Tuesday, December 2, 2014

CAF YAWEKA HADHARANI MAJINA YA TIMU SPECHO KWA DROO KUPANGWA.

WASHIRIKI 16 wa Fanali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, ambazo zitachezwa huko Nchini Equatorial Guinea kuanzia Januari 17, watajua nani Wapinzani kwenye Makundi yao Leo Jumatano makundi ya Timu 4 kila moja kutajwa kwa ajili ya Droo hiyo na CAF.
Droo hiyo itafanyika Mjini Malabo Nchini Equatorial Guinea.
Timu hizo 16 zimepangwa kwenye Vyungu Vinne vya Timu 4 kila moja na kwenye Droo kila Chungu kitatoa Timu moja ili kupanga Makundi Manne.
CHUNGU 1
Equatorial Guinea, Ghana, Zambia, Burkina Faso
CHUNGU 2
Ivory Coast, Mali, Tunisia, Algeria
CHUNGU 3
Cape Verde, South Africa, Gabon, DR Congo
CHUNGU 4
Cameroon, Senegal, Guinea, Congo

POLISI MORO NA MWADUI FC ZAMTOLEA MACHO KINDA MIRAJI ADAM LA SIMBA

Timu Polisi ya Morogoro na Mwadui FC ya Shinyanga zimewasilisha barua kumuomba beki wa pembeni Miraj Adam wa Simba SC kwa mkopo baada ya kushushwa Simba B.
Polisi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inapambana na Mwadui FC, inayopigania kupanda Ligi Kuu pia kuwania huduma za beki huyo aliyetokea timu ya vijana ya Wekundu hao wa Msimbazi.
Mwadui wanaamini wanaweza kumpata kwa urahisi beki huyo kwa sababu ya mahusiano mazuri ya kocha wao, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na klabu ya Simba SC.
Lakini Polisi nayo inaamini inaweza kumpata kwa urahisi beki huyo wa kulia, Miraj, kwa sababu inacheza Ligi Kuu kwa sasa na Morogoro si mbali sana na Dar es Salaam anakoishi mchezaji huyo.

Kwa sasa, Miraj ameshushwa kikosi cha pili baada ya mechi saba za awali za Ligi Kuu, lakini Simba SC bado haijaamua kumtoa kwa mkopo hadi hapo itakapofanikisha kusajili mchezaji mwingine wa nafasi hiyo.

VITA KALI YA BALLON D"OR MESS VS RONALDO VS NEUER JAN 12/2015.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza orodha ya wachezaji watatu watakaogombea tuzo ya mchezaji ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia maarufu kama Ballon d’Or. 
Wachezaji hao watatu waliopenya katika mchujo wa wachezaji 23 ni pamoja na nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo, Lionel Messi wa Argentina na klabu ya Barvelona na Manuel Neuer kutoka Ujerumani na timu ya Bayern Munich.
Sherehe za utoaji tuzo inatarajiwa kufanyika Januari 12 mwakani huku Ronaldo akiwa ndio mshindi wa mwaka jana. Kwa upande wa wanawake walioteuliwa kugombea tuzo hiyo ni pamoja na Nadine Kessler wa Ujerumani, Marta wa Brazil na Abby Wambach kutoka Marekani. 
Kwa upande wa makocha walioteuliwa kugombea tuzo ni pamoja na Carlo Ancelotti wa Real Madrid, Joachim Loew aliyeiwezesha Ujerumani kunyakuwa Kombe la Dunia na kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone.

Monday, December 1, 2014

WATOTO OBAMA VITUKO NDANI YA SKENDO CHAFU YA MAVAZI YA UWAZI.TAZAMA PICHA ZOTE HAPA

 


Rais Barrack Obama na wanawe Sasha na Malia. Afisa mmoja wa chama cha Republican amewakosoa mavazi yao.Watoto wa rais wa Marekani Barrack Obama, Sasha na Malia wameshtumiwa kwa kukosa heshima na afisa mmoja wa chama cha Republican baada ya kuhudhuria sherehe za kutoa shukrani.
Elizabeth Lauten ,ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano wa mbunge Stephen Fincher alitoa matamshi yake katika mtandao wa 
facebook
 ambayo baadaye yalifutwa.

Baada ya kukosolewa Bi Lauten aliomba msamaha kwa kutoa matamshi hayo ya kukera.

Aliku akikosoa sketi fupi zilizovaliwa na wasichana hao wa Obama.Bi Lauteni 
pia
 aliwashtumu wasichana hao kwa kuonyesha uchovu wakati waliposimama na baba yao katika sherehe hiyo ya ikulu ya Whitehouse.

YACINE BRAHIMI ATWAA TUZO YA BBC YA UCHEZAJI BORA MWAKA HUU

Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika BBC mwaka huu amepatikana. Baada ya maelfu ya kura kuhesabiwa, mchezaji wa Algeria na nyota wa Porto, Yacine Brahimi ndiye mshindi wa mwaka huu.
Hapajawahi kutokea katika miaka 23 ya historia ya shindano hilo kwa mchezaji bora kutoka Algeria kuishinda, lakini Brahimi amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya mwaka uliokuwa na mbwembwe wa 2014.
Aliingiza bao la ushindi dhidi ya mabingwa wa Hispania Barcelona, bao lengine la kisasa katika ligi ya mabingwa wa ulaya na kisha kuwa katika msitari wa mbele wakati nchi yake iliposonga mbele katika michuano ya kombe la dunia.
Hio ilikuwa historia kwa Algeria kufika katika awamu ya muondoano katika dimba hilo.
Hii bila shaka ilikuwa nafasi nzuri kwa mashabiki wa BBC pamoja na wapenzi wa soka kumchagua kama mchezaji bora zaidi wa Afrika mwaka huu.
Aliwapiku wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast na hatimaye Yaya Toure - aliyenyakua ushindi mwaka jana.

EMERSON KIUNGO MBRAZIL ASAINI MKATABA MWAKA MMOJAYANGA

Kiungo Emerson De Oliveira Neves Roque leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Young Africans baada ya benchi la ufundi kuridhika na uwezo wake,na mchezaji mwenyewe kufikia makubaliano hayo ya kuwatumikia watoto wa Jangwani.
Baada ya kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo chini ya makocha Marcio Maximo, Leonardo Neiva na makocha wazawa Salavatory Edward, Shadrack Nsajigwa kwa pamoja wameridhiswa na uwezo wake na kuomba apewe kandarasi la kuitumikia klabu ya Young Africans.
Emerson aliyekua akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye jimbo la Rio de Janeiro anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" ambaye ameshindwa kureje nchini kutokana na matatizo ya kifamilia na kuomba klabu ya Young Africans imuache.
Kocha wa Young Africans Marcio Maximo amesema wamerizishwa na uwezo na kiungo mkabaji Emerson na kusema ataisaidia timu katika michuano mbali mbali ya Ligi na Kimataifa.
Ujio wa Emerson unafanya klabu ya Young Africans kufikisha jumla ya wachezaji watano wa kimataifa, wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey Coutinho.

SERIKALI YASEMA NI WAJIBU WA KILA SEKTA KUANDAA WATENDAJI WAO KWA KUWADHAMINI KATIKA MASOM

SERIKALI imesema ni wajibu wa kila sekta kuandaa watendaji wao kwa kuwadhamini katika masomo.
Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia habari na masiliano (Tehama) kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dokta Ally Simba, amesema hayo katika hafla ya kutoa tunzo za udhamini kwa masomo ya Tehama kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka 2014/2015.
Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Ubungo jijini Dar es Salaam.
Dokta, Simba amesema kuwa ni mara ya nne kwa TCRA kutoa udhamini kwa elimu ya juu hasa kwa wale wa Tehama lengo ni kupata faida katika kizazi hiki na kijacho kikiwa na uelewa wa hali ya juu.