Kiungo Emerson De Oliveira
Neves Roque leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Young
Africans baada ya benchi la ufundi kuridhika na uwezo wake,na mchezaji mwenyewe
kufikia makubaliano hayo ya kuwatumikia watoto wa Jangwani.
Baada ya kufanya mazoezi kwa
siku nne mfululizo chini ya makocha Marcio Maximo, Leonardo Neiva na makocha
wazawa Salavatory Edward, Shadrack Nsajigwa kwa pamoja wameridhiswa na uwezo
wake na kuomba apewe kandarasi la kuitumikia klabu ya Young Africans.
Emerson aliyekua akichezea
katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye jimbo la Rio de Janeiro
anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" ambaye
ameshindwa kureje nchini kutokana na matatizo ya kifamilia na kuomba klabu ya
Young Africans imuache.
Ujio wa Emerson unafanya
klabu ya Young Africans kufikisha jumla ya wachezaji watano wa kimataifa,
wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey
Coutinho.