Monday, November 3, 2014

MBEYA CITY YABAMIZWA NA MAFAANDE WA JKT MGAMBO

Timu ya Mbeya City wagonganyundo wa jiji la mbeya ikiwa katika dimba la mkwakwani imepokea kipondo kingine baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Mgambo JKT.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, washindi walipata mabao yote katika kipindi cha kwanza.


Mbeya City wakajitahidi kupata bao katika kipindi cha pili na kuzaa matokeo ya mabao 2-1 katika dakika 90.


SUMATRA MKOA WA MBRYA YASEMA HATAVUMILIA TABIA ZA MADERA KUJAZA MAFUTA WAKATI WA KUBEBA ABIRIA.

MAMLAKA ya usafiri na udhibiti wa nchi kavu na majini (Sumatra) mkoa wa Mbeya imesema kuwa haitavumilia tabia ya baadhi ya watumiaji wa vyombo vya usafiri  kujaza mafuta  wakati vikiwa vimebeba abiria.
Aidha mamlaka hiyo imesisitiza kuwa ikiwa watumiaji hao watabainika kutenda kosa hilo watatozwa faini ya shilingi laki mbili na nusu.
Akizungumza na Highlands fm, Afisa mfawidhi wa Sumatra, Denis Daud amesema vitendo hivyo vinahatarisha usalama wa abiria na kwamba  mamlaka hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa watumiaji hao.

Katika hatua nyingine Daud, amewataka watumiaji hao kujaza mafuta ya kutosha kwenye magari yao ili kuondoa usumbufu kwa abiria pindi magari hayo yanapokata mafuta barabarani.

MAKONDA AKANUSHA KUMPIGA MZEE WARIOBA NA KULAANI VIKALI WALIOANZISHA VURUGU,

Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionesha vitu alivyokwenda navyo kwenye mdahalo huo ambavyo ni katiba ya sasa na katiba pendekezwa kwa ajili ya kutumia kujibu hoja mbalimbali wakati wa mdahalo huo.
M3
Makonda amelaani na kukanusha kuwa hakumpiga Mzee Warioba isipokuwa alikuwa na kazi moja ya kuhakikisha anamsaidia Anold Kayanda mwandishi wa BBC ambaye aliumizwa  katika vurugu hizo na  Mzee Warioba na aliyekuwa mbunge wa bunge maalum la katiba asiyeona Amon Mpanju  wakati wa vurugu zilizotokea katika  mdahalo wa kujadili rasimu ya Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza  jana, ambapo Makonda aliyedaiwa kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji mstaafu Joseph Warioba, amekanusha kumpiga leo katika mkutano wa waandishi wa habari, Dar es Salaam.
Pia Makonda amesema kuwa hawezi kabisa kudiriki kumpiga kwani anamheshimu kama babake mzazi. 
Amesema kuwa hata leo asubuhi amezungumza na warioba kwenye simu kumjulia hali. Warioba naye amekanusha kupigwa na Makonda wala mtu yoyote kwenye vurugu hizo

MWAKIBINGA AONDOKA BODI YA LIGI

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga amemaliza mkataba wake tangu Oktoba 31 mwaka huu.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na TPLB wanamshukuru Mwakibinga kwa mchango wake kwa kipindi ambacho ameitumikia Bodi, na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya huko aendako.

TPLB hivi sasa iko katika mchakato wa kupata Ofisa Mtendaji Mkuu mpya kwa ajili ya kuziba nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mwakibinga baada ya muda wa mkataba wake kumalizika.

KOCHA NOOIJ KUTAJA KIKOSI STARS
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij keshokutwa (Novemba 5 mwaka huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini Novemba 16 mwaka huu.

Nooij atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Swaziland, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Mbabane.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Saturday, November 1, 2014

JUMUIYA YA WAZAZI YA(CCM) MKOA WA DAR YAZINDUA DAFTARI LA WANACHAMA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed amewata viongozi wa jumuia hiyo kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuifanya jumuia hiyo kukua kiuchumi.
Moto huo ameutoa wakati akizindua Daftari la Wanachama wa Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam leo.
Alisema kwa mfano katika shule ya jumuia hiyo ya Boza iliyopo mkoani Tanga kuwa ina ardhi ya kutoka lakini haifanyiwi uzarishaji mali wowote.
Mohamed alipongeza Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha daftari hilo kwani litasaidia kuwatambua wanachama wao kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa hivyo kurahisisha shughuli za kisiasa kwa kutambuana katika chaguzi mbalimbali na shughuli za maendeleo.
Katika hatua nyingine Mohamed alisema wanajumuia wote ya wazazi wanaiunga mkono rasimu ya Katiba mpya iliyopendekezwa na Bunge Maalumu na kuwa wao wanautaka muundo wa serikali mbili kwani ndio utalipeleka mbele Taifa la Tanzania. 
Ametoa mwito kwa wanachama wote wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuwachagua viongozi wao kuanzia ngazi za mashina wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika hivi karibuni.
Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje alisema mpango wa kuanzisha daftari hilo ni moja ya mikakati yao ya kuibadilisha jumuia hiyo kiutendaji badala ya kuegemea katika eneo moja la siasa.

TANZANIA NA BURUNDI ZA SAINI MKATABA WA MIAKA 50 KUSAFIRISHA UMEME.

SERIKALI ya Tanzania na Burundi zimesaini mkataba wa miaka 50 wamakubaliano wa mradi wa pili wa kusafirisha umeme utakaozalishwa kwenye kituo cha Rusumo.
Awali Tanzania, Burundi na Rwanda zilisaini mkataba wa kwanza wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme cha rusumo chenye mega watt 80, kilichopo wilayani Ngara, Mkoani Kagera, mwaka 2013 ambacho kiligharimu takribani dola za kimarekani milioni 340 zilizotolewa na benki ya Dunia.
Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo, alisema mkataba huo umezihusisha nchi mbili ambapo alibainisha kuwa kupitia mradi huo ambao umeanza katika sehemu ya mwisho ya kutekeleza mradi wa kwanza ulioanza mwaka jana yapo baadhi ya maeneo nchini yatapata umeme.

Alisema kupitia mradi huo nchi itaweza kuimarisha grid ya Taifa na kupunguza tatizo la umeme kwenye maeneo mengi nchini.
Waziri Muhongo aliongeza kuwa pamoja na hatua hiyo pia kuitia mradi huo utaajiri wafanyakazi kutoka nchi zote tatu na hata wa mataifa mwengine ambapo alibainisha kuwa kwa sasa katika kituo cha mto rusumo wapo walioajiriwa kutoka nchi husika na miradi hiyo na mataifa mengine.

Kuhusu ujenzi wa mfumo wa usafirishaji umeme alisema kila nchi itajitegemea katika kusafirisha umeme na kubainisha kuwa Tanzania itajenga mfumo huo kuanzia miaka michache ijayo.

Hata hivyo Prof. Muhongo hakubainisha kiasi halisi kitakacho tumika kuendeshea mradi huo wa wamu ya pili

VPL:AZAM FC, YANGA ZAPIGWA KIMOJA, SIMBA YALE YALE.

MATOKEO:
Jumamosi Novemba 1
Kagera Sugar 0 Yanga 1
Coastal Union 1 Ruvu Shooting 0
Ndanda FC 1 Azam FC 0
Mtibwa Sugar 1 Simba 1
JKT Ruvu 1 Polisi Moro 2
Stand United 0 Prisons 1

MABINGWA wa Ligi Kuu Vodacom Azam FC Leo Wameambua kipigo cha pili mfululizo baada kuchalazwa1-0 na Ndanda FC huko Nangwanda, Mtwara.
Wikiendi iliyopita, Azam FC, wakiwa kwao Azam Complex, walichapwa 1-0 na Ruvu JKT.

Huko Kaitaba, Bukoba, Kager Sugar iliifunga Yanga Bao 1-0 kwa Bao la Paul Ngway la Dakika ya 52 na Yanga kumaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada Nahodha wao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa tuhuma za kucheza vibaya.
Nao Simba wameendeleza mwendo wao ule ule wa kutoka Sare Mechi zao zote za Ligi Msimu huu baada ya kutoka 1-1 na Mtibwa Sugar huko Jamhuri, Morogoro.
Simba walitangulia kufunga Dakika ya 35 kwa Bao la Kichwa la Joseph Owino na Mchezaji wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgosi, kuiswazishia Mtibwa kwenye Dakika ya 58.
Huko Mkwakwani, Tanga, Coastal Union waliichapa Ruvu Shooting Bao 1-0 na kuchupa hadi Nafasi ya Pili.
Ligi hii inaendelea hapo Kesho huko Mkwkwani Tanga kwa Mechi kati ya Mgambo JKT v Mbeya City.