Saturday, November 8, 2014

YANGA YAKWEA MPAKA NAFASI YA PILI MBEYA CITY BADO HALI TETE YAPIGWA 1 NA STEND UNITED.


MATOKEO MECHI ZA VPL
Stand United 1 Mbeya City 0       
Yanga 2 Mgambo JKT 0             
Mtibwa Sugar v Kagera Sugar (Mvua yavunja yaleta balaa Mtibwa 1 Kagera 0)             
Azam FC 2 Coastal Union 1                 
Polisi Moro 1 Prisons 0
Katika Mtanange wa Vinara wa Ligi Kuu Vodacom, Mtibwa Sugar, na Kagera Sugar huko Morogoro umevunjika kutokana na mvua kunyesha ambapo Mtibwa wakiwa mbele kwa Bao 1-0 na katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam baada ya kupoteza dhidi ya kagera sugar Yanga leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-0 zikiwekwa kimiani na Saimon Msuva kunako Dakika za 74 na 90 na kuipandisha Yanga hadi Nafasi ya Pili. .
na huko katika Viunga vya Azam Complex, Chamazi Mabingwa Azam FC walifunga mabao yao katika dakika za mwishoni na kushinda 2-1 wakiumana na Coastal Union.
Mabao Azam FC wamefunga Kipre Tchetche Dakika ya 88 kwa Azam FC na Rama kuisawazishia Coastal lakini Shomari Kapombe akaipa ushindi Azam FC kwa Bao la Dakika ya 90.
LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumapili Novemba 9
Simba v Ruvu Shootings             
JKT Ruvu v Ndanda FC
Ijumaa Desemba 26
Simba v Kagera Sugar
Jumamosi Desemba 27
Mtibwa Sugar v Stand United               
Prisons v Coastal Union             
JKT Ruvu v Ruvu Shootings
Jumapili Desemba 28
Mbeya City v Ndanda FC            
Polisi Moro v Mgambo JKT          
Yanga v Azam FC             
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Mtibwa Sugar
6
4
2
0
9
2
7
14
4
Yanga
7
4
1
2
9
5
4
13
3
Azam FC
7
4
1
2
8
4
4
13
2
Coastal Union
7
3
2
2
8
6
2
11
5
Kagera Sugar
6
2
3
1
4
2
1
9
12
Polisi Moro
7
3
2
2
6
7
-1
9
6
Mgambo JKT
7
3
0
4
4
7
-3
9
13
Stand United
7
2
3
2
5
9
-4
9
7
JKT Ruvu
6
2
1
3
5
7
-2
7
8
Ruvu Shooting
6
2
1
3
4
6
-2
7
9
Simba
6
0
6
0
6
6
0
6
10
Tanzania Prisons
7
1
3
3
5
6
-1
6
11
Ndanda FC
6
2
0
4
8
10
-2
6
14
Mbeya City
7
1
2
4
3
5
-2
5

Friday, November 7, 2014

UUZAJI MCHANGANYIKO WA TIKETI MWISHO WIKIENDI HII

Uuzaji mchanganyiko wa tiketi za elektroniki kwenye Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakoma baada ya mechi mbili za wikiendi hii kati ya Yanga na Mgambo Shooting na Simba na Ruvu Shooting zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ligi itasimama kupisha mechi ya Kalenda ya FIFA, mashindano ya Chalenji na dirisha dogo la usajili. Baada ya hapo tiketi zote zitauzwa kwa njia ya mtandao, hivyo hakutakuwepo na vibanda vya kuuza tiketi viwanjani.

MSHAMBULIAJI WA YANGA MRISHO NGASSA RASMI AINGIA KATIKA REKODI AFRIKA.

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Mrisho Ngassa, ameingia kwenye Rekodi rasmi za Afrika baada ya kuibuka kuwa Mfungaji Bora wa CAF Championz ligi Msimu wa 2014 akiwa na Bao 6 akifungana na Wachezaji wengine Watatu.
Wengine waliofunga Bao 6 kwenye Mashindano hayo ambayo ES Setif ya Algeria iliibuka kuwa Mabingwa ni El Hedi Belameiri wa Setif, Firmin Ndombe Mubele wa AS Vita ya Congo DR na Haythem Jouini wa Esperance ya Tunisia.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kuingia kwenye Chati aina hii kwenye Mashindano ya Barani Afrika.
CAF CHAMPIONZ LIGI 2014  
WAFUNGAJI BORA:
Wote Bao 6
@Mrisho Ngasa (Yanga, Tanzania)
@Haythem Jouini (Espérance Tunis)                  
@Firmin Ndombe Mubele (AS Vita, Congo DR)                      
@El Hedi Belameiri (ES Setif, Algeria)                        
Ngassa alifunga Bao zake zote 6 dhidi ya Komorozine ya Visiwa vya Comoro waliyokutana nayo Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI mapema Mwaka huu.
Kwenye Mechi ya kwanza Jijini Dar es Salaam Ngassa alipiga Bao 3 Yanga waliposhinda 7-0 na marudiano huko Comoro, Ngassa tena alipiga Hetitriki Yanga ikishinda 5-1.
Raundi iliyofuata Yanga walikutana na waliokuwa Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri na kubwagwa nje. 
Ngassa, mwenye Miaka 25, Mwaka 2009 aliwahi kwenda kufanya majaribio huko England na Klabu ya West Ham na vile vile huko Marekani na Klabu ya Seattle Sounders Mwaka 2011 na kucheza Mechi dhidi ya Manchester United waliyofungwa 7-0.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MAHAKAMA ZA MWANZO KUAMUA MASHAURI YA KESI ZA ARDHI.

SERIKALI, imezipiga marufuku Mahakama za Mwanzo kuamua mashauri ya kesi za Ardhi kwani jukumu hilo ni la Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya.
Onyo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki, wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama (CCM), lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugola (CCM).
Mbunge huyo ametaka kujua kwanini serikali isitoe kauli na tamko la kuwataka Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo kutopokea kesi hizo na badala yake izipeleke kwenye mabaraza ya ardhi.
Amesema, kukomesha tabia ya mahakama za Mwanzo kuhukumu kesi la Ardhi serikali itawasiliana na Makama za mwanzo ili ziweze kuchukua hatua stahiki katika jambo hilo.
Kuhusu, ucheleweshwaji wa kesi taratibu  zinafahamika kwa wale ambao watakuwa na sababu za msingi lakini mahakama zimekuwa haziahirishi kesi bila sababu yoyote endapo itakuwa kusababu zimeeleweka kamati za mahakimu na za majaji wataweza kufuatilia na kuchukua hatua.

UKATILI KWA WATOTO BADO TATIZO KATIKA JAMII YA KITANZANIA.

MTOTO aliyefahamika kwa jina moja la Rehema Matola mwenye umri wa miaka sita, mkazi wa Airport jijini Mbeya amefanyiwa vitendo vya ukatili na mama yake wa kambo, ambae hakuweza kufahamika.
Vitendo anavyodaiwa kufanyiwa mtoto huyo ni kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake, kisha kung’olewa jino, kujeruhiwa eneo la mdomo na mguuni, pamoja na kuumizwa sehemu zake za siri hali iliyopelekea mwili wake kudhoofu.
Mtoto huyo ambaye mama yake mzazi alikwishafariki dunia amedai kuwa amekuwa akipigwa mara kwa mara na mama yake wa kambo na wakati mwingine na baba yake hali inayomsababishia  majeraha na kisha kumwacha ndani bila kumpatia matibabu mpaka pale majirani walipobaini na kutoa taarifa kwenye uongozi wa serikali za mitaa.
Nae Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Airport,kata ya Ileya bi, Rehema Mohamed amelaani tukio hilo na kusisitiza kuwa sio la mara ya kwanza na ameziomba mamlaka husika kupita mitaani na kwa ajili ya kutoa elimu.
Hata hivyo juhudi za kumtafuta mtuhumiwa huyo hazikuzaa matunda kwani amekimbia mara baada ya tukio hilo.

TFDA:MAMA NTILIE MBEYA WATAKIWA KUBORESHA MAENEO YA KAZI.

MAMLAKA  ya chakula na dawa TFDA, kanda ya nyanda za juu kusini imekiri kuwa mazingira wanayofanyia biashara baadhi ya mamantiliye jijini Mbeya, hayakikidhi viwango vya usafi hali inayoweza kuhatarisha afya za watumiaji wa vyakula.
Hayo yamebainishwa na kaimu meneja wa TFDA, wa kanda hiyo Rodney Analanga wakati akizungumza na Highlands fm radio ofisini kwake.
Analanga amesema kuwa mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua za kisheria mama ntiliye ambao hawafuati kanuni za usafi wa chakula ikiwa ni pamoja na kutumia maji safi na vyombo vilivyooshwa na maji safi na salama.
Kauli hiyo imekuja kufuatia Highlands fm, kufanya uchunguzi kwenye mabanda ya mama ntilie katika eneo la Sido jijini Mbeya na kubaini kuwa wafanyabiashara hao hawakidhi viwango vya usafi wa chakula.

VPL:TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUTOUZWA KWENYE MAGARI

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii ambapo tiketi za elektroniki hazitauzwa tena kwenye magari, hivyo washabiki wanunue tiketi hizo kwenye mtandao au kwenye maduka ya CRDB Fahari Huduma.

Kesho (Novemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutakuwa na mechi kati ya Yanga na Mgambo Shooting wakati Uwanja wa Chamazi kutakuwa na mechi kati ya Azam na Coastal Union. Jumapili ni mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting.

Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Taifa ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 (VIP B na C) wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Mechi za Uwanja wa Chamazi kiingilio ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Mechi nyingine za VPL kesho ni kati ya Stand United na Mbeya City (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Mtibwa Sugar na Kagera Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo ya saba itakamilika Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Ndanda kutoka Mtwara.
Wakati huo huo, mchezaji bora wa VPL kwa mwezi Oktoba, Salum Abubakar wa Azam atakabidhiwa zawadi yake kesho (Novemba 8 mwaka huu) kabla ya mechi kati ya Azam na Coastal Union.