Tuesday, September 23, 2014

KIONGERA NJE KUIKOSA YANGA KATIKA MTANANGE WATANI WA JADI OCT 12 MWAKA HUU.

MSHAMBULIAJI Mahiri Wa Simba Mkenya, Paul Raphael Kiongera yupo katika hatari ya kukosa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wapinzani wa jadi, Yanga SC Oktoba 12, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hiyo inafuatia kuumia katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Jumapili Uwanja wa Taifa, Simba SC ikilazimishwa sare ya 2-2 na Coastal Union, licha ya kuongoza kwa 2-0 hadi mapumziko.

Kiongera alitokea benchi dakika ya 67, lakini dakika mbili kabla ya mpira kumalizika  alimpisha Amri Kiemba baada ya kuumia, kufuatia kugongana na kipa wa Coastal Union, Shaaban Kado.

Kiongera ameumia goti ambapo leo alikuwa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo, ila inasemekana mchezaji huyo ana maumivu sugu ya goti hilo baada ya kuumia awali kwao, Kenya.
Taarifa za awali zinasema Kiongera anaweza kuwa nje ya Uwanja kwa muda wa kati ya wiki sita hadi miezi miwili kabla ya kuanza mazoezi mepesi, maana yake hataweza kucheza Oktoba 12 pambano la watani.

Baada ya taarifa hiyo kuna hali ya wasiwasi ndani ya Simba SC kwamba huenda wameingia mkenge’ kumsajili Mkenya huyo bila kumfanyia vipimo vya afya, kufuatia habari kwamba ana maumivu sugu ya goti.

KOCHA MWAMWAJA ASEMA TZ PRISON ITAENDELEZA VIPIGO TU VPL

Baada ya Kuifumua Tanzaania Prison Kocha Mkuu wa Prisons ya Mbeya, David Mwamwaja amesema kuwa mpango mkubwa walionao ni kuendeleza vipigo kwa lengo la kujiimarisha kileleni.

Mwamwaja Kocha mzoefu aliyewahi kuifundisha Simba, amesema ushindi wao wa kwanza wa ligi katika mechi ya kwanza, umewapa motisha na nguvu za kutaka kuendelea kujinyakulia pointi tatu.

Prisons iliitandika Ruvu Shooting kwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandizi, Pwani.

Mwamwaja amesema kuwa Mechi na Ruvu shooting ilikuwa ngumu lakini tumefurahia kushinda ambapo amesema lengo kuu Tunataka kushinda zaidi na tumeanza kucheza mechi kadhaa za kirafiki kujiimarisha.


WAGOSI WA KAYA COASTAL UNIONI WAFURAHIA MAJERUHI WA MBEYA CITY 3 NJE.

Kuelekea Mtanange wa Juma mosi Timu ya mbeya city itawakosa baadhi ya wachezaji wake watatu baada ya kuumia katika mechi ya jumamosi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu  iliyomalizika kwa suluhu ya bila kufungana, uwanja wa Sokoine, Mbeya, na watakaa nje ya uwanja kwa wiki mbili.
Akizungumza na Mkali wa dimba tz.blogspot Afisa habari wa mbeya city Dismas Ten amesema kuwa baada ya mechi iliyopita, wachezaji watano walipata majeruhi, lakini wawili kati yao watarejea uwanjani jumamosi ya septemba 27 kuchuana na Coastal Union.
Wachezaji hao ni Kabanda, Alex Seth na Eric Mawala, hawataweza kucheza kabisa siku ya jumamosi kwasababu watakaa nje kwa majuma mawili, kwa mujibu wa daktari wa timu
Dismas aliongeza kuwa maandalizi ya mechi ya pili nyumbani yanakwenda vizuri na wachezaji wana morali ya kutafuta ushindi na kuendeleza rekodi yao ya msimu uliopita ambapo walimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na mabingwa Azam fc.
sanjari na hayo Dismas amesema kuwa Hali ya kambi ni nzuri, tunajiandaa vizuri na tunaamini tutaibuka na ushindi. Tulicheza mpira mkubwa sana dhidi ya JKT Ruvu.

Monday, September 15, 2014

MOURINHO ASEMA AMTUPIA LAWAMA CRISIANO RONALDO

KOCHA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amemtupia lawama Cristiano Ronaldo kwa kushindwa kwake kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati akiinoa Real Madrid. 
Mourinho alijiunga na na Madrid mwaka 2010 baada ya kuisaidia Inter Milan kunyakuw ataji hilo lakini katika msimu mitatu aliyokuwa Santiago bernabeu alishindwa kabisa kupata mafanikio barani Ulaya akiwa ameambulia kuingoza timu hiyo mpaka hatua ya nusu fainali katika kipindi chote hicho. 

Mara ya mwisho Mourinho kukaribia kutinga fainali ya michuano ya hiyo ilikuwa msimu wa mwaka 2011-2012 wakati walipokwenda katika hatua ya changamoto ya mikwaju ya penati baada ya muda wa nyongeza katika nusu fainali ya pili lakini walitolewa baada ya nyota wake akiwemo Ronaldo, Kaka na Sergio Ramos kukosa penati muhimu. 

Akihojiwa Mourinho ametamba kuwa kushinda taji la michuano hiyo mara mbili kama imefanya kazi yake hiyo kuwa ya kipekee. 

Mourinho amesema amekuwepo katika nusu fainali kadhaa na baadhi imekuwa ngumu kukubali kushindwa kama goli walilofungwa na Liverpool wakati akiwa na Chelsea mwaka 2005 pamoja matuta ya mwaka 2011 wakati mchezaji wao tegemeo Ronaldo alipokosa penati ya kwanza.

WEKUNDU WA MSIMBAZI WAREJEA ZANZIBAR KUWEKA KAMBI KWA MARA YA PILI.

Klub ya simba wekundu wa Msimbazi , Simba SC wamerejea tena Visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya ligi kuu soka  Tanzania bara inayotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu.
20140913_160508Simba chini ya kocha Mzambia Patrick Phiri wataanza kampeni za kusaka ubingwa walioukosa kwa misimu miwili dhidi ya Wagosi wa ya, Coastal Union, septemba 21 mwaka huu uwanja wa Taifa , Dar es salaam.
Hii itakuwa mara ya pili Simba kujificha Zanzibar kwa sabababu ilikuwa huko kabla ya kuja Dar es salaam kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, septemba 6 mwaka huu uwanja wa Taifa na kuitandika 3-0.
Ijumaa ya wiki iliyopita, Simba ilicheza mechi ya pili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya URA ya Uganda na kulala bao 1-0.
jumamosi ya wiki iliyopita, Simba ilisafiri kwenda Mtwara ambapo ilicheza mechi ya kirafiki na Ndanda fc katika uwanja wa Nangwanda Sijaona na kutoka suluhu pacha ya bila kufungana.
Baada ya mechi hiyo, jana wachezaji walipewa mapumzikio, na leo jumatatu wanaanza mazoezi kabla ya kuelekea Zanzibar.
Simba wamekuwa wakiijenga timu upya chini ya kocha Phiri na usajili wao unawafanya wapinzani wawe na wasiwasi.
Wachezaji wa kigeni waliopo Simba wameonekana kuwa na ubora wa kutosha, hivyo kujenga imani kwa mashabiki wao.
Warundi, Amissi Tambwe, Pierre Kwizera, Mkenya, Paul Kiongera na Waganda Joseph Owino na Emmanuel Okwi wameonekana kuwa na msaada mkubwa kwa Simba.
Pia wapo wazawa waliosajiliwa kama, kipa Hussein Sharrif, Shaaban Kisiga, Elius Maguli,Joram Mgeveke, Tshabalala, na wengineo.
Wachezaji hawa wameonakana kuelewana na kucheza mpira mzuri kama walivyoonekana kwenye mechi dhidi ya Gor Mahia na URA.

MINZIRO ASEMA TUNAWAKATI MGUMU LIGI KUU LAKINI TUTAPAMBANA TU" WACHEZAJI 7 NJE

Maafande wa Jkt Ruvu kutoka kibaha mkoani pwani kushuka kitaanza Ligi Kuu Bara bila ya wanandinga wake saba wa kikosi cha kwanza.
Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Felix Minziro, amethibitisha kutokuwepo kwa wachezaji hao ambao wamekwenda kushiriki michuano ya Majeshi ya Afrika Mashariki iliyokuwa ikifanyika mjini Zanzibar.
Wachezaji wangu takribani saba wa kikosi cha kwanza, hawapo kwa sasa, hili linanipa wakati mgumu sana.
Minziro amesema ligi inaanza siku ya Jumamosi, uwepo wao una mchango mkubwa katika timu na wako Msumbiji kwa sasa kulitumikia jeshi katika masuala la michezo.

KAMATI YA SHERIA YAPITISHA USAJILI KLAB ZA VPL NA FDL MSIMU 2014

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imepitisha usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza huku wenye kasoro ndogondogo klabu zao zikitakiwa kuziondoa ili waweze kupatia leseni za kucheza ligi msimu huu wa 2014/2015.
Kasoro hizo ni kufikia makubaliano na klabu ambazo wachezaji husika wametoka, kuwafanyia uhamisho (transfer) na kulipa ada za uhamisho. Kamati vilevile ilibaini wachezaji wengi hawakufanyiwa uhamisho kama kanuni za ligi hizo zinavyoelekeza.
Hivyo, klabu ambazo hazitakuwa zimeondoa kasoro hizo kwa wachezaji wao leseni zao zitazuiliwa mpaka watakapokuwa wamekamilisha kila kitu. Ni wachezaji wenye leseni tu ndiyo watakaoruhusiwa kucheza mechi za ligi.

Klabu za African Lyon, African Sports, Ashanti United, Coastal Union, Kiluvya United, Majimaji, Mji Mkuu, Polisi Dodoma, Polisi Morogoro, Red Coast na Stand United ziliwawekea pingamizi wachezaji mbalimbali kwa kutofanyiwa uhamisho.
Kuhusu Ike Bright Obina wa Nigeria aliyewekewa pingamizi na African Lyon dhidi ya Coastal Union, Kamati imezitaka klabu hizo kufikia makubaliano, na zikishindwa mchezaji huyo atabaki African Lyon.

Kamati vilevile ilijadili malalamiko ya Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic dhidi ya klabu hiyo, na kuzipa pande hizo mbili siku 14 kufikia muafaka juu ya malalamiko hayo, na zikishindwa ndipo zirejee tena mbele ya Kamati.
Logarusic aliyewakilishwa na mwanasheria wake Dickson Sanga anailalamikia klabu hiyo kwa kuvunja mkataba kinyume cha taratibu, hivyo kutaka Simba imlipe dola 6,000 kwa kuvunja mkataba, na pia kulipa dola 50,000 ikiwa ni fidia maalumu ya madhara yaliyotokana na uvunjwaji huo.
BONIFACE WAMBURA
KNY KATIBU MKUU
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)