2014
MALAWI KUTUA NCHINI KESHO MEI 1 MWAKA HUU.

Flames yenye msafara wa 31 utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu cha Malawi (FAM) utaingia Mbeya kwa usafiri wa barabara. Wachezaji katika msafara huo ni 20.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha
mpya, Mart Nooij tayari ipo jijini Mbeya kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Zimbabwe
itakayochezwa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.
KATIBU MKUU WA FIFA AWASILI KESHO DAR

Valcke
ambaye atafuatana na maofisa wengine saba wa FIFA baadaye kesho hiyo
hiyo (Mei 1 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari.
Mkutano huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi kwenye hoteli ya Double Tree
by Hilton iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam.
Tuesday, April 29, 2014
KAVUMBAGU ATUA AZAM KWA MKATABA WA MWAKA MMOJA.
Mshambuliaji Didier
Kavumbagu mchana wa leo amesaini mkataba
wa mwaka mmoja na mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu
ya Azam fc.

Maganga amesema Kavumbagu
tumem
alizana nae na amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja, hivyo basi tutakuwa
nae msimu ujao kwenye kampeni ya kutetea ubingwa wetu pamoja na michuano
ya klabu bingwa ya Afrika.
Kavumbagu ambae ni Mshambuliaji mahiri na nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi ameamua kumwaga wino
Azam baada ya Uongozi wa Yanga kusuasua kumpa mkataba mwingine baada ya
ule wa miaka miwili kumalizika.
Maganga amesema kuwa lengo la kuanza usaji mapema ni kuweka mipango mathubuti katika kuhakikisha azam fc inakuwa timu bora na kuweza kukiweka imara kikosi hicho katika msimu ujao pamoja na ligi ya mabingwa barani africa
MALAWI KUWASILI MEI 1 KUIVAA STARS
Timu
ya Taifa ya Malawi (Flames) inatarajiwa kuwasili nchini Mei 1 mwaka huu
kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Mei 4
mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha
mpya, Mart Nooij tayari ipo jijini Mbeya kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Zimbabwe
itakayochezwa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.
LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA KUTIMUA VUMBI MEI 10
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu
wa 2013/2014 itakayochezwa kwa mkondo mmoja inaanza kutimua vumbi Mei 10 mwaka
huu katika vituo vitatu vya timu tisa kila kimoja.
Tmu itakayoongoza katika kila kituo
cha ligi hiyo itakayomalizika Juni 2 mwaka huu ndiyo itakayopata tiketi ya
kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu ujao wa 2014/2015. Vituo hivyo ni
Mbeya, Morogoro na Shinyanga.
Kituo cha Morogoro ambapo mechi
zitachezwa Uwanja wa Jamhuri kitakuwa na timu za Abajalo FC ya Dar es Salaam,
African Sports (Tanga), Bulyanhulu FC (Shinyanga), Kariakoo SC (Lindi), Kiluvya
United (Pwani), Mji Mkuu FC (Dodoma) Mshikamano FC (Dar es Salaam), Navy FC
(Dar es Salaam) na Pachoto FC (Mtwara).
Uwanja wa Sokoine ndiyo utakaotumika
katika kituo cha Mbeya chenye timu za AFC ya Arusha, Magereza FC (Iringa),
Mpanda United SC (Katavi), Njombe Mji FC (Njombe), Panone FC (Kilimanjaro),
Tanzanite SC (Manyara), Town Small Boys (Ruvuma), Ujenzi (Rukwa) na Volcano FC
(Morogoro).
Timu za Eleven Stars ya Kagera, Geita
Veterans (Geita), JKT Rwamkoma FC (Mara), Mbao FC (Mwanza), Milambo SC
(Tabora), Mvuvumwa FC (Kigoma), Simiyu United (Simiyu), Singida United
(Singida) na Wenda FC (Mbeya) zitacheza katika kituo cha Shinyanga kwenye
Uwanja wa Kambarage.
Orodha ya usajili wa wachezaji wa
timu zote kwa ajili ya RCL imetumwa kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na
klabu zote za RCL, FDL na Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa ajili ya kipindi cha
pingamizi ambacho kinamalizika Mei 4 mwaka huu.
Hata hivyo, katika usajili
uliowasilishwa na baadhi ya klabu imebainika kuwa kuna wachezaji walioshiriki
VPL, FDL na wale U20 za VPL waliocheza ligi msimu wa 2013/2014.
Kiongozi yeyote atakayebainika katika
udanganyifu kwenye usajili huo, awe wa klabu au chama cha mpira wa miguu cha
mkoa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni ikiwemo kufikishwa katika vyombo
vya kimaadili vya TFF kwa hatua zaidi.
Ligi ya Mabingwa haina mdhamini, hivyo timu shiriki zitajitegemea kwa kila kitu, na zinakumbushwa kuwahi vituoni.
Ligi ya Mabingwa haina mdhamini, hivyo timu shiriki zitajitegemea kwa kila kitu, na zinakumbushwa kuwahi vituoni.
Subscribe to:
Posts (Atom)